NA. HONORIUS MPANGALA
0628994409
Rais
Joseph Kabila ni mmoja ya marais wa Afrika ambao ni wamashabiki wakubwa wa
mchezo Wa soka. Amekuwa akisapoti sana mchezo Wa soka Kwa timu yao ya taifa
inayoitwa chui. Wadau wengi wa soka wanakumbukumbu ambayo aliiweka kwa kuwapa
zawadi ya magari kila mchezaji na viongozi wote walioshiriki katika michuano ya
CHAN iliyofanyika mwaka Jana 2016 nchini Rwanda.
Kabila
ameonekana mara nyingi sana katika viwanja vya michezo akihudhuria mechi
mbalimbali.Hata katika video ya ule wimbo maarufu 'Leopards fimbu na fimbu'
ulioimbwa na Felix Wazekwa umemwonyesha rais akikabidhiwa kombe la Chan mwaka
2009 na Nahodha Wa wakati huo Tresor Mputu,ambalo Jamhuri ya kidemokrasia ya
Kongo walilichukua baada ya kuwafunga Ghana katika uwanja wa Felix
Houpout-Boigny pale Abidjan Nchini Ivory Coast.
November
25,2017 katika ardhi ya Afrika kusini klabu ya Tout Puissant Mazembe Englebert
ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo walifanikiwa kunyakua ubingwa Wa Afrika kwa
kutwaa kombe la shrikisho la soka Afrika Caf ambao walikuwa wanauchujua kwa
Mara ya pili mfululizo.Ilikuwa ni wiki mbili tu baada ya kupatikana bingwa wa
ligi ya mabingwa Afrika ambaye ni Wydad Athletic Club Casablanca.
Mazembe
walifanikiwa kupata ushindi katika chezo wa awali uliofanyika nyumbani kwao kwa
magoli mbili kwa moja dhidi ya wageni Super sport United ya Afrika kusini.
Mchezo wa marudiano katika uwanja wa Lucas Moripe jijini Pretoria unamalizika
kwa sare ya bila magoli. Hatimaye Mazembe akatwa ubingwa.
Wakiwa
Afrika kusini Mazembe walipambana kwa dakika zote za mchezo kuhakikisha
wanalinda ushindi walioupata nyumbani na wanarejea na kombe. Walifanikiwa
katika hilo na matarajio yalikuwa kikombe kitumike kuwasahaliulisha Wakongomani
ambao kwa sasa wana machafuko ya kuhitaji kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa rais.
Ni wazi maandamano yanayofanyika maeneo mbalimbali ya Kongo ni kushinikiza
uchaguzi na Vyama Vingi vikiungana ili kumwondoa Kabila maradakani kwa kupitia
boksi la kura.
Wakiwa
nchini Afrika kusini klabu ya Mazembe siku ya November 27 jumatatu walitarajia
kusafiri kwa ndege moja kwa moja hadi Lubumbashi ilipo maskani ya klabu hiyo.
Kioja kilichotokea wachezaji na viongozi walisubirishwa kwa masaa kumi katika
uwanja wa ndege wa Johannesburg wakisubili ndege waliyotakiwa kusafiri nayo.
Huku
nchini Kongo mashabiki wa Mazembe walifurika kuilaki timu yao wakasubiri kwa
masaa mengi bila mafanikio. Ilibidi wasubiri hadi jumanne ya November 28, baada
ya kupata ndege iliyoweza kuwafikisha katika uwanja wa Simon Mwansa Chapwepwe
mji wa Ndola nchini Zambia na baadae msafara kuelekea Lubumbashi kuwa wa njia
ya barabara.Mazembe walitakiwa kuwahi ili siku ya jumatano November 29 wacheze
mechi ya ligi kuu ya Kongo dhidi ya Don Bosco.
Katika
changamoto hizo walizokutana nazo Mazembe Mmliki wa klabu Alimlaumu waziwazi
rais wa Kongo Joseph Kabila kuwa hayo yote yametokana na yeye kuwa sehemu ya
Mazembe.
Kumbuka
Moise Katumbi Chapwe ni mmoja ya wanasiasa wenye nguvu nchini Kongo akitarajiwa
kumpa changamoto kubwa Kabila katika uchaguzi ujao ambao Moise anaungwa mkono
na vya vya upinzani taklibani tisa. Mosie aliandika katika ukurasa wake wa
mtandao wa kijamii wa tweeter"mazembe ni bingwa wa afrika, ubingwa wa mazembe
ni wakongo wote na sio wa Katumbi.
Nyakati
zote nimekuwa nikisema Kabila ni mtu mbaya anayekiuka haki za binadamu"
baadae akawashukuru mamlaka ya usafiri wa anga wa Zambia kwa huduma
waliyowapatia na kusema "hii ndiyo afrika ambayo iko fair na inasapoti.
Pamoja na kutua Ndola klabu hiyo ilitumia nafasi hiyo kuwafanya wachezaji wao
wenye asili ya Zambia kushukuru sapoti waliyowapa kureje na Kuwaonyesha kombe
lao. Ni Raniford Kalaba,Nathan Sinkala na Kabaso Chongo ambao hutokea Zambia
wakihudumu katika klabu ya Mazembe.
Unaweza
kusema Kabila alikuwa hana uelewa na suala la ka klabu kupandishiwa Bendera ya
taifa inalotoka? Hajui kama klabu zinaimbiwa nyimbo za taifa za nchi zinatoka
bila kujali kuwa na wachezaji wasio wa nchi husika?. Au ndo ubabe wa kisiasa wa
kunyimana nafasi ya kuonyesha walicho nacho wapinzani wake kisiasa.
Msafara
wa Mazembe ulishika barabara ya Ndola hadi Mpakani Kasumbalesa kupotia
Kitwe,Chingola na Chililabombwe.
Kikundi
maarufu cha ushangiliaji cha klabu hiyo ambacho husafiri kila mahali kusapoti
klabu yao kinaitwa 100% 'cent pour cent' . kilirejea baada ya mchezo huku
baadhi ya washangiliaji wa kikundi hicho ambao hawakusafiri waliendesha
shamrashamra uwanja wa ndege wa Lubumbashi.
Hata
hivyo iliwalazimu kuelekea Kasumbalesa siku ya jumanne ili kuipokea klabu yao
huku wakiwa na zama zote wanazotumia katika kushangili.Kutokana na Katumbi
kutohudhuria mechi hiyo Afrika Kusini ilimlazimu kulipia tiketi elfu tano na
kitoa magari ishirini ili mashabiki waemde kuishangilia timu yao.
Kwa
Mara ya kwanza niliwaona asilimia mia moja wa Mazembe katika mchezo wa Simba
dhidi yao mwaka 2011 katika uwanja wa taifa. Pia niliwaona tena mwaka 2016 juni
28 katika mchezo wa Mazembe dhidi ya Yanga,nadiliki kusema hakuna kikundi
chenye kujua kushangilia mechi kama 'cent pour cent'. Ni kikundi kinachojua
kushangilia wakati wote wa mchezo huo. Na kina watu maarufu kama ilivyokuwa kwa
yule mshangiliaji maarufu wa Yanga marehemu Ally Yanga. Lakini katika kikundi
kile kuna watu wawili ambao ni mhimili mkubwa wa kundi na wameliongoza kwa
miaka mingi. Ni Nkolomoni almaarufu kama 'Ninja' na Mutamba Kelemuta kaka wa
golikipa wa Mazembe Robert Kidiaba ambao waanzilishi kwa kundi tangu Mwaka
1983. Amewahi kukariri mmoja ya wanakikundi hicho alipokuwa akiongea na
aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo Rex Mumba kuwa wao hawajali kuhusu matokeo
bali wanajua kazi yao moja tu kuishangilia Mazembe.
Wimbo
ambao unajukikana kama ndio wimbo wa klabu uitwao 'Ooh Mazembe Ooh Mazembe'
ulitungwa na Young Kazadi almaarufu kama 'Chirika'.Pia wana wimbo ambao
humsimamisha kila mmoja hata Katumbi bila kujali yuko jukwaa kuu unaitwa
'Okoyoko' maana mirindimo ya sauti na ngoma hakuna ambaye ataweza kumudu kukaa
akaacha kusimama na kuimba pamoja 'Okoyoko' huku wakipiga makofi uwanja mzima
na kuserebuka na 'outro' kama 'Tp yoyoyoooh Tp yoyoyooh'.
Kundi
lina Wachezaji,waimbaji pamoja na wanamuziki. Kwa idadi yao wako wanakikundi
500 wenye umri wa mika kuanzia miaka 20 hadi 50,wanamuziki ndani yake wako 32
na bendi mbili Na uongozi wa kundi uko mbioni kuongeza wanakikundi vijana
wadogo wa umri wa miaka 14 hadi 15 ili kuwapa changamoto wale watu wazima. Kwa
aina yao ushangiliaji imekuwa ya kipekee na klabu kuona mafanikio yao nyuma
yake wako 'cent pour cent'. Uundwaji wake ulikuwa kupeana upinzani na makundi
ya Timu za Kinshasa.
Iliwahi
kutokea katika moja ya mechi za Klabu bingwa ya dunia zilizofanyika Umoja wa
falme za kiarubu, mechi kati ya Mazembe na Intacionale ya Brazil. Mashabiki
taklibani elfu tano wa Brazil waliokuwa washangiliaji wa klabu yao walicheza
Samba jukwaani na kuimba sana. Baadae 'cent pour cent' waliuwasha moto katika
uwanja wa Abu Dhabi kwa Ngoma, filimbi, tarumbeta,kayamba,vinubi na nyimbo.
Hali iliyoufanya uwanja kuwa na ndelemo za hali ya juu toka kwa wakongo. Huku
wakicheza rhumba ,sebene na mitindo mbalimbali ya Ngoma za kongo, Wabrazil
iliwabidi kutulia na kuwa wapole mbele ya 'cent pour cent' .
Aliwahi
kunukuliwa aliyekuwa Kocha Mazembe Msenegal Lamine Ndiaye nilikuwa inamuwia
vigumu kufikisha maelekezo yake kwa wachezaji kwasababu walikuwa hawamsikii
kutokana na sauti zilizoko juu za 'cent pour cent' na hakuweza kuwaambia
wapunguze kuimba kwani ile ndiyo kazi yao inayowafanya waifuate klabu popote
inapocheza.
Kitendo
cha kutotua katika uwanja wa ndege wa Lubumbashi kiliwasikitisha kwa kiasi
kikubwa mashabiki wa Mazembe na Wakongo kwa ujumla. Usafiri wa gari walioutumia
iliwalazimu 'cent pour cent' kufika hadi boda Kasumbalesa na kuwalaki mashujaa
wao.
Njiani
katika Maeneo ya Whisky, Seventie Maile,Shamba la kabila,Lumata,Kashamata hadi
Kisanga sehemu zote Wakongo walipungia mikono msafara wa klabu hiyo. Katika
eneo la Kisanga ndipo anapotokea rais Kabila ndani ya Jimbo la Katanga ambalo
zamani lilikuwa chini ya Gavana Moise Katumbi Chapwe.Shagwe za mashabiki
wakikundi hicho wamekuwa na kawaida ya kuzunguka katika mitaa ya Lubumbashi
kama Machipisha na Kigoma na misafara ya magari na pikipiki wakicheza na kuimba
kwa pamoja.
Unaweza
kujiuliza ni wakongo wangapi ambao wanaisapoti Mazembe na wakawa hawana furaha
na kilichotokea baada ya klabu yao kutotumia usafiri wa ndege kutua Kongo. Wako
ambao sio mashabiki wa mazembe lakini pia hawamuungi mkono Kabila lazima
watalichukulia kwa mihemko ya juu kwasababu linaonekana ni jambo la kisiasa.
Hata wale Mashabiki wa Fc Lupopo, Darling Club Motema Pembe,Don Bosco hata As
Vita wataona kama kilichotokea kwa wapinzani wao sio 'fair' kwa taifa ambalo
linajua nini maana ya soka.
Ifike
mahali viongozi wa nchi watambue soka ni kama dini maana ni utamaduni ambao
watu wameutithi Tangu miaka iliyopita. Wasiwe wanapenda kuitumia tu michezo
kujitangaza katika kupata kura za wapiga kura wao pia watambue kama ni sehemu
ambayo watu huwekeza na kutoa ajira kwa watu.
Hata
hapa Tanzania tuliona mapema kabisa katika maandalizi ya msimu wa ligi kuu
klabu ya Njombe Mji ilipata changamoto kutoka kwa viongozi wa kiserikali katika
Mkoa wa Njombe waliposema rangi ya jezi zao inafanana rangi za bendera ya chama
kikuu cha upinzani nchini. Na walikagaa kuhudhuria sherehe za utambulisho wa
klabu hiyo kwa mashabiki na wadau wa soka Njombe.Hizo ndio fikra mgando mbazo
zinafanya watu kama rais Kabila aone kuwanyima wasaa wa kuserebuka katika
uwanja wa ndege mashabiki wa mazembe ni kumkomoa kiongozi wa upinzani.
Wanasiasa
wamekuwa waharibuji wakubwa utamadumi na ustarabu wa soka letu Mara nyingi
duniani kote. Hata sakata la Wakatalunya ni siasa tu ambayo almanusura
itukimbizie 'el clasico' . soka ni zaidi ya kucheza uwanjani linarudisha imani
ya waliokwazana na kugombana linawaweka pamoja wanasiasa wenye upinzani mkubwa
kisiasa. Lakini ni hatari kama kiongozi mkuu kama kabila kuingia katika
'skendo' ya kuwanyima ndege TP Mazembe na kujikuta wakikaa uwanja wa ndege Kwa
masaa kumi kisa mambo binafsi ya kisiasa. Hapo anajiharibia mwenyewe.
0628994409
No comments:
Post a Comment
Maoni yako