September 15, 2017

UTUNZI WA FADHY MTANGA

NA MARKUS MPANGALA

KIMSINGI huyu bwana ni rafiki yangu sana tena kwa miaka mingi mno. Katika maisha ya kawaida mtu akifuatilia humu mitandaoni utadhani tumekwazana, kumbe walahi hata chembe. Ni sehemu ya burudani tu.
 
Tugeukie huku!
Mojawapo ya vitu vinavyonivutia ni namna anavyotengeneza wahusika wake kwenye simulizi zake zote anazozitoa. Umahiri wa Fadhy Mtanga ni namna anavyoumba tabia ya mhusika wake kwenye kila riwaya anayoandika. Kila mhusika anakuwa na tabia fulani ambayo inakuwa haieleweki kwa wengine au inakuwa utambulisho.

Zedi alikuwa na kiburi fulani na hulka ya kutotaka kutekeleza ushauri. Tabia ya Zedi ilikuwa kama chuma, lakini kuna wakati alikubali yaishe. Ile tabia ya Zedi kila nikifikiria na kumtazama Fadhy huwa ninacheka sana.


Kwa mfano kuna tukio moja la Zedi kukamatwa na Askari barabarani kwa kuzidisha mwendo. Jinsi Zedi alivyokuwa akizungumza na yule askari, ikanikumbusha siku moja tukiwa maeneo ya Bamaga na bwana Fadhy. Yaliyotokea yamebaki kuwa kicheko.
Aghalabu wahusika wa riwaya za Fadhy wanakuwa na tabia fulani za kipekee. Ufundi mkubwa wa Fadhy ni namna anavyoumba tabia za wahusika wake. Wahusika wake wanakuwa na kitu tofauti kabisa, na kitabu kinapomalizika unagundua kuwa kila mmoja anakuwa na tabia zake.

Chukulia mfamo Justine alikuwa mcheshi, lakini ni mtu aliye bize sana na shughuli zake. Wakati mwingine ule UBIZE wa Justine hunikumbusha Fadhy mwenyewe jinsi alivyo na majukumu yake. Hahahaaaaaaaaa!

Njoo wa Tony, ni kijana mpole na mwenye wajihi wa kupendeza. Tabia aliyoumbiwa Tony ni uvumilivu, lakini naye ni binadamu kama wengine (ingawa wa kusadikika). Tabia aliyoumbiwa Tony ni uungwana, mpambanaji wa maisha na mpiganaji wa kimya kimya (moyoni). 

Hapa napo namkumbuka Fadhy mwenyewe huwa nacheka pia. Hahahaaaa!
Kuna mstari unasema kuwa PENZI la askari linakuwa na amri amri tu bila masikilizano. Hapa Fadhy alijaribu kuumba tabia ya aina ya mapenzi. Ni aina nyingine ya ufundi wake wa kuumba tabia za vitu au jambo. Ni upekee wa mwandishi huu. Ni kama vile amenikumbusha mambo yangu ya zamani. Loooooh kwakuwa anayajua!

La nyongeza ni kwamba Fadhy mwenyewe anao uzoefu juu ya eneo hilo na amri amri za askari. Nina uhakika kabisa kabisa kwamba Fadhy ameandika mistari juu ya penzi la askari lenye amri kwakuwa anao uzoefu binafsi kwani amewahi kuwa mahusiano na kachero wa kike.

Baba yake Noella pia anawakilisha tabia nyingine ya wahusika wa Fadhy. Ameumbiwa tabia ya usikivu, na mvumilivu licha ya kushambuliwa na upande wa baba yake Justine.
Kwa namna nyingine Fadhy Mtanga amemuumba mama Justine kama akina mama wa kileo au wale 'wenye tabia za kishangingi', wasiokopesha maneno.

Kuna hizi hulka za wasichana Noella. Jinsi alivyomuumba mwanamke huyu huwa ninatabasamu. Ni utundu tu aliotumia, ni kama vile namtazama Laura Pettie, Glory Tausi, Gloria Sizya.

TULIA KIDOGO...
Hivi NOELLA na TONY wameshafunga ndoa au ndo tutakutana nao kwenye Patashika nguo kuchanika au Nyaraka za ndoa yao zitapatikana mwakani? Nimeona tujikumbushe kidogo hiii riwaya. Kama hujasoma TAFUTA KITABU HIKI UJIONEE.




..© Markus Mpangala

No comments:

Post a Comment

Maoni yako