NA ALBANO MIDELO, NYASA
NYUMBA 25 zilizokuwa na kaya 65 ambazo zilijengwa katika
hifadhi ya msitu milima ya Ruhekei katika Halmashauri ya Nyasa mkoani Ruvuma
zimebolewa na kuondolewa ndani ya hifadhi hiyo.
Afisa Maliasili na Utalii wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
Bugingo Bugingo amesema zoezi la kubomoa nyumba hizo katika hifadhi hiyo limedumu
kwa miaka mitatu na kwamba zoezi limefanyika kwa amani na utulivu kwa njia ya
kidiplomasia hadi wananchi hao walipoamua wenyewe kubomoa nyumba zao na
kuondoka hifadhini mwezi Agosti 2017.
Hifadhi ya msitu wa Ruhekei yenye ukubwa wa zaidi ya hekari
2000,ndiyo hifadhi kongwe kuliko zote katika katika mkoa wa Ruvuma ambayo
ilianzishwa rasmi na kutangazwa katika gazeti la serikali ya kikoloni mwaka
1938.
Hifadhi hiyo ni muhimu kwa sababu ni chanzo muhimu cha maji
ukiwemo mto Ruhekei ambao unamwaga maji yake ziwa Nyasa.Mto huo pia ni mazalia
muhimu ya samaki aina ya ngisi na mbelele.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako