PRETORIA, AFRIKA KUSINI
MAJASUSI wa Afrikia Kusini wanataka kufutiliwa mbali kwa
kitabu kipya chenye utata kuhusu madaia yua rais Zuma kujilimbikizia fedha
kimakosa ,wakisema kuwa kitabu hicho kimajaa makjosa na kinakiuka sheria ya
ujasusi.
Shirika hilo la Ujasusi limetishia kwenda mahakamani iwapo
wachapishaji wa kitabu hicho NP watakataa kukifutilia mbali kitabu hicho kwa
Jina “The Presidency Keepers: Those Keeping Zuma in Power and Out of Prison''-Wale
wanaomueka Zuma mamlakani na kutokwenda jela, kilichotungwa na mwandishi
aliyeshinda tuzo la uandishi wa uchunguzi Jacques Pauw.
Kitabu hicho kinadai kwamba Rais Zuma kwa muda wa miezi
minne alipokea mshahara kutoka kwa mfanyibiashara mmoja mbali na mshahara
anaolipwa na serikali na kwamba hakuutangaza mshahara huo kwa watoza ushuru wa
taifa hilo.
Baada ya nakala za kitabu hicho kuchapishwa siku ya Jumapili
katika gazeti moja, msemaji wa bwana Zuma alitoa taarifa ,akikana makosa yoyote
dhidi ya rais Zuma akidai kwamba alikuwa mwathiriwa wa kampeni mbaya ya
kumchafulia jina.
"Maswala ya ulipaji wa kodi ya rais hayana makosa
'',ilisema taarifa hiyo.
Nakala za kitabu hicho zinauzwa kwa kasi huku raia
wakijaribu kukinunua kabla ya kuisha katika soko.
©BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment
Maoni yako