MWAKA 2012 nilianzisha
kipengere cha “KURUDI NYUMBANI” katika blogu hii. Mtu wa kwanza kuhojiwa
alikuwa Ambroce Nkwera. Unaweza kusoma mahojiano hayo kwa KUBONYEZA HAPA.
Labda swali hapa ni kwanini nilianzisha
kipengere cha “KURUDI NYUMBANI”? Kwanza,
Sababu kubwa ni kwamba kuna wafanyakazi waliowahi kuajiriwa na kupangiwa wilaya
ya Mbinga ama maeneo ya Wilaya za mkoa Ruvuma halafu hawaendi kufanya kazi
vituo vya kazi.
Hilo lilikuwa tatizo kubwa
hivyo niliazimia kuona kuna haja wazaliwa wa maeneo hayo wenye sifa kuomba kazi
ili warejee na kuwatumikia watu wa nyumbani kwao.
Pili, dhana hii ilikuwa
kuzungumza na wazaliwa wa wilaya Nyasa wenye utaalamu wa aina mbalimbali kutoka
darasani au elimu dunia. Kwa kipindi cha miaka minne sijawahi kukifanyia kazi
kipengere hiki hivyo ninadhani ni jambo zuri zaidi kuiendelea kuzungumza na
wasomi wa nyumbani Nyasa, mawazo yao na maoni yao juu ya kuboresha maisha ya wilaya hiyo na kadhalika.
KUNA MAPYA …….VUTA SUBIRA……
Mhariri
Markus Mpangala
Markus Mpangala
No comments:
Post a Comment
Maoni yako