Richard Mwanja |
Na Richard Mwanja, Dar es Salaam
Tangu kutanagazwa matokeo ya kidato cha nne shule mbalimbali
zimekuwa na matokeo mabaya sana. Miongoni mwa
shule hizo ni Lundo sekondari ambayo ilikuwa ikisifika kwa ubora wa wahitimu na
matokeo mazuri.
Lundo sekondari iliwahi kuweka rekodi ya kufaulu wanafunzi
wa kidato cha pili, hivyo hakuna aliyefeli kwa mwaka 1999. Sifa nyingi za shule hii ilikuwa nidhamu na wanafunzi kupenda masomo huku wakikabiliana na hali ya maisha na kuyazoea.
Wengi waliohitimu hapo wamefanikiwa kuwa watumishi imara na kuzalisha wanamapinduzi wazuri kifikra ambao wanaendelea kusukumu gurudumu la maendeleo ya wilaya ya Nyasa, na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla pamoja taifaletu la Tanzania.
Lakini kwa sasa hali
ni tofauti. Licha ya kusifika wakati wa uongozi wa mkuu wa shule Bwan
Ndunguru, sasa hali imekuwa mbaya sana. Maskini Lundo Sekondari.......masikini
wilaya yetu Nyasa....
Inasikitisha kuona shule ile tuliyosoma, shule ile iliyokuwa
kinara kwa ufaulu wa kidato cha nne tangu miaka ile ya 90's hadi mwanzoni mwa
2003.... Leo hii shule ni ya division 4 na 0 tuu.... Kwa mtazamo
Wangu kutokana na vile nilivyokuwa nikifuatilia matokeo ya shule hii kwa miaka
kadhaa,nimegundua shule imekosa Uongozi....
Samahani kwani huenda nitakuwa nimewagusa wengine moja kwa
moja,lakini kwa nini wakati ule wa mzee Ndunguru mambo hayakuwa hivi.... Imeniuma kwa ujumla wa matokeo Kitaifa,lakini nimeumizwa
zaidi na matokeo ya shule zetu wilayani Nyasa.... Sitaki kuamini kama Sisi ni
Vilaza; Hapana!!
Imenigusa sana ..ukizingatia ilikuwa shule yangu ya kwanza ,,,ya msingi yaani...
ReplyDeleteNi kweli kwa sasa matokeo ni mabaya sana, nadhani ni uongozi mbovu wa shule umechangia matokeo mabaya kama hayo
ReplyDeleteMtazamo wangu sio uongozi vijana hawajishughulishi na masomo wapo busy na smart phone ,unakuta muda mwingi wanatumia kuchart,kwani uongozi ndio unaosoma au kufanya mitihani?watoto wazingatie kusoma mambo yatakuwa poa Sana.
ReplyDelete