Markus Mpangala |
Na
Markus Mpangala
“Katika kesi nyingi za rushwa, zimekuwa
zikilalamikiwa sana na wananchi na kwa kuliona hilo mara zote nimekuwa
nikimshauri Jaji Mkuu, Othman Chande kuanzisha Mahakama Maalumu za kesi ya
rushwa kama ilivyo Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki,”.
Hayo ni maneno ya Mkurugenzi wa TAKUKURU,
Dk. Edward Hoseah akizungumza wakati wa Mafunzo ya Walezi na wenyeviti wa klabu
za wapinga rushwa jijini Dar es salaam.
Dk. Hoseah ameibua hoja niliyowahi
kuwasilisha baada ya mahojiano yangu na Hakimu Ambroce Nkwera, siku chache tu
baada ya kuajiriwa kuwa hakimu wilayani ya Mbinga, mkoani Ruvuma.
Mahojiano hayo yalitokana na kuibuka wka
tuhuma za rushwa wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini uliowasilishwa
bungeni kwa mwaka wa fedha wa
2012/2013, na kutawaliwa na tuhuma za rushwa dhidi ya baadhi ya wabunge katika
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.
Katika mjadala huo Wizara ya Nishati na
Madini na Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi, walifichua
mambo mbalimbali ya ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya wabunge kupitia kamati
zao, ambayo baadaye yalishindwa kuthibitishwa kutokana na Kamati ya Ngwilizi
kuwasafisha wabunge waliotuhumiwa.
Hakimu
Ambroce Nkwera ambaye ni
mhitimu wa Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, alieleza kwa
kina juu ya mchakato wa kuanzisha Mahakama maalumu ya rushwa ambayo aliita
Mahakama ya Wahujumu uchumi. Nini alichosema wakati huo na ambacho kinasadifu
tamko la Dk. Hoseah, fuatilia
mahojiano haya;-
SWALI:
Ndugu Ambroce Nkwera, shutuma za
kupokea rushwa dhidi ya baadhi ya wabunge, bila shaka umezisikia. Kuna Kamati
za Bunge zinalalamikiwa kwa vitendo vya rushwa, mfano Kamati ya Bunge ya Nishati
na Madini, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC), Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC). Nini tafsiri yako katika suala
hilo?
JIBU: Nimesoma taarifa
nyingi kuhusiana na shutuma hizo. Kimsingi hizo ni shutuma, kwahiyo kuna
mamlaka zinazohusika na ufuatiliaji wake. Mathalani Spika wa Bunge, Anna
Makinda amewasilisha suala hilo mbele ya Kamati ya Bunge ya Maadili, Haki na
Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo, Hassan Ngwilizi.
Spika ametumia madaraka ya kupeleka suala
hilo kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1). Sasa kumbuka ile ni kanuni ya 53(2) na
58(3)(f) inasema malalamiko juu ya vitendo vya rushwa kwa baadhi ya Kamati za
Bunge na wabunge, lazima Spika atumie kanuni hizo.
Siyo hapo tu, Spika wa Bunge anayo
madaraka ya kuvunja kamati inayotuhumiwa ama kama zipo nyingi zinazotuhumiwa
zitavunjwa. Sikushangaa Spika alipoiagiza Kamati ya Ngwilizi kutengeneza code of ethics ili mbunge yeyote
atakayetuhumiwa, hatua dhidi yake zichukuliwe.
Sasa, tunachoona ni matumizi ya ile
kanuni 113(3) inayompa madaraka Spika kuvunja kamati zinazolalamikiwa kwa
vitendo vya rushwa. Hapo Kamati ya Nishati na Madini ikavunjwa. Kwahiyo
uchunguzi unaofanywa na Kamati ya Ngwilizi, utatupa majibu.
SWALI:Umeeleza kanuni za Bunge zilitumika kuvunja
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. Nini mtazamo wako kwa ujumla katika suala
la vitendo vya rushwa bungeni?
JIBU: Mimi,
nimeshtushwa kama watanzania wazalendo wengine. Napata wasiwasi sana na hii
nchi mwisho wake itakuwaje, na siyo mwisho tu bali hali ya maisha itakuwaje kwa
watanzania.
Hivyo ni hofu ya kila mmoja, ingawa ni
kipindi cha mpito, ninayo hofu eneo la muhimili wa pili wa dola limeingiliwa na
ubadhirifu. Lazima tutafute njia za kukomesha hilo. Na hilo lisiwe interim decision maana athari zinaweza
kushamiri kwa wananchi.
SWALI:
Umedokeza suala la interim decision, unasema iepukwe, nini unachokusudia au
unachomaanisha hapo?
JIBU: Ok! Nazungumzia
uamuzi wa mpito. Hii interim decision
ni mbaya, usifikiri kutafuta suluhisho na
kukomesha ubadhirifu kwa tafsiri ya kushutumiwa baadhi ya wabunge, hata
sekta zote wapo na wanatakiwa kutafsiriwa ni wala rushwa. Suluhisho la muda
mfupi hatuwezi kufanikiwa hata kidogo kwa suala la rushwa.
SWALI:
Unadhani wananchi wanachukulia uzito wowote katika suala la tuhuma za rushwa
dhidi ya baadhi ya wabunge?
JIBU:Huu sio wakati wa
mwaka 1947. Uzito upo siyo lazima wananchi wapayuke, kwamba mtu afike
barabarani aanze kusema nakerwa na rushwa ama inakera wabunge
kutuhumiwakwa vitendo vya rushwa.
Matokeo yake unaweza kuyaona katika
uchaguzi, nadhani patakuwa na mabadiliko bila kujali chama. Natoka kusoma
taarifa zao hapa, nashauri kwa kurudia hii sio interim decision, tuwe au tuanzishe Mahakama za wahujumu uchumi,
mimi nadhani zitakuwa na msaada sana katika haya mambo ya rushwa.
SWALI:
Kwanini Mahakama ya uhujumu uchumi. Muundo wa Mahakama hiyo utakuwaje, sababu
tunazo mahakama zinazofanya kazi vizuri tu?
SWALI: Hebu, kabla hujaendelea, ina maana katika mahakama za kawaida,
hatuwezi kuwafungulia mashtaka hao unaosema wahujumu uchumi?
JIBU: Kama nilivyosema
mwanzo, suala la mgawanyo tu hapa, kama ipo division
ya kazi na biashara, basi nayo ujuhumu uchumi iwe division peke yake. Sasa, mahakama za kawaida siyo vibaya ila
tupanue mitazamo yetu. Mimi naona wahujumu wana uwezekano wa kushinda kesi
mahakama za kawaida.
Kwanza sheria yenyewe haiweki nguvu au
adhabu kali kwa tafsiri zangu za uhujumu uchumi. Mifano ipo, na mimi natafsiri
ni uhujumu uchumi, kuna mifano ya watu ambao wamefungwa jela kwa miaka michache
kutokana na sheria zetu, hasa
kwenye mahakama za kawaida.
SWALI:
Kwahiyo, hapa tatizo ni kushinda kesi na kiwango cha adhabu tu, na pia hizo
sheria haziwezi kuboreshwa na kutumika mahakama za kawaida?
JIBU: Naongelea sheria
inayowahukumu watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na adhabu zake.
Mahakama za kawaida naona wengi wanapata adhabu ndogo. Ingawa ni adhabu lakini
bado tunahitaji kukomesha rushwa, na maana ya kukomesha ni pamoja na kutoa
adhabu kali, hivyo na sheria za
ku-deal na wahujumu zipatiwe mahakama yake. Hata zile sheria za zamani alizotumia
Sokoine (Waziri Mkuu, Edward Sokoine), tutumie na kuongeza kulingana na
mazingira ya sasa na huko mbele, tutengeneze sheria na mahakama za kukomesha
wala rushwa, wanazorotesha nchi.
SWALI:
Unasema sheria za kushughulikia
wahujumu uchumi zipo. Ni sheria gani hizo?
JIBU: Kuna hii Economic and Organized Crime Act, lakini
sijui kama hasa wanatumia, kwani ni sheria ya zamani sana. Pia hii nyingine ya Penal Code inaweza kutumika.
Lakinitukisema economic and organized
crime Act, inabidi ujue sheria hiyo ilikuwa inatumika sana wakati wa Rais
Julius Nyerere, ni hiyo iliyotumiwa pia na WaziriMkuu, Edward Sokoine kuwashika walanguzi na wahujumu
uchumi.Hivyo utaona kuwa tuanzie pale alipoishia mzee Sokoine.
Lakini Penal Code wahujumu wanakuwa wanapelekwa tu katika mahakama za kawaida.
Mimi naona haitoshi kabisa kukomesha suala hili, napendekeza lazima tufanye
jambo dhidi ya wahujumu, nasisitiza lazima tumrejee Sokoine kutengeneza njia
mwafaka kukomesha wala rushwa.
Spika wa Bunge Anna Makinda |
SWALI:
Lakini, unadhani tunao Majaji wa kutosha kuhudumia Mahakama ya uhujumu uchumi
au tuanze mchakato mpya wa mafunzo mapya yao?
JIBU: Siyo kweli
kwamba Majaji hawatoshi, labda tufahamishane, majaji wapo, nahawa wana weledi
tofauti kwenye taaluma hii ya sheria. Kwahiyo, wale majaji wenye weledi wa
mambo ya uchumi watapewa eneo hilo, na jukumu lao litakuwa mahakama ya wahujumu
uchumi.
Ni mpango wa kimkakati na kiutendaji
zaidi, na hapa tusizungumzie vikwazo kwamba hatuna fedha, bali tujikamue kadiri
tuwezavyo. Mfano, serikali yetu imeonyesha pesa zipo za kutosha linapokuja
suala nyeti, angalia kama kwenye Tume ya kukusanya maoni ya wanachi kupata
Katiba Mpya inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, wana nyenzo za uhakika,
dhamira imo serikalini, labda tutapata katiba mpya.
Lakini siamini kama suala la mahakama hii
itatufanya tushindwe sababu ya fedha. Tuweke dhamira tu, yote yanawezekana.
Zipo nchi zinawashughulikia ipasavyo wahujumu uchumi, nazo zilikuwa na dhamira
mbali ya majaji wachache kama tatizo lilikuwepo au la.
Mfano tufanye comparison (tulinganishe) hapa na nchi za China, Thailand,
Marekani, Uingereza au Scotland tuone wanawafanya nini wahujumu uchumi ili nasi
tuwe na mwarobaini wa kukomeshwa rushwa. Angalia, mfano kule Thailand ulimuona
Thaksin Shinewatra, alikuwa waziri mkuu wa nchi ile. Lakini akituhumiwa na
kufunguliwa mashtaka ya vitendo vya rushwa.
Hapa lazima tuelewe hawa PCCB ya bwana
Edward Hosea (Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini)
ndio wanajua suala gani au kesi gani ni ya aina ya uhujumu. Yupo DCI, Manumba,
hivyo wale wengine kule kwa DPP anakuwa tayari amepelekewa kesi inayopaswa
kwenda Mahakama ya uhujumu uchumi, ikiwepo.
Sio hilo tu, hapa tunataka pia watu
werevu, well trained katika PCCB ili
tusiharibu mpango wenyewe. Lazima tuwe na mahakama hizo kila kanda ya nchi
yetu. Uhujumu ni janga baya sana kwa nchi, haya yanayotokea ni kilelezo cha
jamii. Tuchukue hatua, hatuchachelewa.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako