KWA maana nyingine, Kama una mtoto chini ya miaka minne unataka kutoka 'out' kula kwenye hiyo restaurant basi inabidi usiende naye inabidi umfungie ndani au utafate baby sitter au uahirishe. Hayo ni mashariti ya restaurant ijulikanayo kama Milan iliyopo , katikati ya mji wa Geneva eneo la Paqui ambalo linajulikana kama eneo lililochangamka kuliko sehemu nyingine yoyote mjini Geneva. Ukiuliza sababu za kutoruhusu watoto unaambiwa : "Baby strollers" Zinachukua nafasi kubwa kwa wateja wengine.
Ulaya wako zama ambazo mtu hufikiria mara kumi kumi kabla ya kuamua kuzaa, si tu kwa sababu ya gharama , la hasha bali jamii isiyorafiki kwa watoto. Hhii imesababisha gap kubwa kati ya wazee na vijana ( kuna wazee wengi na vijana wachache sana). Watu hawataki kuzaa kabisa kwa karaha kama hizo.
Kuna shuhuda nyingi ambako mwanamke akiwa na mtoto anabaguliwa kazin . Kuna siku nilikuwa kwenye tram naenda kazin hapa Geneva, akaingia mama akisukuma mtoto wake kweye stroller abiria mwingine akaonekana kununa na kumkasirikia yule mama eti stroller yake inachukua nafasi kwenye tram.
Hapa ndipo tulipofikia.Mbaya zaidi divorce rate ni kubwa sana, na kama mama ana mtoto lakin hana mume ndio maisha yanakuwa magumu sana . Single moms ulaya hata kudate ni issue, wanaume wengi wanawaepuka na kuna sababu rational wanazito (sijui kibongo iko vipi hii). Matokeo watu hawana furaha, wengine wana msongo wa mawazo, wengine hadi kujinyonga, ni sababu kama hizo.
Hivi kweli mtu unamchukia mtoto unategemea maisha yako utakuwa na amani, hata kama ungekuwa millionea? At some point ulikuwa mtoto pia , kama ungechukiwa pengnepo usingekuwa hapo ulipo.Kama hupendi watoto na hutaki kuzaa , kaa kimya acha wengine wazae. na usivute midomo ukiona mtu ana mtoto. Hata afrika ambapo watu wanazaa watoto weng bado tunawapenda na tunafuraha kuona watoto , lakin ulaya ambako waliowengi wana mtoto 1 lakin bado hawapendi watoto. Nimechokaaa.
©LAST LAJA
No comments:
Post a Comment
Maoni yako