Na
James Zotto, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Labda
mimi pia niwape habari kama hii ya Mh. Msando Alberto: Kule kwetu Nyasa, kijiji
na kata ya Liuli, kulitokea mzee mmoja anaitwa John John Mpembo Nyirenda. Hili
jina linafana na koo za Malawi, Zambia, Msumbiji na Tanzania.
In
short, koo nyingi za mwambao wa ziwa zinamchanganyiko wa nchi hizi na hata
Swaziland, Lesotho na Afrika Kusini pia.Ni sawasawa tu na sehemu zingine zote
za mipakani si Tanzania tu.
Nimeandika
chapter two ya thesis yangu kuhusu Social formation
na peopling ya watu wa ziwa nyasa. Pia someni Seligman, Ehret, etc mtaona watu
wa bara hii wamezungukaje/asili yao.
Huyu Mzaee niliyemtaja
alikuwa Mwanajeshi wa Jeshi Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Watu wa
Tanganyika/Tanzania Bara. Alipostaafu, akarudi kijijini kwetu Liuli.
Kulikuwa na imani mzee
mmoja alikuwa anafuga mamba. Ni kweli ziwa letu lilikuwa na mamba wengi, ila
sijui ni wa Mungu au binadamu.Watu walikuwa wanauliwa sana na mamba.
Huyu mwanajeshi mstaafu
alisaidia kutega mitego, mamba wengi waliuawa. Tukawa tunaogelea kwa raha zetu.
Huyu mzee alikuwa hataki kusikia uchawi, tena hasa kijana kalogwa, maana aliamini
ndo nguzo ya Taifa na Liuli ya Nyasa. Kwa ukali wake, akabatizwa jina la MREMA.
Akifananishwa na
Lyatonga Mrema wa Vunjo wa kipindi kile. Akagombea udiwani huyu mzee. Kampeni
za nini? Alishinda kwa kura zote. Aligombea na binamu yake ambaye
hawaelewani....wote asili yao Malawi.
Ukoo wa Kondowe! Huyu
binanamu, inaaminika, akamchongea Uhamiajji kuwa Mh. Diwani wetu wa Nyasa si
MTANZANIA. Nafikiri anamihela binamu huyu na nafikiri walidhani angegombea hata
Ubunge.
Na angeshinda kweli. Eh...Uhamiaji
wakafanya mambo. Wakamvua Uraia. Tukampoteza Diwani wetu kipenzi. Akaomba
Uraia. Akapewa 'fasta'!
Msando, naomba usome
hii habari, itakufariji na kuelewa nchi hii.
Sasahivi baba huyu
kafa. Ulikuwa msiba wa aina yake. Si watu ni kama wingu hakuna pa kukanyaga, shujaa.
Jiulize! Tulikuwa na mwanajeshi, tena mwenye kacheo, lakini si Mzawa....Hamuoni
ni hatari?
Tulikuwa na Councillor
lakini si mzawa, hamuoni hatari? ila kwa yote, yupi bora, huyu ambaye kaitwa si
raia aliyepigania haki ya vijana, kaleta amani ama hawa wajiitao wazawa wachawi
na waonevu na hawana la maana?
Lakini wote koo zao ni
asili ya Malawi haimaanishi zimeanzia malawi. Alizaliwa Liuli, baba yake pia,
mababu zao ndo walihamia.......La sivyo, chukua robo tatu ya Nyasa na uiondoe
siujui uipeleke wapi sasa na ndivyo hata maeneo mengi ya mpakani na hata kati.
NANI RAIA WA NCHI HII? Naombeni
jibu. Kama ndo hivyo, lile darasa letu la HGL-1998-2000 lililoongoza nchi nzima
kwa matokeo na ambalo limetoa watu wataalamu wanaosaidia nchi hii, basi karibu
lote linatokea mpakani, na hivyo si RAIA? I wanted to share this with you.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako