Ijumaa iliyopita ndugu Japhet
Nyang’oro Sudi aliwasiliana nami kunijulisha kuwa nimetunukiwa zawadi ya kitabu
chake. Yeye ni mwandishi wa riwaya ya SAA 72. Hima jumamosi nikawasili kwa
bwana George (Muuza vitabu huyu; simu yake; 0713 454152). George huuza vitabu
vyake pembeni ya sanamu la Askari jijini
Dar es salaam (Posta Mpya). ana vitabu vingi, waweza kulonga naye kujipatia
nakala zaidi. Nilianza kusoma kitabu hicho Jumapili asubuhi yapata saa 4 hivi, hadi
saa 2 usiku. Nikatamatisha. Kina kurasa 202.
Masimulizi ya kitabu hiki ni
kuhusiana na mgogoro wa vita vya wenyewe kwa wenyewe unaoendelea nchini Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo Joseph Katanga anaachiliwa huru na Makahama ya
kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa madai ya kubadilika kitabia). Lakini Katanga
hakubadilika chochote. Alitumia kila njia kuendesha maasi kwa wanavijiji, na
kudhoofisha utawala waDRC. Machache tunayoweza kujifunza.
1.Zonu amechorwa kama
mwanamuziki lakini anautumia kujificha kuwa mdunguaji anayewaunga mkono waasi
wanaoongozwa na Joseph Katanga. Kazi yake kuua wanajeshi wa vyeto vya juu.
Muziki wake unateka wengi lakini nyuma ya pazia ni muas sambamba na Joseph
Katanga.
2. Ushirikiano wanaopata waasi
kutoka jeshi la serikali ni chanzo cha kushindikana kutokemezwa kwa vita hivyo
tangu enzi za Patrice Lumumba. Ingawaje ni simulizi pana ukweli juu ya ushirikiano
huu. Jeneral Faustin Munene amekamatwa Januari 10 mwaka huu nchini Gabon kwa
kosa la mwaka 2011 la kutaka kuipindua serikali ya rais Kabila. Naye Kanali John
Tshibangu anye alikamatwa Februai 1 hapa hapa Dar es salaam na kupelekwa DRC.
Wote wawili walikusudia kumpindua Kabila. Ushirikiano wa waasi na jeshi.
3. UBAKAJI. Mara nyingi
wanaoendesha vitendo vya ubakaji ni wale wanaofahamika kwa wabakwaji. Kwamba mwanamke
anaweza kubakwa na mtu ambaye hakutegemea kama atatenda hilo. Tuzichunge njia
zetu.
4. Mwanadamu yupo radhi kumwaga
damu ili atomize kiu yake. (Dr. Jean au KK).
5.Juliana Owima anawakilishi
kundi la wanawake ambao hutajwa kuwa wanaweza kuwa mashushushu wazuri kuliko
wanaume. Ni binti pandikizi, lakini hasara ya kuwa pandikizi wan chi fulani
mahali ni ukosefu wa UHAKIKA wapi utaendesha maisha yako kati ya nchi
uliyopandikizwa na nchi yako. (Hapa nakumbuka mkasa wa Josephine Baker mzaliwa
wa Marekani aliyekwenda kuishi Ufaransa. Akatumia muziki kama kichaka cha
kuficha ushushushu wake). Pandikizwa, ila akili kichwani.
“Hiyo ndiyo tofauti yetu
majasusi na ninyi wapelelezi. Siye hutumia gharama kubwa na miaka mingi kuweza
kuingia kwnye mfumo wa adui, lakini ninyi hufanya kazi kwa lengo moja
maalumu.m(uk199).
7. ukweli ni gharama na kila
ukweli muna gharama zake. Khajat alibakwa, lakini anapotaka kuanza kulipiza
kisasi ndipo ukweli uko bayana kwamba kuna gharama zake kulipiza kisasi.
8. migogoro haimaliziwi kwa
mtutu wa bunduki peke yake.
9. Nia ovu mara nyingi
hushindwa mbele ya wema. Waovu hawaoni kingine zaidi ya uovu wao. Wenye nia
njema huona vyote viwili; uovu na wema.
10;katika maisha kinachoshinda
ni dhamira. Ukiwa na dhamira daima utafanikisha mengi, hutoogopa kikwazo, bali
ukabiliana navyo.
11. MBINU. Katika mbio za
maisha tunahitaji mbinu za kufanikisha mambo. kanuni mojawapo maishani ni hii “Kama
jasusi mambo mawili ni kipaumbele. Kuwa mbali na wapelelezi wa adui ama kuwa
sehemu ya wapelelezi wa adui”(197). Katika maisha ni ama utekeleze ndoto zao au
uziache zipotelee kondeni. Ni uchaguzi wako.
Mwisho bwana Jabir Omar Makame
tafuta demu wa kibongo bhana, usituwakilishe ugenini… Lol
--MARKUS MPANGALA
No comments:
Post a Comment
Maoni yako