Na Kizito Mpangala
Eratosthenes alizaliwa mwaka 276 KK
(Kabla ya kuazaliwa Yesu Kristo) mjini Kirene, Libya ya sasa. Kirene ni mji
mashuhuri ulioundwa na Wagiriki wa kale walioishi Afrika ya Kaskazini hasa
Libya ambako ndiko ulikokuwa mji wa Kirene maeneo ya Tripolitania ( sasa ni
Tripoli), na Misri maeneo ya Alexandria ilikokuwa maktaba mashuhuri iliyotumiwa
na wataalamu wengi wa Ugiriki ya kale.
Alikuwa akifanya mazoezi mbalimbali ya viungo kila siku asubuhi na jioni. Alijifunza kusoma, kuandika, na kuhesabu. Ni kama vile falsafa ya elimu ya msingi inayotumiwa nchini Tanzania yaani KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu). Pia, alijifunza uandishi wa mashairi na vilevile masuala ya muziki.
Alikuwa akifanya mazoezi mbalimbali ya viungo kila siku asubuhi na jioni. Alijifunza kusoma, kuandika, na kuhesabu. Ni kama vile falsafa ya elimu ya msingi inayotumiwa nchini Tanzania yaani KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu). Pia, alijifunza uandishi wa mashairi na vilevile masuala ya muziki.
Baadae
alienda mjini Athens nchini Ugiriki kwa ajili ya kisomo. Alifundishwa falsafa
ya maadili kulingana na matakwa ya jamii ya Wahelleni ambayo ni mchanganyiko wa
tamaduni za Wagiriki na Warumi, kwa ujumla huitwa Utamaduni wa kihelleni
(Hellenistic Culture). Falsafa hiyo ya maadili (Hellenistic Philosophy) iliitwa
Stoicism kama ilivyoasisiwa na
mwanafalsafa Zeno wa Ugiriki.
Ni falsafa
ambayo iko tofauti na zile za Wagriki wengine kama akina Socrates, Plato, Aristotle
na kadhalika, ambayo iliegemea zaidi katika upande wa kile kilichosemwa na
mwanafalsafa husika. Lakini falsafa ya maadili kadiri ya matakwa ya Wahelleni
ilijali kile alichokitenda mtu na siyo alichokisema.
Eratosthenes alikuwa mtaalamu
wa hisabati, lugha, historia, jiografia, mshairi, mnajimu na mtaalamu wa muziki. Daima
alikuwa mtu wa kujifunza. Alikuwa mkurugenzi mkuu wa maktaba mashuhuri ya
Alexandria nchini Misri. Maktaba hiyo vitabu vyake vyote vilikuwa vikiandikwa
kwa mkono, hiyo ilitokana na kutokuwepo kwa teknolojia bora ya kuchapisha
vitabu kama ilivyo sasa.
Alijifunza pia falsafa za
mwanafalsafa mashuhuri Plato na kuzipenda falsafa za Plato. Mwalimu wake mkuu
wa falsafa alikuwa ni Zeno na mwalimu wake mwingine wa falsafa pia alikuwa ni
Aristo wa Chios. Baada ya kuzipenda falsafa za Plato na kuzifuatilia kwa kina,
Eratosthenes aliandika kazi yake ya kwanza akiwa mwanafunzi. Kazi hiyo aliiita Platonikos, ambapo aliandika misingi ya
hisabati kulingana na falsafa za kihisabati za Plato.
Eratosthenes alipenda
kujishughulisha na mambo mbalimbali kitaaluma na hivyo kumfanya awe na kichwa
chepesi katika kufikiri zaidi. Alichunguza na kufuatilia sanaa ya ushairi akiwa
na mwalimu wake wa ushairi, Kallimakhosi ambaye alikuwa mwananchi wa Libya ya
kale akiwa na asili ya Ugiriki.
Eratosthenes aliandika mashairi
mbalimbali hasa kuhusu historia ya miungu ya kale ya Ugiriki ambapo shairi liliitwa
Hermes. Shairi lilingine lilihusu
binti wa Athen aliyejinyonga, lilitwa Erigone. Pia, aiandika kazi yake ya pili iliyofikiriwa
kuwa ni ya kisayansi ambayo ilihusu umuhimu na mwanzo wa vita vya Trojan. Vita vya Trojan ni vita vilivyotokana na tamaduni za Wagiriki (Greek
Mythology). Pia aliandika kazi ya tatu mbayo haikujulikana muda alioandika
lakini alisifiwa sana kutokana na kiwango chake cha uandishi. Kazi hiyo aliiita
Olympic Victors.
Uwezo wa kuandika ulimfanya
atambulike zaidi na hivyo Pharao Ptolemy III Euergetes aliamua kumuomba awe mkurugenzi
mkuu wa maktaba ya Alexandria waka 254. Maktaba
ya Alexandria ni moja kati ya maktaba za kale zinazoheshimika sana duniani. Kwa
sasa maktaba hiyo ni maktaba kuu ya taifa nchini Misri, ni maktaba iliyoanzishwa
mnamo karne ya tatu kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo. Eratosthenes alikubali
wadhifa huo wa kuwa mkurugenzi mkuu wa maktabani hapo.
Baada ya kupewa wadhifa huo
ambao alimpokea mkurugenzi wa awali na mshairi, Apollonius Rhodius,
Eratosthenes aliwekwa kuwa mwalimu wa watoto wa Pharoa Ptolemy ambapo mmoja
kati yao akamrithi baba yake uongozi na kuwa Pharao wa IV yaani Pharao IV Philopator.
Akiwa kiongozi wa maktaba hiyo,
Eratosthenes alitangaza kuwa vitabu vyote vinapaswa kuwekewa alama maalumu ili
kutambua kitabu halisi na kilichotolewa nakala tu. Ndipo utaratibu wa namba za
kimataifa za vitabu ulipoanzishwa. Namba hizo kwa sasa hujulikana kama ISBN
ambapo ni kifupi cha “International
Serial Book Number”. Aliamua kufanya hivyo kutokana na kuzagaa kwa vitabu
mitaani ambavyo vilikuwa vimenakiliwa kwa usahihi kama kitabu halisi husika
ambapo ilikuwa ni vigumu kutambua kipi ni halisi na kipi ni nakala ya ujanja.
Eratosthenes alijidhatiti
kutunza heshima ya maktaba ya Alexandria iliyokuwa na wasomaji wengi kuliko
maktaba ya Pergamom ya Uturuki. Maktaba ya Pergamom ni maaktaba kongwe nchini
Uturuki ambapo kwa sasa ni maktaba ya taifa la Uturuki.
Eratosthenes alikusanya vitabu
vyote vya michezo ya kuigiza (tamthiliya/dramma) vilivyoandikwa na waandishi wa
kale kama vile Sophocles, Aesychylus, Euripides na wengineo, akavihifadhi katika
maktaba hiyo ili kutunza kazi za waandishi hao.
Licha ya kuwa na roho hai
katika masuala ya vitabu na falsafa, Eratosthenes alikuwa mwanahisabti mashuhuri
na kuwa na mchango katika uga wa hisabati kwa ujumla. Alijifunza pia sayansi na
kujenga urafiki baina yake na mwanahisabati na mwanasayansi mashuhuri duniani
kote, Archimedes.
Tufe la armillari (Armillary sphere) |
Mnamo mwaka 253
Eratosthenes aliunda tufe maalumu kwa ajili ya kujifunza nadharia mbalimbali
kuhusu mfumo wa jua na sayari zake. Tufe hilo linafahamika kama “Tufe la armillari” (Armillary Sphere). Tufe hili liliongezewa tafakuri zaidi na kupata
mgawanyiko wa muda kwa namna mbili ambazo zinatumika sasa. Namna hizo mbili za
muda ya mtindo wa masaa 12 na ya mtindo wa masaa 24
kulingana na mistari husika ya longitudo na latitudo.
Eratosthenes aliushangaza
ulimwengu katika kitabu chake kilichohusu mwendo-mduara wa magimba yaliyoko
angani. Kitabu hich kiliitwa “On the
Circular Motions of the Celestial Bodies” ambacho aliushangaza ulimwengu wa
kale na wa kisasa ni kukokotoa na kutoa makadirio ya mzingo wa dunia kwa
kutumia kivuli cha mwanzi. Aliweza kufanya hivyo kwa kutumia maarifa ya
hisabati katika mada kuu ya Trigonometria
kwenye mada ndogo ya Pembe mwinuko (Angle
of elevation) ya jua nyakati za mchana kipindi cha kiangazi akiwa katika kisiwa
cha Syene, kwa sasa ni mji wa Aswan nchini Misri. Eratosthenes aliamini kwamba,
katika kila taifa mazuri na mabaya.
Kielelezo kikionyesha jinsi mzingo wa dunia ulivyopimwa na Eratosthenes. |
Alikokotoa mzingo huo wa dunia
akiwa nchini Misri. Alifanya hivyo kwa kutumia mwanzi mrefu na kupima pembe mwinuko ya jua kutokana na
kivuli cha mwanzi huo na kupata 70. Pia, aliweza
kupima ukubwa wa nchi ya Misri, jambo ambalo liligundulika baada ya tafiti
mbalimbali za kazi zake. Mzingo wa dunia aliopima ulikuwa ni kilometa 44,100.
Miaka
200 baadae,
wataalamu wa anga nchini Italia walifanya vipimo vyao na kupata jawabu
lililozidi kidogo lile la Eratosthenes, majawabu hayo yalitofautioana kwa
kilometa 2,000 tu ambapo wengi walisema kuwa
Eratosthenes alimtuma mtu atembee kuanzia nchini Misri azunguke dunia yote na
kuishia tena alipoanzia safari hiyo!
Miaka
117
baada ya kifo cha Eratosthenes, Christopher Columbus alisoma kazi za Eratosthenes
kuhusu ukubwa wa dunia na akaziamini kulingana na ramani zilizochorwa na
Toscanelli. Christopher Columbus aliamini kwamba mzingo wa dunia uliokokotolewa
na Eratosthenes ulikuwa sahihi na akatoa uamuzi kwamba sehemu aliyofika
alipokuwa akisafiri kwa mashua haikuwa Asia kama alivyodhani, aliamini kuwa
ilikuwa ni dunia mpya! Dunia hiyo mpya iliitwa America pamoja na visiwa vya Caribean
na Bermuda.
Mwaka 2012 mnajimu
wa Italia, Anthony Abreu Mora alirudia upya ukokotosi wa Eratosthens na kupata
mzingo wa dunia kilometa 40,074 ambayo ni tofauta ya
kilometa 36.
Haitoshi katika mzingo nwa
dunia tu, Eratosthenes anaheshimiwa mpaka sasa kuwa ni mwasisi wa somo la Giografia. Alisoma vitabu mbalimbali
kuhusu safari za mabaharia mbalimbali katika maktaba ya Alexandria na kujifunza
zaidi kuhusu dunia na maeneo yake. Aliandika kitabu ambacho kiliitwa GEOGRAPHIKA, kitabu hicho kiligawanyika
katika juzuu tatu. Kutoka hapo somo la Giografia
likawa linajitegemea rasmi. Aliamua kutenganisha mafunzo kuhusu muundo wa dunia
pekee na maeneo yake. Alianzisha istilahi ambazo bado zinatumika mpaka sasa
katika Giografia. Ukuu wa somo la Giografia na aliuanzisha yeye ingawa
wataalamu wengine baadae walikuja kuongeza vipengele vingine.
Kitabu chake cha Geographika juzuu ya tatu aliandika kile alichokiita Jiografia ya kisiasa (Political Geography).
Ni Giografia ambayo huzungumza uhusianao kati ya nchi na watu, serikali na
watu, mipaka na watu, pia hueleza ksababu za watu fulani kufahamiana katika
eneo fulani kwa sifa zinazolandana au kutokana na hali ya hewa ya eneo husika
na uhusiano wake na serikali. Pia masuala ya mipaka ya nchi, uhusiano kati ya
serikali na vyombo vya habari na mafunzo ya matokeo ya uchaguzi (Electoral Geography).
Akiwa mkurugenzi mkuu wa
maktaba ya Alexandria, Eratosthenes alibuni aina ya kalenda ambayo ni chimbuko
la mfumo wa sasa wa kalenda. Alikokotoa idadi ya siku katika mwaka mmoja
kutokana na mwendo wa dunia na njia yake. Baada ya kukokotoa alihitimisha
kwamba mwaka mmoja una siku 365 na
kila baada ya miaka minne kutakuwa na siku 366.
Eratosthenes alikuwa rafiki
mkubwa wa Archimedes. Archimedes na Eratosthenes walijishughulisha na uundaji
wa silaha za kivita kwa kutumia maarifa ya hisabati hasa Jiometri. Archimedes alipokuwa anatoa kitabu kipya, alikuwa anaweka
nakala moja kwa ajili ya Eratosthenes.
Aliishi maisha yake mpaka kufa
nchini Misri katika mji wa Alexandria. Hii ni baada ya kuombwa awe mkurugenzi
mkuu wa maktaba ya Alexandria, hivyo alitumikia wadhifa huo hadi alipopatwa na
ugonjwa wa macho hali iliyomsababishia kuwa kipofu mpaka kifo chake.
© Kizito Mpangala (0692
555 874)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako