Jana
mchana mwendesha Baiskeli alipita kwa kasi katika makutano ya barabara ya Bibi
Mohammed na Morogoro bila kuruhusiwa na taa za kuongoza magari. Wakati anapiga
taa zilionyesha magari yapite, na yalikuwa yakipita kwa mwendo kasi mno, kiasi
kwamba ingetokea gari linalopita basi angegongwa na kusababisha matatizo
makubwa.
Wakati
akivuka eneo hilo upande wa pili alikuwepo askari wa barabarani ambaye alikuwa
ameinamia simu yake kana kwamba hafuatilii kinachotokea kwenye eneo la kuvukia
lenye mistari ya pundamilia. Baada ya mwendesha baiskeli huyo kuvuka, askari
aliona ni kitendo cha hatari kwa kijana huyo, hivyo akamkamata upesi. Adhabu aliyompa
ni kutoa upepo wote kwenye tairi la nyuma la baiskeli, hali iliyofanya kijana
huyo aduwazwe.
Askari alichukua uamuzi sahihi kumlinda mwendesha baiskeli na
kuonyesha funzo kwa wengine wanaohatarisha maisha yao. Kijana huyo aliondoka
kimya kimya huku akikokota baiskeli yake.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako