Na Kizito Mpangala
Ukimtazama hata kwa picha
utasema ni mzaliwa halali wa Gambia kutokana na mwonekano wake katika filamu
iliyomlazimu kuwa Mgambia.
Alizaliwa mwaka 1957 nchini
Ujerumani Magharibi (sasa Ujerumani) kwa wazazi Levardis Robert Martyn Burton
Sr na Erma Gene. Baba yake alikuwa ni mpiga picha wa jeshi la Marekani katika
kituo cha afya cha Landstuhl cha jeshi la Marekani nchini Ujerumani. Mama yake
alikuwa mwelimishaji wa jamii.
Burton Jr na dada zake wawili
walilelewa na mama yao katika mji wa Sacramento jijini Calofonia nchini
Marekani huku baba yao akibaki Ujerumani kikazi.
Burton Jr alivutiwa na kujiunga
na Seminari na hivyo akakubaliwa kuanza masomo katika Seminari ya Mtakatifu
Pius X katika kitongoji cha Calt jijini Califonia kwa lengo la kuwa padre.
Alipokuwa Seminarini, alipenda
kusoma vitabu vya falsafa na kufanikiwa kuwasoma wanafalsfa kadhaa Seminarini
hapo. Katika falsafa hizo, alivutiwa na kuwasoma kazi za wanafalsafa Lao Tzu,
Nietzsche na Kierkegaard ambazo zilimfanya awahoji walimu wake kama Ukatoliki
ndiyo dhehebu pekee kweli.
Alipofikia umri wa miaka 17
alihitimu katika Seminari hiyo na kuamua kujiunga na chuo kikuu cha Califonia
Kusini kwa masomo ya sanaa. Alitunumiwa shahada ya kwanza ya sanaa huku
akijikita katika uigizaji.
Mwaka 1977 alikuwa kumzo katika
vyombo mbalimbali vya kimataifa baada ya kuwa mhusika mkuu katika filamu ya Roots iliyotokana na hadithi (riwaya)
iliyoandikwa na Alex Haley katika kitabu chake cha Roots: The Saga of an American Family ambacho kinasimulia kuhusu
kijana aliyeitwa Kunta Kinte ambaye iliaminika alizaliwa nchini Gambia na
kutekwa na wakoloni kisha kupelekwa Marekani kama mtumwa. Katika filamu hiyo,
Burton Jr ametambulika kwa jina la KUNTA KINTE.
Burton Jr alitunukiwa tuzo
mbalimbali na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo BBC kutokana na umhairi wake
katika filamu ya ROOTS ambayo ilikuwa ni filamu hyake ya kwanza kuigiza kwa
umahiri ule. Filamu hiyo mpaka sasa ina matoleo kadhaa. Alipoulizwa na watu
kuhusu mtazamo wa jamii yake ya Marekani katika filamu ya Roots alisema kwamba “filamu
hii imeongeza utambuzi na kujiamini miongoni mwa watu. Watu weusi na weupe
wameanza kutambuana wenyewe kwamba wote ni binadamu, lakini si kama matoleo ya
binadamu. Na ukirusha jiwe bwawani lazima utaona mawimbi yakisambaa kama
mduara, hayasimami. Ninafikiri jambo muhimu ni mabadiliko, na daima yakuwa
taratibu. Jambo lolote linalotokea usiku huwa halina msingi yakinifu ya taarifa
zake. Filamu ya Roots ni sehemu ya mabadiliko, na bado inachezwa katika matoleo
mbalimbali”
Burton Jr anatambulika na wengi
pia katika filamu za Star Trek: The Next
Genaration, Fantasy Island, Battle of the Network Star na The
Muppet Movie. Pia alialikwa katika kipindi cha televisheni kilichoitwa Rebop ambacho kilikuwa ni kwa ajili ya
watoto.
Burton Jr (Kunta Kinte) alipata
heshima kubwa kutokana na kazi yake ambayo ilitangazwa mara 200. Ni mlolongo wa
vipande vya filamu kwa ajili yha watoto, mlolongo huo uliitwa Reading Rainbow ambao unaaminika mpaka
sasa kuwa ni mrefu zaidi kwa katika filamu za watoto kuwahi kutokea. Kutokana na
kutangazwa mara 200, Burton Jr (Kunta Kinte0 na rafiki yake Mark Wolfe walipata
haki miliki ya mlolongo huo kwa ajili ya watoto na wakafungua kampuni ya
utangazaji kwa ajili ya vipindi vya watoto tu. Mwaka 2012 mlolongo huo wa
filamu ya Reading Rainbow ulitengenezewa
kiambata maalumu yaani Application (App)
kwenye ubamba (iPad) ambayo inaitwa RRKIDZ.
Mwaka 1986, Burton Jr (Kunta
Kinte) alifuatwa na mwongozaji wa filamu, Gene Roddenberry ili awe muhusika
mmojawapo katika mlolongo wa filamu yake. Uhusika aliompangia ni Luteni Geordi
la Forge katika mlolongo (series) wa filamu ya Star Trek: The Next Generation. Kisha akaawa anacheza uhusika huo
katika matoleo mbalimbali ya filamu hiyo ambayo ilianza kuitwa Stae Trek: The Next Genaration baadae
ikaiwa Star Trek Generation na kuishia na Star Trek: Nemesis mwaka 2002.
Mwaka 2001 alikuwa muhusika
mkuu katika filamu iliyoitwa Ali
iliyokuwa ikimwelezea Martin Ruther King Jr ambapo Barton Jr ( Kunta Kinte)
mwenyewe ndiye aliyecheza kama Martin Luther King Jr. ameshinda tuzo mbalimbali
ambazo kwa jumla ni 49.
Hakuishia katika uigizaji tu. Burton
Jr (Kunta Kinte) alikuwa pia mwongozaji wa filamu na ameongoza filamu nyingi
sana. Kazi yake mojawapo ya uongozaji wa filamu inayokubalika sana ni matoleo
yote ya filamu ya Star Trek: The Next
Genaration.
Mwaka 1992 Burton Jr (Kunta
Kinte) alimuoa Stephania Corzat ambaye ni mtaalamu wa urembo. Wanao watoto wawili
ambapo mmoja pamoja na mkewe huyo na mwingine ni katika mapito yake ya ujana.
0692 555 874.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako