Na.Honorius Mpangala
MABADILIKO ya bechi la ufundi
katika klabu yoyote huja na matokeo chanya na hasi kulingana na mwenendo wa
timu au klabu kwa ujumla.Katika hilo kuna mambo huenda yakawa tofauti kwa
wachezaji walioonekana kupata sana nafasi kabla ya mabadiliko.Unayakumbuka
maisha ya mchezaji wa Chelsea John Mikel Obi baaada ya kutumuliwa kwa Jose
Mourinho pale klabuni.Ujio wa Guus Hindik ulirudisha kwenye hali ya kupata
nafasi hadi kufikia hatua ya mashabiki wa kitazania walimpachika jina la Ombeni
Sefue.
Kupachikwa kwa jina la Ombeni
Sefue kwa Obi kulitokana na jinsi alivyoonekana kutotumika wakati wa Mourinhona
alipofika Hidink akaanza kumpa nafasi.Hii ilifananishwa na Sefue wakati wa
utawala wa awamu ya tano alivyokuwa hasikiki katika serikali hadi ilipoingia
serikali ya awamu ya tano.
Mabadiliko ya makocha yanakuwa
yenye kuleta mabadiliko katika vikosi kutokana na kila kocha hupenda kuja na
falsafa zao.Hili ndilp lililomkumba mchezaji fundi wa mpira aliyepita katika
mashamba ya miwa pale Manungu Turiani Mohammed Ibrahim.Hadi klabu ya Simba
inafikia hatua ya kukubali uwezo wake na kumsajili ni kutokana na kile
alichokuwa akikifanya akiwa na klabu ya Mtibwa Sugar.
Simba waliamua kufanya usajil
ulijumuisha wachezaji watatu kwa pamoja toka Mtibwa sugar yaani waliwasajili
Mzamiru Yassin,Shiza Kichuya nay eye Mo Ibrahim ambao walikuwa mhimili mkubwa
wa klabu hiyo yeneye maskani yake katika mashamba ya miwa Manungu Turiani.
Wajihi wa Mo Ibrahim ilikuwa
mija ya kumfanya natofuatiane na wenzake kimwinekano kwani alikuwa kafuga rasta
hivyo kwa uwezo wake ilikuwa ni kitu chepesi kutambua uwezo wake kwani
alionekana sana.Lkini hali imekia tofauti sana mara tu alipotua katika klabu ya
Simba.Hatumwoni tena uwanjani mara kwa mara,sio kama uwezo wake umepungua
hapana ila ni matumizi ya mbinu za kisoka ambazo kocha anaweza kuona kuwa watu
Fulani wananifaaa katika mbinu hii na hawa hawanifai katika mbinu hii.
Wakati wa usajili wa dirisha
dogo msimu huu ziliibuka tetesi za yeye kutaka kuondoka katika klabu hiyo ili
akapate muda wa kucheza katika klabu nyingine na alinde kiwango chake.Hii
ilitokana na tangu ujio wa Joseph Omog kulifanya Mo awe na muda mchache sana wa
kuonekana uwanjani akicheza tofauti na ilivyo kuwa kwa Jackson Mayanja wakati
huo anainoa simba kama kocha mkuu.
Omog alifanya Mo awe anayepata
muda mcheche na baadae kutomtumia kabisa pale alipokuja kocha msaidizi mwingine
Masoud Djuma Irambonaimana.Madiliko ya klbu ya simba ya kumtimua kazi Omog na
kucha mikoba kwa Irambonaimana kukafanya Mo apotee kabisa katika kikosi. Hii ni
kutokana na machagulio ya kocha katika kufanikisha mbinu zake za
kimpira.Kupotea kwake kumefanya aibuke Nickolas Gyan ambaye alionekana kutopata
nafasi mbele ya mtamgulizi wa Irambonaimana.
Licha ya kwamba hali hiyo
imeweza kumkuta hata mchezaji Mohammed Hussein lakini yeye ni kutokana na
kuletewa msaidizi wake ambaye kaja na akafanya vyema sana. Kumbuka Zimbwe jr
ndiye aliyekuwa amecheza mechi zote za simba msimu uliopita akifuatiwa na
mkongomani Javier Besela Bukungu.Sasa benchi laufundi lilikuwa na haja ya
kumlrata msaidizi wake ndipo walipomsajili Erasto Nyoni n baadae wakamleta pia
Asante Kwasi.
Utofauti wa Mo na Mohammed
Hussein unatokana na kile kinachoonekana kuwa kiungo huyo hana nafasi ya kucheza
wakati hata kuipata hiyo nafasi ya kuwaaminisha mashabikia na wakarizika na
kinachofanywa na benchi la ufundi wakione kiko sahihi.
Kwa idadi yao kama walivyoka
Mtibwa sugar nyota ilikuwa imeng’ara kwa Shiza Kichuya na Mzamiru licha ya
kwamba nae kwa sasa amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza dakika
zote kama ilivyo kuwa awali kutokana na uwepo wa kiraka James Kotei na Nyoni
ambao wanlifanya nechi na ufundi kuina lina uwanja mpana wa kuchagua kikosi
kulingana na uwezozwa wachezaji ambaounakuta wanacheza nafasi zaidi ya moja
uwanjani.
Ujio wa kocha Pierre Liechantre
kumefanya Mo azidi kupotea machoni kwa wapenzi wa klabu ya simba kutokana na
kuwepo kwa mwendelezo wa kutopata nafasi ya kucheza.Iliwahi kumkuta mchezaji
Paul Nonga ambaye alitoka Mwadui na kujiunga na klabu ya Yanga na akawa na
ufinyu wa kuapata nafasi ya kucheza.Alisajiliwa dirisha dogo kwa mkataba wa
miaka miwili lakini aliitumikia Yanga kwa miezi sita na akawepo katika kikosi
kilichoipa yanga ubinwa na baadae akaomba kuondoka na uongozi ukaridhia kwa
matakwa yake aliyoeleza.Unaweza kusema alioogopa kupigania namba lakini
kiuhalisia alienda Yanga huku wakiwa na wachezaji wanaocheza eneo la
ushambuliaji kama Donald Dombo Ngoma,Amis Jocelyn Tambwe,Obrey Cholla Chirwa
ilikuwa ngumu kwake kupenya kwa washambuliaji hao na akaanza badala yao.Maamuzi
aliyoyafanya ilikuwa kwenda katika klabu ambayo atapata muda wak kucheza kuliko
Yanga.
Mo ukiinuka hapo katika benchi
au huko jukwaani na kujipukuta vumbi na kwenda zako mahala pengine hutoonekana
mjinga bali utakuwa umetoa maamuzi ya kiume na yenye kila chembe chembe ya
mafanikio. Ni ngumu sana kufanya maamuzi kuziacha hiziz timu za kariakoo lakini
yawezekana matunda ambayo utayapata baada ya nkwenda utakako ona watatunza
kipaji chako basi utafurahia. Nyakati zote ni ngumu kufanya maamuzi kuondoka
unapopapenda lakini uhalisia wa kama ulikuwa sahihi kutoka au kuto kutoka
utakuja kuona ukiwa nje ya hapo.
Kwa uwezo wa Mo sio mchezaji
wakukosa nafasi uwanjani kwani anaweza kama kutumika kama kiungo wa pembeni
akiwa na jukumu la kusaidia kiungo cha kati,pia anamudu kucheza nyuma ya
mshambuliaji na hata kiungo mchezeshaji.Kama unakumbuka katika klabu ya Mtibwa
kiungo cha chini na juu walisimama Shaaban Nditi na Mzamiru Yassin na kulia na
kushoto ndiko walikocheza Mo na Kichuya.
Katiika klabu ya simba alikuwa
akitumika hivyo hapo awali lakini ujio wa Haruna Niyonzima ukafanya lile eneo
ambalo yeye alilicheza kwa ufasaha linachezwa pia na mnyarwanda huyo.Hali hiyo
ikafanya Mo kuwa na hatiahti ya kucheza kila mchezo,majeruhi ya Niyonzima
hayaweza kumpa tena nafsi kwani tayari kwani Saidi Ndemla kashika kasi hivyo
kutokana na uwepo wa viungo wengi na simba wanakawaida ya kupenda soka lakuoiga
psi nyingi inawafanya wawe na winga mmoja tu asilia na winga nyingine kuchezwa
na mtu wa kiungo kama ilivyo kwa Ndemla anavyofanya.
Wako wachezaji wengi
walioonekana kutokuwa na lolote katika klabu ya Simba lakini walipoenda
kwingine wakarejesha ukali wao.Ilitokea kwa nahodha wa Mtibwa Shaaban Nditi
alisajiliwa simba lakini mambo hayakumyokea akarejea Manungu hadi leo
anaendelea na soka lake.Pia mmoja wa wafungaji bora wa ligi kuu ya Tanzania
Abdallah Juma alitokaMtibwa kwenda Simba hakuweza kufanya lolote ndani ya
wanamsimbazi akaamua kurejea tena shambani manungu na akarejesha ukali wake
uleule.Hivyo kuna kila sababu ya kujitazama tena upya kwa Mo Ibrahim ili alinde
kipaji chake.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako