October 04, 2017

KAMERA YETU NORWAY



Furahisha macho kwa vipawa walivyo navyo wenzetu. Hapo ni Norway kwenye bahari ya Atlantic ambapo walijenga barabara kukatiza bahari kuunganisha miji iliyoko visiwani kwenye eneo la bahari. Kwa kuisoma zaidi tafuta Google. Atlantic way in Norway utaiona. Ila nilipata bahati ya kuzuru eneo hili wiki chache zilizopita nikiwa kwenye mkutano huku mwezi uliopita.

PICHA KWA HISANI YA BENJAMIN MBEZI

October 02, 2017

MSUGUANO WA NYERERE NA IDD AMIN


NA WILLIAM KAIJAGE

NI VIGUMU KUREJESHA ZAMA ZA RTC NA RELI KIGOMA.

NA. HONORIUS MPANGALA
WENGI wanapajua kwa jina la utani mwisho wa reli. Ni kigoma mkoa wa kanda ya Magharibi ukiwa na sifa kemkem katika kila nyanja iwe medani ya siasa,sanaa na hata soka. Kabila la Waha ndio wenyeji wa mkoa huo lakini yako makabila mengine. Wako wabembe na wanyema pia. Moja ya nyimbo bora za bongo fleva 'Leka tutigite' wa Kigoma All stars ni kati alama ambayo inatumika kuutambulisha mkoa huo.Hifadhi ya Gombe na Mahale ambayo ina sokwe ni miongoni mwa kivutio , pia meli kongwe duniani iliyoundwa na wajerumani mwaka 1913 katika maandalizi ya Vita ya kwanza ya dunia MV Liemba iko Kigoma na ingali inafanya kazi hadi Leo.
Umati wa wapenda soka mkoa wa Kigoma wakitazama mechi ya fainali ya mashindano ya kugombea ng'ombe katika uwanja wa Lake Tanganyika.

UTALII KATIKA WILAYA YA NYASA

Makala haya yalichapishwa kwneye gazeti la HABARI LEO kuelekea suala la utalii katika wilaya ya Nyasa.

SOMO LA LEO



“Kitendo cha serikali kutowasilisha taarifa za utendaji wa robo mwaka kwenye Kamati ya Bunge ya Bajeti kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria ya Bajeti ya mwaka 2014 ni dharau kubwa kwa mhimili wa Bunge,”

-Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini

DUNIA KUSHUHUDIA TAIFA JIPYA LA KURDISTAN?


NA MWANDISHI WETU

SEPTEMBA 25 mwaka huu jamii ya wakurdi waliopo Kaskazini mwa Iraq katika jimbo la Kurdistan walipiga kura ya maoni kwa lengo la kujitoa  kutoka kwenye dola la Iraq na kuunda taifa lao.Uamuzi wa wakurdi wa Irak unashahibiana na ule wa wananchi wa jimbo al Catalunya (Catalonia) la nchini Hispania ambalo kwa kipindi kirefu wamekuwa wakipigania kujitenga kutoka Uhispania na kuunda taifa lao.
Asilimia 93 ya kura zilionesha kuwa wakurdi wa Iraq wanahitaji kujitawala wenyewe. Tume ya uchaguzi ilisema idadi  ya waliyoshiriki kura ya maoni ilikuwa zaidi ya asilimia 72.Mamilioni wa wakurdi walishiriki kura hiyo licha ya onyo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa na majirani zake. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema imesikitishwa na hatua ya serikali ya jimbo la Kurdistan kuandaa kura hiyo ya maoni.

Taarifa ya wizara ya ulinzi ya Mrekani ilisema, "Mahusiano ya kihistoria kati ya Marekani na watu wa Kurdistan hayatabadilika kufuatia kura hiyo lakini tunaamini hatua hii itasababisha kutokuwepo na uthabiti na kuzidisha maisha magumu katika eneo la Kurdistan na watu wake." 

September 30, 2017

NADHARIA YA FIBONACCI.

NA KIZITO MPANGALA
 
FIBONACCI alikuwa mwanahisabati mdogo nchini Italia. Aliraruliwa uhai wake na watu "wasiojulikana" kutokana umahiri wake katika hisabati. Wakati anararuliwa uhai wake alikuwa na umri wa miaka 21 tu na tayari alikuwa amekwishachapisha ubunifu wake wa namba katika kitabu.

Ingawa kazi zake nyingi hazikutambuliwa zilikohifadhiwa, lakini ubunifu wake maarufu wa kufinya namba umekuwa na umuhimu mkubwa katika uhandisi na usanifu wa majengo. Utafiti ulifanyika kwa kina na kuweza kuona kwamba kijana Fibonacci amechangia kadiri ya uwezo wa ubongo wake katika hisabati. Hisabati inaishi, ili kujua inaishi basi usione aibu kujufunza na kuona wapi inatumika.


Mfumo wa elimu katika nchi nyingi barani Ulaya, Amerika, na Australia umejengwa katika misingi ya udadisi mkubwa. Udadisi huo ni wa kutaka kujua kwamba anachafundishwa mwanafunzi anaweza kukitumia au kuona kinatumika namna gani. Ndio maana ukitazama vitabu vingi vya hisabati vilivyoandikwa maeneo hayo ni kama vile mapambo tu fulani au masimulizi ya picha mbalimbali lakini ndio msingi ulipolala.

Kinachofundishwa katika hisabati kinatolewa na uwezekano wake katika matumizi maishani mwetu. Hisabati ina msaada mkubwa sana. Ukweli ulivyo, hisabati haiwezekani kuelezwa kama hadithi, ni lazima iwe katika maandishi na kisha kutolewa maelezo kwa kina zaidi. Hisabati si sawa na hadithi ya Pwagu na Pwaguzi.

Pichani ni sehemu za majengo ya hoteli moja katika pwani ya Australia. Upande wa kushoto ndivyo inavyoonekana kutoka juu, na upande wa kulia ni sehemu mojawapo ya majengo hayo. Hisabati inaendana na sanaa. Ndio maana tunasema "kusanifu majengo". Ukitazama kwa makini jengo hili upande wako wa kulia lina umbo la gamba la konokono, ndivyo ilivyo.

UTUNZI WA VITABU NA KISWAHILI CHA PROFESA SHAOPING

NA KIZITO MPANGALA

KESI YA ALMASI ni kitabu kilichoandikwa na Profesa Rao Shaoping wa China. Kitaaluma yeye ni mhandisi. Alijifunza Kiswahili nchini Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja na ushee, mwalimu aliyemfundisha aliitwa Ali Omari Mzee.
Profesa Shaoping ndiye msimamizi wa kazi za TAZARA wakati inajengwa. Alikuwa akimtafsiria Mwalimu Nyerere mazungumzo aliyokuwa akijadiliana na wenzake. Pia alikuwa mkaliamani kwa Mh. Salim Ahmed Salim, Mh. Rashid Kawawa, Spika Adam Sapi kwa mazungumzo aliyokuwa akijadiliana na Wachina wenzake. Na mwaka 2013 Profesa Shaoping alikuja tena nchini Tanzania kumtembela Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Profesa Shaoping anasema hivi "ninaipenda Tanzania. Ninawapenda watu wa Tanzania". Profesa Shaoping anayafahamu maeneo mengi nchini Tanzania ambayo amewahi kutembelea, maeneo hayo ni kama vile Kisuwa cha Saa Nane, Arusha, Ifakara, Iringa, Kimbwe, Kidatu, Mikumi, Makambako, Mbarali, Tunduma, Zanzibar, Moshi, Dodoma na kadhalika.

Profesa Shaoping ameandika kitabu hiki kwa bidii mno. Anasema tangu tuwe Koloni la Mjerumani na baadae Mwingereza, wageni hao hawakuwa na morali ya kutunga riwaya za Kiswahili lakini yeye kama mgeni alipenda sana kuacha kitabu kwa Kiswahili, naam, ndicho hiki hapa pichani.

BATAMZINGA SI MWEWE

1    Wako wapi wanaume, majemedari ya nguvu,
Wenye nguvu ya umeme, wasofikwa na uchovu,
Watu wasio kinyume, ubongo uso mbovu,
Batamzinga si mwewe, maneno haya shahada.

Wako wapi wanawake, watalamu wa urembo,
Kwao haki itendeke, wakaziimbe na nyimbo,
Mioyoo iridhike, pasi kushikiwa fimbo,
Batamzinga si mwewe, maneno haya shahada.

Wanaume watukutu, ni vema watakasike,
Mioyo yao ya kutu, inayo mengi makeke,
Miili ya ukurutu, ni vema isafishike,
Batamzinga si mwewe, maneno haya shahada.

MTOTO UMLEAVYO

Mtoto umleavyo, hivyo ndivyo akuavyo,
Akilelewa hovyo, naye atakuwa hovyo,
Ukimdekeza hovyo, na atalemaa ovyo,
Mtoto umleavyo, hivyo ndivyo akuavyo.

Mtoto mlee vema, aje kukusaidia,
Umzoeshe mapema, kufua na kufagia,
Tamsaidia mama, baba atafurahia,
Mtoto umleavyo, hivyo ndivyo akuavyo.

Ukimletea ukali, atakuwa mwoga sana,
Atajiweka mbali, si jambo lenye maana,
Hapo huzuka kitali, sio vema kuchapana,
Mtoto umleavyo, hivyo ndivyo akuavyo.

MADAKITARI WENGI

1   Kijana mimi rijali, ninaishi Afrika,
Nipo hapa kwa asili, siwezi kubadilika,
Jambo hili nakubali, kichwani halitatoka,
Madakitari ni wengi, waniweka njiapanda.

Juzi nilipata shida, tatizo langu kusema,
Nilimueleza dada, akamueleza mama,
Nilingoja kwa muda, na kichwa kikiniuma,
Madakitari ni wengi, waniweka njiapanda.

Dada na mama wakaja, ili kuijua homa,
Mahoma nikayataja, yakamshangaza mama,
Madakitari kataja, basi homa itakoma,
Madakitari ni wengi, waniweka niiapanda.

September 29, 2017

KWA WAANDISHI WA VITABU NA MACHAPISHO MENGINE YA KISWAHILI.

NA MAUNDU MWINGIZI

Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), kwa mujibu wa sheria ndio chombo, kwa niaba ya serikali, kinachosimamia masuala yote yanayohusu lugha ya Kiswahili Tanzania. Kwa miezi kadhaa sasa limekuwa likiandaa kanuni mpya za Kiswahili Tanzania. Rasimu ya kanuni hizo imeshakamilika na baadhi ya wadau walipewa kuisoma na kutoa maoni yako, na baadaye wadau wachache walialikwa kwenye kikao kingine cha kupitia maoni yaliyotumwa na wadau juu ya rasimu hiyo. 

Wajumbe wa kikao wengi waliwakilisha wenzao kutoka sekta ndogondogo zinazogusa lugha ya Kiswahili. Mfano, Watunzi wa vitabu, waandishi wa habari za Kiswahili, Bodi ya filamu Tanzania, Wakalimani/Wafasiri wa kawaida na wale wakalimani wa lugha za alama, walimu wa Kiswahili kwa wageni, watu wa matangazo, wawakilishi kutoka vyuo vikuu, watu wa mashairi n,k. 

MADENI YANATUKABILI


UFUKWE WA BANDARI YA MBAMBA BAY


SHULE YA MSINGI CHIMATE INA HALI MBAYA

Kwa yeyote aliyezaliwa au kusoma kijiji cha Chimate, wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma, au hata kuweka makazi huko, unaombwa kuungana na wananchi kusukuma maendeleo ya Kijiji hicho.

Kwa hatua za awali ni jitihada za kuhakikisha ujenzi wa jengo la vyumba vya madarasa 3, ambapo uongozi wa Kijiji unakusudia kulibomoa jengo hilo na kulijenga upya kutokana na ufa unaohatarisha maisha ya wanafunzi na walimu.

Njooni tuungane na wana Chimate wenzetu waliopo katika kundi la Whatsapp tayari kwa kuendeleza kijiji hicho, waweza kufanya mawasiliano kupitia namba hizi 0762 996 271 au 0768 841 819 au 0753 771 328 au 0713 599 462.
ASANTENI

UTAFITI: UHANDISI NI FANI INAYOLIPA ZAIDI

WANAFUNZI wa elimu ya juu ambao husomea taaluma ya uhandishi au biashara katika wana nafasi kubwa kuwa mabilionea kuliko wanafunzi wanaosomea taaluma nyingine.

Aidha, wanafunzi wale ambao tayari wameingia katika soko la ajira katika kazi ya mauzo au biashara ya hisa ni miongoni mwa wenye fursa kubwa  kuwa katika sehemu watu matajiri duniani.

Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa hivi karibuni na shirika la ajira la Aaron Wallis, ambalo utafiti wake umeangalia watu matajiri duniani zaidi 100 ili kuona kama kuna uwiano au uhusiano wowote kati ya taaluma yao ya kwanza na jinsi walivyokuwa matajiri au kutengeneza utajiri.

Ripoti hiyo ilibaini  kwamba kazi yao ya kwanza, kati ya mabilionea wakubwa wa juu waliajiriwa kwa mara ya kwanza katika mashirika ambalo sio yao. Pia  kuna wajasiriamali ambao walianza kampuni zao wenyewe na wengine wale walioajiriwa katika biashara za kifamilia  katika nafasi masoko na mauzo.
Mabilionea 10 wa mwanzo kati ya 53 ambao waliajiriwa  katika shirika ambalo sio yao wakati mabilionea tisa tu walianza kazi yao kama mfanyabiashara wa hisa au mauzo.

Utafiti huo pia uligundua kuwa matajiri wakubwa duniani 75 kati ya watu 100 akiwemo Bill Gates, Warren Buffet, George Soros na Jeff Bezos wana elimu ya ngazi ya shahada tu.

Kati ya hao 75,  matajiri 22 walisomea shahada katika taaluma ya uhandisi (ikiwa ni pamoja na mwanzilishi wa mtandao wa Amazon, Jeff Bezos na  mwanzilishi wa Google Larry Page, aidha matajiri 16 walisomea masuala ya biashara ambapo 11 wamesoma taaluma ya fedha na uchumi.

Mabilionea 30 kati ya 100 wanautajiri wa kurithi au wanafanya kazi katika biashara ya kifamilia, wakati 17 walianza kampuni zao wenyewe. Mwezi Julai mwaka huu, muda mfupi tajiri Jeff Bezos alichukua nafasi ya Bill Gates kuwa mtu tajiri zaidi duniani baada ya kuongezeka kwa hisa katika mauzo ya mtandao kabla ya ripoti yake ya mapato, lakini hisa zilishuka tena na Gates alirejea katika nafasi ya kwanza.

Bill Gates ambaye ana utajiri wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 87, na amekuwa mtu tajiri  zaidi duniani tangu mwaka 2013. Billionea huyu mwenye moyo wa kusiadia ametoa dola bilioni 31.1 ya utajiri wake katika kusaidia jamii kupitia taasisi mbalimbali, wakati Jeff Bezos ametoa dola milioni 100 kwa mujibu wa jarida la Forbes  la nchini Marekani.

Hata hivyo, ripoti imebaini kuwa matajiri wengi katika 100 wamesomea shahada ya kwanza ya uhandisi kama orodha ilivyoeleza. Matajiri wakubwa 22 duniani wanataaluma ya uhandisi, ambapo matajiri 16 wamesomea masuala ya biashara, katika fedha na uchumi (11) sheria (6) sayansi ya kompyuta (4) historia (3) Falsafa (2), Siasa (2), lugha ya Kiingereza (2), Historia (2), Hisabati (2) na masuala ya madawa (1).

©MTANZANIA


SOMO LA LEO

Kulala kwa muda mrefu kunasababisha  upweke. Utafiti unaonyesha kuwa watu wapweke wanatumia muda mwingi wakiwa kitandani licha ya kujua hatari zinazotokana hali hiyo. Upweke husababisha kudhani kitandani ni sehemu muhimu zaidi hata kama wakiwa hawana uchovu.