September 25, 2017

MAPIGANO YAENDELEA KATI YA WANAMGAMBO WA MAIMAI NA JESHI LA TAIFA

MAPAMBANO MAKALI yanaripotiwa kati ya jeshi ya Congo FARDC na waasi wa maima wa YAKUTUMBA katika maeneo ya wilaya ya Tanganika tarafani fizi, Katika mkoa wa Kivu ya kusini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Taarifa zenye uhakika zaeleza kuwa waasi hao wamevizibiti vijiji kadhaa ikiwemo mji wa Mboko.
 
Hofu na wasiwasi unazidi kutanda kwa raia wamaeneo ya Lusenda,mboko ,a hata SWAIMA ambapo jeshi lataifa FARDC linakabiliana na wapiganaji wa kundi la Maimai CNPS linaloongozwa na Yakutumba. Duru zenye kuaminika zaeleza kuwa makabiliano yalianza hio jana mapema alfajiri,wakati wapiganaji hao wa maimai waliposhambulia ngome kadhaa za jeshi la taifa katika mji wa Mboko na kuuzibiti. 


Kumekuwa na taarifa kwamba wapiganaji hao wameteka vijiji vingine ikiwemo Kabumbe,Swima,na Munene ,Lakini Serekali upande wake imekanusha kuwempo Taarifa hizo, nakusema kwamba maeneo hayo yako chini ya ulinzi wa Jeshi la taifa. Hata hivyo,mashirika ya kiraia imeziomba mande zote mbili kukaa kwenye meza ya mazungumza,ilikuepusha raia na athari zinazo weza kutokea.Lusambya wa numbe ni kuongozi wa mashirika ya kiraia Tarafani Fizi. 

Kumekuwa na hali ya ukosefu wa Usalama katika maeneo mengi ya mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo,kutokana na mapigano ya mara kwa mara kutoka kwa makundi ya waasi dhidi ya vikosi ya jeshi la taifa. 

Maelfu ya wakaazi hulazimika,kuyaama makwao na kusababisha wengine wengi kupoteza maisha yao,alkadhalika kusababisha uporaji wa mali na vitu vya samani.

©RNAFIZI

No comments:

Post a Comment

Maoni yako