"Aya zilizopo katika msahafu wa Shetani ni kutafuta
walio wasafi na kuwaingiza kwenye uchafu. Haziangalii hulka au usomi wa mtu.
Kumbuka, Vivi naye ni mke wa mtu! Kama ameshindwa kuziona dhambi zake, hawezi
akaziona anazomfanyia mwingine," alisema Lucas na kusisitiza Judith
amekuwa msagaji kama Mama Jenifer na Vivi. (uk.182).
MAHABUSU
Mahabusu yote ilinuka harufu nzito yenye jasho la watu
wasiooga, mikojo na hata vinyesi. Kwa hali halisi Mahabusu yote ilinuka Kutuzi,
alisema George (uk.199).
Kiburi cha Judith kinaendana na simulizi nyingine ya
"DHIHAKA" iliyoandikwa Beka Mfaume.
WATU.
Katika maisha kuna watu wanaweza kukulaghai, kukuyumbisha,
na kulinda maslahi yao kwa staili ya "ACACIA". Najua nakuibia ila ni
sheria zako (akili zako) sio Mimi. Mtu anajua anakuharibu lakini hajali juu ya
hatima yako. Subira ni jambo muhimu sana kuwajua wadanganyifu. JILINDE.
©Markus Mpangala,
No comments:
Post a Comment
Maoni yako