Na Aaron Kinunda, Mbinga
Mambo niliyoochunguza nikiwa MBINGA ambayo kimsingi
yanahatarisha ustawi na maisha ya wanambinga wote kiujumla.
1. Uharibifu wa mazingira uliokithiri ambao unatishia
uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
2. Kuongezeka kwa kasi maambuzi ya UKIMWI. Hali hii ni mbaya
zaidi, kwa haraka haraka unakuja kugundua kuwa takribani karibu katika kila
mtaa kuna familia kadhaa ambazo zinawaathirika wanaotumia ARV.
maeneo ya wilaya Mbinga
Mbaya zaidi
wengi ni vijana wenye watoto wadogo na ndio nguvu kazi ya jamii. Hali hii ni
mbaya sana kwani kuna hatari baada ya miaka kadhaa tukawa na yatima wengi sana
na wazee wakabakiwa na majukumu mazito ya kulea watoto hao. Kinachosikitisha
zaidi ni ile hali ya watu kutochukua tahadhari wala kujali na pale wanafunzi wa
shule zetu za kata kujikuta wakiingia kwenye huu mtandao mkubwa wa UKIMWI.
3. Ongezeko la vijana wasiojishughulisha na kazi yoyote na
badala yake kubaki kucheza Kamali na kuiba mazao na mifugo ya wazee wao.
Stendi kuu ya Usafiri, Mbinga
HALI INATISHA KWELI, JARIBU KUCHUNGUZA MAENEO UNAYOTOKEA NA
UONE HALI HALISI NA NINI SULUHISHO? HATUA ZA MAKUSUDI INABIDI ZICHUKULIWE
VINGNEVYO....
No comments:
Post a Comment
Maoni yako