December 09, 2017

SIKU YA UHURU DESEMBA 9: PAPII KOCHA NA NGUZA VIKING WAACHILIWA HURU.

NA MWANDISHI WETU, DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amewasamehe wafungwa zaidi ya 8000 na kuagiza wengine takribani 1000 waachiliwe huru leo. Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa sherehe za uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) ambapo kila mwaka rais anatoa msamaha kwa wafungwa kulingana na taratibu zilizowekwa. 
 BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO YA WIMBO WA SEA
Miongoni mwa wafungwa ni wanamuziki mashuhuri, Nguza Viking au maarufu kwa jina la ‘Babu Seya’, na Johnson Nguza maarufu kwa jina la ‘Papii Kocha’ wameachiliwa huru kwa msamaha wa rais. Wanamuziki hao walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela kutokana na kuhukumiwa kwa makosa ya kuwadhalilisha kijinsia watoto. Msamaha huo ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanzania Bara iliyopata uhuru wake mnamo Desemba 9 mwaka 1961.
Akizungumzia kuhusiana na kuwasamehe wafungwa, Rais John Magufuli katika hotuba yake aliyotoa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma, alisema, "Nimesamehe wafungwa 8157 na kati ya hao wafungwa 1828 watatoka leo. Nimeamua kusamehe familia ya Nguva Viking (Babu Seya) na Johnson Nguza na waachiwe HURU kuanzia leo,” 

"Nimesamehe wafungwa 8157 na kati ya hao wafungwa 1828 watatoka leo. Nimeamua kusamehe familia ya Nguva Viking (Babu Seya) na Johnson Nguza na waachiwe HURU kuanzia leo,” alisema Rais John Magufuli katika hotuba yake aliyotoa akiwa uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Katika hatua nyingine, Raisi Magufuli amewaachia huru wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa wafungwa walio hukumiwa kunyongwa kupewa msamaha.

''Nimeamua kusamehe wafungwa waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa, na leo au kesho wafanye process za kuwatoa, yuko mtu aliyefungwa akiwa na miaka 18, na sasa hivi ana miaka sitini na kitu'. Nimesamehe wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa na mchakato wa kuwatoa ufanyike leo au kesho. Yuko mtu aliyefungwa akiwa na miaka 18, na sasa hivi ana miaka sitini na kitu. Yumo mtu anaitwa Mganga Matonya, ana miaka 85 na ameishakaa gerezani miaka 44,” alisema Rais Magufuli.

Raisi Magufuli ametoa msamaha huo katika sherehe za miaka 56 ya uhuru wa Taifa hilo zilizofanyika mjini Dodoma ikiwa ni kwa mara ya kwanza zimefanyika nje ya jiji la Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako