NA.HONORIUS MPANGALA
MAISHA popote unaweza kusema hivyo kwani
waliofikiria katika hoja hii walikuwa na sababu za msingi zilizokuwa na maana
kiuhalisia. Wakati kipato ndio sababu hasa zilizopelekea kukawa na maneno kama
haya ambayo yanasadifu uhalisia wa maisha. Katika mazungumzo yangu na mmoja ya watanzania
waishio nchini Afrika kusini ilinifanya nistaajabu kile anachonieleza ambacho
ndio uhalisisa wa maisha ya huko.
Ni rafiki yangu na ndugu yangu Joseph Boimanda
alinifanya nistaajabu pale aliposema mtaji wa milioni hamsini za kitanzania
ukiwa Afrika Kusini sio lolote kwa serikali ya huko. Maisha yamekuwa yenye uhuru
na amani ya kutosha kwa raia.
Wakati nataka kuyajua haya ananieleza kuwa
mamlaka ya mapato ya huko haina muda wa kufuatilia mfanyabiashara wa kati.Kama
inatokea mtu anataka kulipa mapato serikalini basi ni hiari yake,hii ni kwa
wale wafanyabiashara wadogo na wa kati amabao mtaji yao ni kitu kidigo kwa
serikali yao.
Moja ya kauli yake ambayo inaingia katika masikio
yangu na najikuta natumia akili nyingi kutafakari ni pale aliposema kuwa
siwezi kurejea haraka huko nyumbani. Ananieleza hakuwahi kufanya shughuli akiwa
hapa nyumbani na akaweza kupata pesa ya kitanzania milioni moja na
akaishika.Lakini anasema kama naweza kufanya shughuli zangu huku ugenini na
niweza kupata kiasi cha milioni kumi za kitanzania zangu kwanini nirudi sasa.
Ukitafakari sana hoja za Boimanda unapata
uhalisia wa wale wapambanaji wa maisha ambao wanafanya hivyo wakiwa mbali na
nyumbani. Watu wenye malengo katika utafutaji siku zote
wawapo ugenini jicho lao linakuwa katika kulinganisha kipato anachoweza kupata
sehemu moja na akakitofautisha na sehemu nyingine.
Hiki ndicho ambacho kinanipa majibu ya kwanini
kijana huyu aseme sitoweza kurejea sasa. Katika utafutaji maisha kitu namba moja tunaweza
kukitaja mtu ambacho anapaswa kuwa nacho ni uthubutu ten ulio wa hali ya
juu.Hiki ndicho ninachoweza kukisema kipo kwa wale ambao wamechagua njia Fulani
ya maisha yenye utofauti na ujamaa tuliouzoea.
Nini kinakujia kichwani kwako raia wa nchi jirani
anakuambia sina mpango wa kwenda nyumbani kwetu sasa kwani hapa natafuta kwa
uhuru na pesa inapatikana sana. Hakika katika mtazamo wa haraka utaweza kujivunia
moyoni kuwa mwenendo wa nchi yako umekuwa na kivutio kwa wageni kwani wenyewe
wanakili juu ya yale yanayoendelea hapa.
Boimanda hilo ndilo analoniambia kuwa Durban
maisha yamekuwa kama anaishi nyumbani Nyasa. Anafanya yale yaliyompeleka kwa
amani na uhuru kubwa. Anakiri changamoto hazikosekani popote duniani
katika suala la utafutaji maisha lakini kile kinachoendelea kwake kinamfanya
aamue kuisafirisha hadi familia yake kwenda huko aliko.
Licha ya kuwepo kwake mbali lakini amekuwa
akifuatilia kila jambo la huku nyumbani Tanzania.Wakati mwingine yeye ndio
amekuwa mtu wa kuniuliza juu nya jambo ambalo hata mimi niliyeko nchini
sijasikia. Hii inatokana na yeye kuwa msikilizaji wa radio
za kitanzania kwa njia za kimtandao na pia mtazamaji mkubwa wa vituo vetu vya
luninga kwa njia hiyo ya kimtandao hivyo humfanya kuwa na kila taarifa ya yale
yanayoendelea hapa nyumbani.
Hebu katika mtazamo wa kawaida unafanya biashara
ambayo mtai wake ni kamafedha za kitanzania milioni hamsini halafu mamlaka ya
mapato hawana habari na wewe nini kinajengeka kichwani kwako juu ya hili. Rand 100 ni sawa na pesa yetu ya kitanzania
shilingi 17000 ina maana katika mtaji wa mfanyabiashara wa milioni
hamsini za kitanzania tulizosema ambazo hata mamlaka ya mapato hawakufuatilii
na kutambua kama unaliingizia taifa kipato ni sawa na rand 294117.647.
Sasa anakuambia kiasi hicho unaweza kukikusanya
kwa muda wa miezi kuanzia tisa hadi mwaka. Ananikumbusha moja ya simulizi la
mchezaji aliyekuwa na asili ya Nigeria kuwa aliapa kutorejea kwao kama hana
chochote.
Aliyaeleza haya akiwa anatafuta timu ya kuchezea
soka nchini Israel hivyo alisema aheli nife nikiwa natafuta kuliko kurejea
Nigeria nikiwa sina chochote.
Wenye mitazamo kama hii ni wachache na huenda
wakawa na haya kutokana na sababu za kifamilia au uchumi wa nchi.
Kama mjuavyo utulivu wa mahali popote ndipo
panapoweza kufanya maendeleo yakafanyika kwa kiasi kikubwa na kwa kasi
pia.Itazame Rwanda ya mwaka 1994 ndio hii ya leo? Yote yaliyotokea ni kwasababu ya utulivu kwa raia
ambao hutoa mwanya wa wananchi kuwa na busy na shughuli zao za kila siku.
Vitisho kwa raia na kuwapo kwa hofu ndiko kunako
fanya maisha ya mwanachi mmoja kuishi kifukara kwa hofu ya matukio ya
kiujambazi au hata yale yanayoweza kutokea kwasababu kisiasa.
Kutokana na dunia kuwa kama kijiji hivyo binadamu
wamebadilika sana kimitazamo. Mitazamo hiyo isiweze kuwafanya watu wakashindwa
kuenzi yale ambayo yalizoeleka kufanyika kwa sisi kama jamii na badala yake
hufanyika kwa hofu kwasababu ya maagizo wanayopewa watu.
Pale ambapo tuliamini ndio kimbilio la wasio na
kwao dhana hii imekuwa ikibadilika kutokan nay ale yanayokuwa yakitokea. Tulikumbwa
na tatizo la watu wasiojulikana katika wilaya ya mkuranga lakini askari wetu
walikuwa makini hadi kuhakikisha hali ile inatulizwa na kuitokomeza kabisa.
Licha ya kufanikiwa katika hilo,upande wa pili wa
kimtazamo mambo yamekuwa tofauti juu ya siasa za nchi hii. Hili nalo linaweza
likawa sababu ya kuwafanya watu wakaona ni heli nikafie ugenini nikiwa natafuta
kuliko kuwepo nyumbani ambapo tunasema pana kila kitu ila kilichopo mioyoni mwa
watu ni hofu dhidi yali ya matukio yanayoendelea kufanyika na kutokea kama
kutekwa na kupotea kwa watu.
Tuna kila sababu ya kuirejeshea hali ya kujiamini
na kuondokana na hofu ambayo inazunguzka katika vichwa vya watanzania wengi. Hofu
hii iko ndani na hata kwa wale wanao kaa nje kwani maswali ya kujiiuliza
yamekuwa mengi na yakakosa majibu.
Cerakote Titanium - Tantric Artworks - Titanium
ReplyDeleteCerakote Titanium. A Tantric titanium price per ounce artworks sculpture titanium knee replacement that contains copper and platinum. The painting titanium nail is based on the Tantric and titanium trimmer is of the highest does titanium set off metal detectors quality.