Na Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mechi ya
hisani itakayowakutanisha waheshimiwa wabunge na Wakuu wa wilaya, itakayopigwa
Juni 29, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya
Juni 22 mjini Dodoma, ambapo huko mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, ambapo lengo la mechi hizo ni kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya
albino, huku kukipangwa kuwa na burudani za kila aina, sambamba na wasanii
watakaoamua kuungana na serikali juu ya uchangiaji huo.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Msemaji Mkuu wa timu hiyo ya wakuu wa wilaya, ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kuwa huku mheshimiwa rais akiwa
mgeni rasmi, ila wamejipanga imara kwa ajili ya kuwaonyesha kazi wabunge, ambao
baadhi yao wameanza kujigamba dhidi ya mechi hiyo ya aina yake.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu |
Alisema kuwa Watanzania wote
watakaopata fursa ya kuhudhuria kwenye mechi hizo wataaburudika kwa kiasi
kikubwa, huku wakiamini kuwa licha ya wakuu wa wilaya wengi kuwa mikoani, ila
wana nguvu na ari ya kushinda mbele ya wabunge.
“Tupo imara na tutaanza mazoezi yetu
kesho Jumatatu kwa kukutanisha wakuu wa wilaya wote waliokuwa kwenye timu hii,
huku barua za kuwaombea mialiko kutoka kwa Wakuu wa Mikoa tayari zimeshafika
kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.
“Katika mechi hizi, mwamuzi wa kati
atakuwa atakuwa Reginald Mengi, ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, huku
waamuzi wa pembeni wakiwa ni IGP Said Mwema na Stephen Wassira, ambapo wote
watashiriki katika mchezo huu,” alisema.
Aliwataja Wakuu wa wilaya waliotwa
kwenye uundwaji wa kikosi hicho kuwa ni pamoja na Venas Mwamoto (Kibondo),
Ramadhan Maneno (Kigoma), Norman Sigara (Mbeya), Krispin Meela (Rungwe), Benson
Mpesya (Kahama), Deodatus Kinanilo (Chunya), Herman Kapufyi (Same), Francis
Isaac ( Chemba), Wilson Mkambaku (Kishapu), Yahya Nawanda (Iramba), Elibariki
Kingu (Igunga), Festo Kiswaga (Nanyumbu), Paza Mwamlima (Mpanda), Abdallah
Ulega (Kilwa), Seleman Mzee (Kwimba), John Mongela (Arusha), Konstantin Kanyasu
(Ngara), Paulo Mzindakaya (Busega), Mrisho Gambo (Korogwe), uhingo rweyemamu
handeni, Cristofa Magala( Newala), Erasto Sima (Bariadi), Jordan Rugimbana
(Kinondoni), Joseph Mkirikiti (Songea), Ngemela Rubinga (Mpanda) nay eye
mwenyewe anayotokea wwilaya ya Handeni, ambaye pia ni msemaji wa timu hiyo.
Aidha, Muhingo alitaja kikosi cha
wanawake kuwa kinaongozwa na Beth Mkwasa (Bahi), Sarah Dumba (Njombe),
Josephine Mapiro (Makete), Hafsa Mtasiwa (Pangani), Mboni Mgaza (Mkinga),
Halima Dendegu (Tanga), Queen Mlozi (Singida), Angelina Mabula (Butiama), Merry
Tesha (Ukerewe), Christina Mndeme (Hanang), Anna Magoha (Urambo) Jacqueline
Liana ( Magu).
mwisho
No comments:
Post a Comment
Maoni yako