September 15, 2017

MWANDIKO WAKO NI UPI?



Kila mwandishi wa kitabu anatakiwa kuwa mwandiko wake rasmi. Mwandiko huo humtambulisha mwandishi kila kazi yake inapochapishwa na kuingizwa sokoni. Hiyo inatusaidia sisi wasomaji kutambua mwandiko wa mwandishi husika.

Na mwandiko huo upo kwenye “Font Style”. Uchaguzi mzuri wa mwandiko unamfanya mwandishi kuuza kazi zake kwa mwandiko rasmi.

 
Aidha, mwandiko huo hubeba alama ya mwandishi husika, bila kubadili badili ‘Font Style’. Mathalani, mwandiko wa mwandishi Fadhy Mtanga unafahamika. Tazama vitabu vyake utagundua ana “Font Style” rasmi inayokaa vema kitabuni.

Pia jina la mwandishi linatakiwa kuwa na ukubwa unaoonekana siyo mdogo kama ‘byline’ ya gazetini. Jina lako ni biashara, lazima lionekane kuwavutia zaidi wasomaji kama sisi tunaopenda kutemea mate kidoleni na kufunua ukurasa unaofuata. Mwandiko kama huu kitabuni unafaa kuendelezwa na ndugu mwandishi wa riwaya hii. Ni mwandiko mzuri.

©Markus Mpangala

No comments:

Post a Comment

Maoni yako