Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ONYESHO kubwa ambalo ni uzinduzi wa Shindano la QS Queens
linalotarajiwa kufanyika Jumamosi ya kesho ya Juni Mosi katika Ukumbi wa Dar
Live, Mbagala, pia limepangwa kuwa sehemu maalum ya kuenzi mchango wa msanii
Albert Mangwea, aliyefariki nchini Afrika Kusini.
Ngwea amepangwa kuletwa kesho Jumamosi kwa ajili ya maziko
yake yaliyopangwa kufanyika mkoani Morogoro, huku onyesho hilo la maombolezo
likihudhuliwa na wakali kibao wa muziki hapa nchini lilioandaliwa kwa muda
mrefu na kilele chake kuwa Jumamosi hii.
MB Dog kutia timu rasmi jukwaani |
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya
Habari Maelezo, leo mchana, Meneja Masoko wa Kampuni ya QS Mhonda J
Entertainment, Freddy Felix, alisema kuwa shindano hilo litafanyika pia katika
mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata warembo 20 watakaoishi katika Jumba moja
kwa ajili ya kupata kimwana huyo wa QS Queens.
Alisema kuwa wasanii wengi wamepangwa kupanda jukwaani kwa
ajili ya kuomboleza msiba huo, akiwamo Ney wa Mitego, Wanaume Halisi,
ikiongozwa na Juma Nature, MB Dog, Diamond, Inspector Haroun, Madee, H-Baba,
Snura, Khadija Kopa, Solid Ground Family na wengineo, wakiwamo wasanii
chipukizi, Amor na Shalviny.
Ney wa Mitego, mzee wa Muziki Gani naye ndani |
“Wasichana wote wanaotaka kushiriki shindano hili ambao ni
kama uzinduzi wake, watajiandikisha katika fomu maalum ukumbini hapo, ambapo
baadaye watatafutwa wengine ambao wote wataishi kwa miezi miwili katika nyumba
moja itakayotembelewa na watu mbalimbali.
“Huku mshindi akijishindia gari la kifahari, pia wanapokuwa
katika jumba hilo kila siku mtu atalipwa kadri tutakavyokubaliana, huku
tukiamini kuwa huu utakuwa ni mwanzo mzuri katika shindano hili,” alisema
Felix.
Kwa mujibu wa Felix, shindano hili kabla ya kupatikana
warembo hao litatembelea mikoa kadhaa ya Tanzania Bara, kama vile Mwanza,
Tanga, Morogoro, Mbeya, Iringa na kwingineko kwa ajili ya kutafuta msichana
mmoja wa kuingia katika kinyang’anyiro hicho.
Madee akiwa Jukwaani |
Aidha QS ilitangaza kuwa mabinti wanaotakiwa kushiriki
katika shindano hilo ni wale wenye vipaji maalum na uwezo wowote wa kupambanua
mambo, huku kigezo cha elimu kikiwekwa pembeni.
Shindano hilo pia litaonyeshwa katika vituo vya Channel Ten,
DTV, Clouds, ambapo huko kote wadau na wapenzi wa mambo ya urembo na burudani
watapata fursa ya kuwapigia kura washiriki kabla ya siku ya kilele chake
kitakachofanyika baadaye mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako