February 28, 2018

SERIKALI IMESIKIA KILIO CHA WENGI

NA GABRIEL MWANG’ONDA
HATIMAYE serikali imesikia kilio chetu kuhusu Single Customs Territory (SCT), wakati mfumo huu ukianzishwa na kutumika hapa kwetu Tanzania, binafsi nilipinga sana japo yalikuwa ni maazimio ya jumuiya za uchumi za Afrika Mashariki na SDC countries walikuwa ndio wanaanza kuipigia chapuo.
Mfumo huu unahusisha maafisa wa Forodha kutoka nchi jirani kuja kuweka kambi katika bandari yetu ili mtu akisema anaingiza bidhaa na zinaelekea DRC kisha aende kwenye deski la DRC lililopo hapahapa bandarini kwetu na kulipa kodi zote pale Bandari ya Dar es salaam. Kifupi ni kwamba sisi tulikuwa tunasaidia nchi jirani kudhibiti ukusanyaji kodi.
Mfumo huu ulilenga pamoja na mambo mengine kudhubiti wizi mkubwa wa bidhaa zinazokuwa zinanasinishwa kwamba ziko in transit wakati si kweli kwamba ni transit, mara nyingi huishia mikoa ya karibu na Dar es salaam na kurudi sokoni hapa nchini. 

Nadhani sote tunajua vituo vilivyokuwa vinajengwa mithili ya uyoga kila uchwao barabara ya Morogoro. Mizigo ilikuwa inaandikwa transit ikifika Mlandizi unaweza kushushwa then unarudi Dar es salaam na biashara inaendelea.

Madhara yake ni kwamba wafanyabiashara wasiowaaminifu wamekuwa wakikwepa kodi kubwa sana kwa jina la Transit wakati bidhaa hizo huishia hapahapa nchini, na kuuzwa kwa bei rahisi, huku wafanyabiashara waaminifu wakiumizwa na ushindani usio sawia.

Hii hali ililetelea wafanyabiashara wengi wafikiri kuwa wakwepa kodi. Kwanini basi binafsi niliamua kupinga huu mfumo, sababu ni kwamba sisi wa Afrika tunajuana vizuri sana, takribani nchi zote zinazotuzunguka ni kama Banana Republic (samahani kwa lugha hii) lakini nataka kumaanisha kwamba ni nchi zilizo na mifumo dhaifu sana katika nyanja nyingi ikiwemo hii ya ukusanyaji kodi.

Sasa kwa wale wenzangu waliowahi kufika DRC watakuwa wanajua kuwa hiyo ni moja kati ya nchi ambazo kodi zingine zinakusanywa na mtu yeyote mbabe tu so mifumo ni dhaifu sana.

Kwakuwa DRC huagiza asilimia kubwa ya bidhaa zao kwakuwa hamna production kubwa ndani ya ile nchi basi automatically DRC ndio mtumiaji mkubwa sana wa Bandari yetu salama kuliko nchi yeyote ile hap East Afrika tena kwa mbali.

Sasa wengi wa hawa waagizaji toka DRC hukwepa kodi za bidhaa huko kwao DRC, sasa ukiwabana walipe kodi bandarini kwetu bila shaka wataenda kwenye bandari zingine ambazo hazina mfumo kama huu, ama hazifuati haya makubaliano.

Waagizaji wa bidhaa toka DRC wengi wakahamia bandari za Msumbiji na Afrika kusini, hili binafsi nililiona kabla ya kuanza kutukia, matokeo yake ikawa ni mizigo ya DRC kushuka bandarini kwetu. Kwakuwa sio nchi zote ziko makini kama sisi kwenye kukusanya kodi wengine hawako strictly kama sisi basi zimekuwa wanufaika wakubwa wa mfumo huu ambao sisi tuliutekeleza kwa moyo wote.

Kwahiyo kuondolewa kwa utaratibu huu wa kutoza kodi popote ni bora tuuache ili kila nchi ipambane na hali yake. Kenya, Msumbiji, South Africa hawajali kabisa hii system na wala hawaitekelezi kiivyo coz wanajua kuwa utawafukuza wateja wao.

Uchumi haufai kuwa suffocated moja kwa moja kwahiyo ni lazima kuwe na sehemu ya kupumulia hewa, ndio maana nchi kama Uingereza wanaojitamba kwa utakatifu wanamiliki visiwa kama Isles of Man ambavyo ni tax haven, hakuna kodi huko wala kutoa taarifa za wamiliki wa makampuni yaliyoko huko.

Marekani nao wanavisiwa vyao vya kufanya uchumi upumue. Netherlands ndio wanaongoza kwa kuacha uchumi upumue. Kwa bahati nzuri sie tumezungukwa na nchi ambazo zinaweza kutusaidia uchumi wetu ukapata hewa na kupumua vizuri na DRC is the best example, so acha sisi hapa ndani tubanane lakini tuwaache hawa DRC kama kipumulio chetu.

Cha msingi ni sisi kuimarisha mifumo yetu ili mtu akisema yuko transit basi tuweze kujua boda atakayotokea tum track na tuhakikishe katoa/kapitisha mzigo wake la hasha asakwe, ukiwekeza vizuri kwenye tekinolojia hili ni jambo rahisi sana.

Nawasilisha.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako