NA ALBANO MIDELO, LITUHI
HIKI ni kisiwa kidogo cha
Falkland ambacho kipo kwenye maingilio ya Mto Ruhuhu katika Ziwa Nyasa.Kisiwa
hiki kinamilikiwa na wavuvi toka Ludewa mkoani Njombe na Nyasa mkoani Ruvuma.
Asili ya kisiwa hiki kuitwa
Falkland ni mgogoro wa kugombania kisiwa hicho uliotokea mwaka 1982 kati ya
wavuvi wa Ngelenge wilayani Ludewa wakati huo mkoa wa Iringa hivi sasa Mkoa wa
Njombe na wavuvi wa Lituhi wakati huo wilaya ya Mbinga ambapo sasa ni wilaya ya
Nyasa mkoani Ruvuma.
Kwa mujibu wa historia ya
mgogoro toka kwa Vikta Komba aliyekuwa kipindi hicho,wavuvi wa pande zote
walikuwa wanadai kisiwa hicho ni mali yao.Hata hivyo historia inaonesha kuwa
Aprili 2,1982 hadi Juni 14,1982 ulizuka mgogoro wa kugombania visiwa vya
Falkland vilivyopo katika bahari ya Antlantiki kati ya nchi ya Uingereza na
Agentina kila nchi ikidai kuwa kisiwa hicho ni miliki yao.
Wakati mgogoro wa visiwa vya
Falkland nchini Uingereza unaendelea pia katika ziwa Nyasa kwenye maingiliano
ya Mto Ruhuhu, mgogoro wa kugombania kisiwa uliendelea ndipo kisiwa hicho
kilipewa jina la Falkland ambalo linaendelea hadi leo.
Eneo hili linatajwa kuwa na
utajiri wa samaki wakubwa na watamu wakiwemo mbasa,ngumbo,mbufu,masangalafu na
mbelele.Anayejua zaidi historia ya Falkland Nyasa, nafasi ipo wazi kutujuza.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako