KITABU:
IT CAN’T BE TRUE
MWANDISHI:
JOHN MWAKYUSA
MCHAMBUZI:
MARKUS MPANGALA
HII
ni mara yangu ya kwanza kusoma riwaya ya mwandishi John R.P. Mwakyusa, mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Riwaya inaitwa “It Can’t Be True: A Story from
Uganda-the Pearl of Africa”, na kuchapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2017 na
kampuni ya Partridge Publishing ya India.
Kitabu
hiki kimepewa nambari za usajili 978-1-54-37-0041-1, ambapo kimegawanywa katika
sura 13 zilizobeba matukio tofauti yanyomsaidia msomaji kupata picha kamili.
Mandhari
ya kitabu hiki ni Tanzania na Uganda. Mwandishi anasimulia mkasa wa Albert Mukasa
ambaye akiwa na miaka 10 na mwanafunzi wa shule ya msingi Kyashemeire iliyopo
Mbarara nchini Uganga anashuhudia wazazi wake wakiteswa na baadaye kuuawa na
askari wa serikali iliyokuwa madarakani.
Huzuni
aliyokuwa nayo Albert haielezeki. Maisha yalikuwa shuruba kwake. Akajiunga na
kikosi cha waasi akiwa kinda. Alipania kulipa kisasi juu ya watu waliohusika na
mauaji ya wazazi.
Mwandishi
anaanza kwa kutusimulia namna Albert Mukasa alivyoshuhudia askari hao baada ya
mauaji wakilaumiana kwanini walimuua mama yake Albert. Mwandishi anasimulia kuwa ghadhabu ya Albert
ilichochea kukatisha shule na kujiunge na kikosi cha waasi cha NRA, na baada ya
kuchukua madaraka, Albert na askari wengine ambao hawakumaliza shule
walipelekwa tena shuleni.
Mwandishi
anaonyesha mabadiliko ya uongozi kati ya awali na ulioingia kwa njia ya mtutu
wa bunduki. Kwamba waasi wa NRM walikuja na mipango mizuri ya uongozi na
kuituliza Uganda.
Katika
sura ya pili Mwandishi anasimulia wasifu na shughuli za Alvani Kasalirwe. Alvin
alikuwa wakili mashuhuri akifanya kazi na taasisi mbalimbali akiwemo mwekezaji
raia wa Denmark, Karina Kirsten. Hata
hivyo likatokea tukio la kushangaza baada ya wakili Alvin kuuawa kwa bomu
lililotegwa garini. Ni nani ameshiriki kutega bomu lililomuua Wakili Alvin?
Hapo ndipo kazi ya Albert inaanza kuchukua nafasi kwakuwa alikuwa ofisa usalama
mwenye jukumu la kupeleleza mkasa huo.
Katika
hekaheka za kupeleleza mkasa kifo cha Alvin anajikuta akiangukia mikononi mwa
wanawake wawili wenye sifa tofauti; Sharon Erepu na Esther Atukunda.
Mwandishi
anaonyesha matukio matatu tofauti yanayowahusisha wanawake hawa. Esther alikuwa
mhudumu wa Baa, wakati Sharon binti mrembo alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu.
Tukio la kwanza ni lile la Albert kukutana na Esther aktika Baa akiwa njiani
kuelekea kwenye maziko ya wakili Alvin Kasalirwe kama sehemu ya upelelezi wa
mauaji yake.
Mazungumzo
ya Esther na Albert yanajenga taswira ya kipekee ambayo msomaji anavutiwa namna
wamandishi alivyopangilia mkasa wenyewe. Baadaye tunadokezwa kuwa Esther
Atukunda alikuwa shushushu anayejihusisha kukusanya taarifa za matukio
mbalimbali mitaani. Hivyo kukutana na ‘mpelelezi’ Albert Mukasa.
Tukio
la pili ni lile la Sharon Erepu kukutana na mpelekezi Albert kupitia kaka yake
Lawrence Okanya ambaye alisoma naye alipokwua chuoni (King’s College, Budo).
Sharon alikuwa mchumba wa wakili Alvin, kwahiyo Lawrence alikuwa shemeji ya
Alvin.
Mwandishi
anatuonyesha ‘lifti’ aliyotoa Albert wka Lawrence na Sharon inampa mwangaza
mpya kumfahamu muuaji wa wakili Alvin. Tukio la tatu linamhusu Sharon Erepu
ambaye alipanga kumtambulisha mchumba wake, Paul Emmanuel Komba, mtoto wa
askari wa zamani wa JWTZ aliyepigana vita vya Uganda na baadaye kutoa maunzo
kwa askari wapya walioachwa madrakani nchini humo.
Inagundulika
kuwa Paul Komba ni binamu wa Sharon. Paul ni mtoto wa sajenti mstaafu Emmanuel
Komba aliyezaa na mwanamke wa Uganda, Ajaro ambaye ni shangazi wa Sharon. Upelelezi
unaendelea hadi kubainika kuwa muuaji wa Alvin ni Lawrence Okanya. Lawrence
alitumiwa na mwekezaji raia wa Denmark,Karina Kirsten. Wasifu wa Karina Kirsten
umechorwa kama mchungaji ambaye alikuja kueneza neno la Mungu na rafiki yake
Mchungaji Sebina.
Nyuma
ya pazia wawili hawa walipanga mauaji ya wakili Alvin kwakuwa alikuwa
mwanaharakati wa mazingira kwa upande mmoja na mwingine kama wakili wao. Alvin
alipinga ajira za watpto migodini.
Dhamira
kuu zinazopatikana katika kitabu hiki; madhara ya utawala mbovu katika
nchi,utumikishaji wa watoto vitani,umasikini,tama ya kupata mali ya Lawrence
hadi kuua, nafasi ya watoto kuchagua wachumba kwasababu Ajaro alikataliwa na
wazazi wa Emmanuel Komba kwakuwa walishamchagualia mchumba, uthubutu, kutokata
tamaa,thamani ya kufanya kazi,maadili, na ulevi kwa kutaja chache.
Mwandishi
amedumisha baadhi ya mila na desturi muhimu kwa wakazi wa Afrika masharika.
Pili, amedumisha matumizi ya misemo ya lugha asili na Kiswahili. Uhondo wa
kitabu hiki ni kukisoma mwenyewe zaidi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako