ANESA COMPANY LIMITED
P.O.BOX 1295, IRINGA. Mobile +255 719 127 901
Email: anesagroup@yahoo.com, website: www.anesagroup.com
TANGAZO LA KAZI
Anesa Co.,Ltd ni kampuni ya kitanzania iliyosajiliwa na BRELA na kisha kupewa leseni ya kuendesha biashara mbalimbali kwenye maeneo ya Kilimo, Ufugaji, Majengo na Nyinginezo. Kampuni ina masikani yake mkoani Iringa huku ikiendesha shughuli zake katika mikoa ya Iringa, Morogoro na Dodoma. Kwa mwaka 2013 kampuni imepanga kujitanua; hivyo inahitaji wafanyakazi wapya, vijana wenye ari, wabunifu, waaminifu na wenye weledi wa hali ya juu; ili kufanikisha mikakati ya kuitoa kampuni kutoka ngazi moja kwenda nyingine. Kampuni inayofuraha kutangaza nafasi za kazi katika maeneo yafuatayo:
Anesa Co.,Ltd ni kampuni ya kitanzania iliyosajiliwa na BRELA na kisha kupewa leseni ya kuendesha biashara mbalimbali kwenye maeneo ya Kilimo, Ufugaji, Majengo na Nyinginezo. Kampuni ina masikani yake mkoani Iringa huku ikiendesha shughuli zake katika mikoa ya Iringa, Morogoro na Dodoma. Kwa mwaka 2013 kampuni imepanga kujitanua; hivyo inahitaji wafanyakazi wapya, vijana wenye ari, wabunifu, waaminifu na wenye weledi wa hali ya juu; ili kufanikisha mikakati ya kuitoa kampuni kutoka ngazi moja kwenda nyingine. Kampuni inayofuraha kutangaza nafasi za kazi katika maeneo yafuatayo:
A)MENEJA
MAUZO/MASOKO.
SIFA ZA MWOMBAJI
1.
Awe
na elimu ya cheti, diploma au digrii katika masomo ya biashara. Wale
waliodurufu (specialize)kozi za masoko, ugavi au utawala watapewa kipaumbele.
2.
Awe
na umri wa miaka kuanzia 25-35
3.
Awe
ni mbunifu, mpana katika uelewa wa masuala ya biashara, awe ni mchapa kazi na
anayeweza kujisimamia. Mwombaji ajiridhishe kuwa ni mwaminifu na anayeweza
kutumia vichache na kuzalisha vingi.
4.
Awe
na ufahamu wa kutosha kuhusu taratibu za uendeshaji wa makampuni.
B) MUHASIBU
SIFA ZA MWOMBAJI
1
Awe
na elimu ya cheti, diploma au digrii katika masomo ya uhasibu.
2
Awe
na umri wa miaka 21-35
3
Awe
na ufahamu wa kutosha kuhusu taratibu, kanuni na sheria za makampuni
4
Awe
na uzoefu ama uelewa wa kinadharia wa kukokotoa mizania ya mirejesho ya kodi za
makampuni kwa mujibu wa kanuni na taratibu za TRA.
5
Awe
ni mbunifu, mwaminifu, anayejituma na anayeweza kujisimamia mwenyewe.
C) KATIBU MAHSUSI
(OFFICE SECRETARY)
SIFA ZA MWOMBAJI:
1.
Awe ni wa jinsia ya kike
2.
Awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne na awe na cheti
cha mafunzo ya kompyuta au ya ukatibu mahsusi (secretarial certficate)
3.
Awe na umri wa miaka 22-29
4.
Awe na uzoefu usiopungua miezi sita katika shughuli
zinazofanana ama kukaribiana na nafasi hii.
5.
Awe ni mchangamfu, mkarimu, mwaminifu na anayejituma
D) DEREVA
SIFA ZA MWOMBAJI
1.
Awe na umri miaka 25-40
2.
Awe
na leseni class E na kuendelea
3.
Awe
na uzoefu wa kuendesha magari ya mizigo kwa miaka isiyopungua mitatu
4.
Awe
mwaminifu na anayeweza kujisimamaia
MISHARA NA MARUPURUPU.
Kampuni ina sera
nzuri ambazo zinampa nafsi mfanyakazi kufurahia mazingira ya kazi huku akilipwa
mshahara bora na stahiki zinazopendeza.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI.
1.
Waombaji
wote watume barua za maombi zikiwa zimeambatanishwa na maelezo yao (CV), vivuli
vya vyeti pamoja na picha ndogo moja (passport size). Maombi hayo yatumwe kwa
“Meneja Utawala” kupitia baruapepe: anesagroup@yahoo.com
2.
Mwisho
wa kutuma maombi ni tarehe 10/Machi/2013, saa 12 jioni.
3.
Wale
watakaopita katika mchujo wa awali ndio watakaoitwa kwenye usaili.
4.
Usaili
utafanyika Isimila Hotel, Iringa mjini katika tarehe ambayo itajulishwa kwa
wale watakaoitwa kwenye usaili.
IMETOLEWA NA:
MENEJA UTAWALA
ANESA CO.,LTD,
25/FEBRUARI/2013
Howdy this is kinda of off topic but I was wanting to know if blogs use WYSIWYG editors or
ReplyDeleteif you have to manually code with HTML. I'm starting a blog soon but have no coding skills so I wanted to get advice from someone with experience. Any help would be enormously appreciated!
Here is my site - intend
Ahsante kwa taarifa hii!
ReplyDeleteNasisi wavulana tulioishia kidato cha nne wenye miaka 19 mnatusaidia vp katika kampuni yenu
ReplyDelete