December 06, 2012

HAPA NA PALE WILAYANI MBINGA

Kilimo cha Kahawa husaidia kuongez akipato na kukuza uchumi wa wakazi wa wilaya ya Mbinga. Pichani mkulima akifurahia mavuno yake. 

Hii ni moja ya sehemu ya kukumbukwa sana. Ni mji wa Mbuji uliopo wilayani Mbinga. Mji wa mbuji unasifika kwa kuwa na na Mwamba huu ambao hutembelewa na watu wengi sana kujionea maajabu. Mwamba huu hutembelewa pia na wanafunzi wa shule mbalimbali katika ziara za kimasomo ili kujifunza mengi zaidi. Mji wa Mbuji hupokea wageni wengi kutokana na mwamba huu ambao haujaandikwa vya kutosha katika vitabu vya historia.

Mandhari ya wilaya ya Mbinga.

Picha zote kwa hisani ya credo Paul, mkazi wa Mbinga.

2 comments:

  1. Shukrani kwa picha na taarifa. Ndio nyumbani huko. Nilizaliwa nikakulia nikichunga mbuzi na ng'ombe na kondoo, na pia nikichuma kahawa.

    Kwa taarifa tu ni kwamba hiyo picha ya jiwe la Mmbuji inaonekana mtandaoni, kama vile Facebook, ila nilipiga mimi, nikatoa maelezo katika blogu yangu, hapa.

    ReplyDelete
  2. tushirikiane kuitangaza mbinga wajamani

    ReplyDelete

Maoni yako