September 29, 2017

SHULE YA MSINGI CHIMATE INA HALI MBAYA

Kwa yeyote aliyezaliwa au kusoma kijiji cha Chimate, wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma, au hata kuweka makazi huko, unaombwa kuungana na wananchi kusukuma maendeleo ya Kijiji hicho.

Kwa hatua za awali ni jitihada za kuhakikisha ujenzi wa jengo la vyumba vya madarasa 3, ambapo uongozi wa Kijiji unakusudia kulibomoa jengo hilo na kulijenga upya kutokana na ufa unaohatarisha maisha ya wanafunzi na walimu.

Njooni tuungane na wana Chimate wenzetu waliopo katika kundi la Whatsapp tayari kwa kuendeleza kijiji hicho, waweza kufanya mawasiliano kupitia namba hizi 0762 996 271 au 0768 841 819 au 0753 771 328 au 0713 599 462.
ASANTENI

Mojawapo ya madarasa ya shule ya msingi Chimate.
Mlango wa kuingilia katika darasa mojawapo katika shule ya msingi Chimate.


No comments:

Post a Comment

Maoni yako