September 29, 2017

UTAFITI: UHANDISI NI FANI INAYOLIPA ZAIDI

WANAFUNZI wa elimu ya juu ambao husomea taaluma ya uhandishi au biashara katika wana nafasi kubwa kuwa mabilionea kuliko wanafunzi wanaosomea taaluma nyingine.

Aidha, wanafunzi wale ambao tayari wameingia katika soko la ajira katika kazi ya mauzo au biashara ya hisa ni miongoni mwa wenye fursa kubwa  kuwa katika sehemu watu matajiri duniani.

Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa hivi karibuni na shirika la ajira la Aaron Wallis, ambalo utafiti wake umeangalia watu matajiri duniani zaidi 100 ili kuona kama kuna uwiano au uhusiano wowote kati ya taaluma yao ya kwanza na jinsi walivyokuwa matajiri au kutengeneza utajiri.

Ripoti hiyo ilibaini  kwamba kazi yao ya kwanza, kati ya mabilionea wakubwa wa juu waliajiriwa kwa mara ya kwanza katika mashirika ambalo sio yao. Pia  kuna wajasiriamali ambao walianza kampuni zao wenyewe na wengine wale walioajiriwa katika biashara za kifamilia  katika nafasi masoko na mauzo.
Mabilionea 10 wa mwanzo kati ya 53 ambao waliajiriwa  katika shirika ambalo sio yao wakati mabilionea tisa tu walianza kazi yao kama mfanyabiashara wa hisa au mauzo.

Utafiti huo pia uligundua kuwa matajiri wakubwa duniani 75 kati ya watu 100 akiwemo Bill Gates, Warren Buffet, George Soros na Jeff Bezos wana elimu ya ngazi ya shahada tu.

Kati ya hao 75,  matajiri 22 walisomea shahada katika taaluma ya uhandisi (ikiwa ni pamoja na mwanzilishi wa mtandao wa Amazon, Jeff Bezos na  mwanzilishi wa Google Larry Page, aidha matajiri 16 walisomea masuala ya biashara ambapo 11 wamesoma taaluma ya fedha na uchumi.

Mabilionea 30 kati ya 100 wanautajiri wa kurithi au wanafanya kazi katika biashara ya kifamilia, wakati 17 walianza kampuni zao wenyewe. Mwezi Julai mwaka huu, muda mfupi tajiri Jeff Bezos alichukua nafasi ya Bill Gates kuwa mtu tajiri zaidi duniani baada ya kuongezeka kwa hisa katika mauzo ya mtandao kabla ya ripoti yake ya mapato, lakini hisa zilishuka tena na Gates alirejea katika nafasi ya kwanza.

Bill Gates ambaye ana utajiri wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 87, na amekuwa mtu tajiri  zaidi duniani tangu mwaka 2013. Billionea huyu mwenye moyo wa kusiadia ametoa dola bilioni 31.1 ya utajiri wake katika kusaidia jamii kupitia taasisi mbalimbali, wakati Jeff Bezos ametoa dola milioni 100 kwa mujibu wa jarida la Forbes  la nchini Marekani.

Hata hivyo, ripoti imebaini kuwa matajiri wengi katika 100 wamesomea shahada ya kwanza ya uhandisi kama orodha ilivyoeleza. Matajiri wakubwa 22 duniani wanataaluma ya uhandisi, ambapo matajiri 16 wamesomea masuala ya biashara, katika fedha na uchumi (11) sheria (6) sayansi ya kompyuta (4) historia (3) Falsafa (2), Siasa (2), lugha ya Kiingereza (2), Historia (2), Hisabati (2) na masuala ya madawa (1).

©MTANZANIA


No comments:

Post a Comment

Maoni yako