MTAZAMO WANGU KWA UFUPI;
Odinga amefanya makosa kisiasa. Timu ya Odinga mwaka huu
ilikuwa dhaifu kupindukia. Haikuwa na ushawishi wowote wenye maana. Kalonzo
Musyoka anastahili kuheshimiwa lakini naye tumwambie hana ushawishi wowote
ambao ungemsaidia Odinga.
Hebu angalia timu ya zamani; Najib Balala, Charity
Ngilu, Mudavadi, William Ruto, na wengine wengi. Odinga amejitakia kushindwa
kwanza kabla ya kuangalia kwamba amekuwa kibaraka wa ubeberu. Angalia njia zake,
angalia timu yake; AMEJITAKIA KUSHINDWA kabla ya kuwa kibaraka. Kama mtu anakumbuka timu ya NARC ilivyokuwa mwaka 2002, kisha ile ODM ya mwaka 2007, kisha kilichotokea katikati na kusambaratika kabisa kwa timu yenyewe kisiasa, basi hakuna shaka kabisa Odinga alijitakia kushindwa uchaguzi kabla ya kulalamika.
Loading .........
KWA BARRACK OBAMA, MAREKANI
KWA BARRACK OBAMA, MAREKANI
kwamba Obama mwanzoni
alimzodoa Uhuru Kenyatta, lakini baadaye nadhani alisoma upepo wa kisiasa na
nguvu ya Wiiliam Ruto ilivyokaa vema na Uhuru. kwanza Obama sio raia wa Kenya
hata kama mzazi wake anatokea Kenya. Obama akumbuke swali alilowahi kuulizwa na
marehemu Hugo Chavez, "Mwanangu Obama unataka kupata kura za uchaguzi
nchini kwako kwa kuwashambulia raia wangu wa Venezuela?" Lilikuwa swali
zuri sana. Sasa Obama anatakiwa kutambua yeye sio Mkenya, na wakenya wameamua
kile kinachofaa kwao bila kujali mashtaka ya Uhuru kule ICC. Na Obama hana
sababu za kushinikiza suala la ICC, kwanza aifanye Marekani kuwa mwanachama wa
ICC halafu tumkamate Geprge W. Bush. Kama akishindwa kuiingiza nchi yake kuwa
mwanachama wa ICC, basi hana mamlaka pia ya kuwachagulia wakenya rais wao.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako