November 08, 2017

MABALOZI WETU WASIWE WAZITO KUJENGA UCHUMI

NA GABRIEL MWANG’ONDA 

RAIS John Magufuli ametimiza miaka miwili madarakani tangu alipoapishwa Novemba 5 mwaka 2015. Miaka hiyo serikali imefanya mambo mengi ambayo si lazima kueleza hapa leo. Lakini itoshe kusema lipo jambo ambalo ninajikita nalo ili kuangazia miaka hiyo. Ni dimplomasia ya uchumi.

Diplomasia ya Uchumi (Economic diplomacy) limekuwa somo gumu sana kueleweka kwa mabalozi wetu. Yaani sisi wengine tumeiimba mpaka tukaona tupumzika tu kwasababu somo limekuwa gumu sana kwa balozi zetu. Binafsi nimeliongelea sana kwenye ma redio nyingi hapa ndani ya nchi na nje pia, lakini ndugu zetu wameamua kutoelewa tu hii dhana kitu ambacho kinaligharimu sana Taifa letu.
Ufukwe wa Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma. Ni miongoni mwa vivutio vya utalii.
Kila balozi utakae onana nae ukimuongelesha kuhusu hii diplomasia ya uchumi anasingizia udogo/ufinyu wa bajeti. Lakini hiki kamwe hakiwezi kuwa kikwazo kwa mtu mzalendo mwenye ubunifu alienuia kwa dhati kabisa kuitumikia nchi.

Si mambo yote yanahitaji fedha nyingi kuyafanya kuhusu hii dhana ya diplomasia ya uchumi. Balozi zetu hata utume baraupepe kwa vitu ambavyo ni vya kawaida sana bado hutojibiwa kabisa. 


Hii dhana kama ingetumika vizuri ingeweza sana kuinua hali yetu ya kilimo. Mara zote nimekuwa nikisisitiza kuwa soko letu la mazao hapa ndani ni dogo sana, halitoi motisha kwa vijana kulima kisasa na kibiashara, ni vyema tukawa na soko la uhakika nje ya Tanzania. 


Iwe mazao ya biashara ama ya vyakula, hiki ndicho kitu pekee cha kuanza nacho ni kuangazia masoko ya nje. Kwanini nasema hivyo, ni kwasababu ndicho tunachoweza kukifanya vizuri zaidi na kwa haraka pia kwa ubora unaotakiwa na kwamba zaidi ya 85% ya watanzania wanakifanya sasa na wako tayari kubadilika ili wanufaike zaidi, kwakuwa hakuna mtu anaependa umaskini.

Kwakuwa watanzania wengi ni wakulima basi inamaanisha wengi wanajitosheleza kwa vyakula. Wakulima hula mazao yao na kununua kidogo na kuuza pia kidogo, ndio maana tunasema mji wenye wakulima wa mbao wengi hauwezi kuwa soko zuri la mbao inatakiwa tufungue masoko yetu nje ya nchi kwenye uhitaji mkubwa ili kuwe na motisha ya kulima.

Nina uhakika pindi masoko yatakapotafutwa vijana wengi wapo tayari kuchapa kazi mashambani bila kusukumwa kwakuwa hata sasa wapo waliothubutu na wanaendelea hivyohivyo kibishi. Tunaweza kifanya kilimo kuwa kitamu na cha kisasa na kuvutia wasomi wengi huko.

Kilimo kikikua walau kwa asilimia 8% kwa miaka mitatu mfululizo utakuwa umewatoa wakulima zaidi ya nusu kutoka kwenye umaskini uliokithiri.  Watanzania wa vijijini hao 85% ni wachapakazi kwelikweli sote tunajua ndio maana ni nadra sana kwa njaa kutokea Tanzania kwakuwa kuna watu ni ma Stadi kwenye ukulima Japo ni ukulima duni na wakutosheleza familia zao tu.
Serikali kupitia Balozi zetu inaweza kabisa kupunguza tatizo la masoko kwa kuwatumia vizuri maafisa masoko/biashara walioko kwenye balozi zetu huko ughaibuni kwenye balozi zetu na sehemu nyinginezo. 

Si kila mkulima ana uwezo wa kusafiri na kwenda kutafuta masoko ya mazao yake nje ya nchi, lakini kodi zetu zinazoendesha balozi zetu huko nje zinaweza kutumika vizuri kwa kuifanya kazi hii kwa niaba ya wananchi, hii ndio njia nzuri ya matumizi ya kodi zetu hadi mtu unajisikia raha kulipa kodi ukijua kabisa kuwa inatatua kero zetu.

Mara nyingi mabalozi watatangaza kuwa hii nchi inahitaji, mihogo, ama asali ama kunde ama kitu chochote kile, lakini sasa pindi unapotaka kupata hizo taarifa vizuri ili uanze kuitumia hiyo fursa wanakimbia na wanakuwa hawana msaada kwako tena, mnakuwa kama mnahadaana watu.

Siamini kuhusu uvivu wa vijana wetu ila naamini wanahitaji msaada kidogo tu. Vijana wetu ni wachapakazi wazuri sana wapeni fursa kwa kukifanya kilimo kiwavutie.
Kwenye uteuzi wakati Katibu mkuu kiongozi alipokuwa akitaja majina ya wateule alipofika kutaja jina la katibu mkuu mpya Wizara ya mambo ya nje alistop kidogo, na kutia neno pale kwamba kwasasa Rais Magufuli kaamua kumuweka Mchumi nguli awe katibu wa hiyo Wizara ili asaidie kugeuza fikra za mabalozi wetu ziwe za kibishara zaidi.

Wakati wanaapishwa mabalozi Rais kasisitiza tena kuwa hafurahishwi na utendaji wa Wizara hiyo kwenye kuitekeleza diplomasia ya Uchumi, hilo si Jambo geni kwa sisi wengine tulioanza kupiga hizi kelele kitambo. Swali ni Je! Hawa watu wanamuelewa Rais kweli kwasababu huu wimbo haujaanza kuimbwa leo wala jana lakini hakuna matokeo chanya so far. 

Mbali na hili kuna kipindi Mh Rais aliweza kuwafanyia training hawa mabalozi na kuwaambia kuwa hawako huko kuwakilisha siasa tu bali kuleta wawekezaji, kutafuta masoko na mitaji, kuwa kiunganishi cha biashara zetu za huko, kutangaza utalii na vivutio vingine vya uwekezaji lakini inaonekana ile semina haikufua dafu coz response ni zero kabisa.

Namshauri katibu mkuu mpya awawekee malengo yanayotekelezeka kabisa KRA's, key results areas Kila mmoja aje atoe hesabu kila baada ya miezi sita kaleta investments kiasi gani, katafuta masoko kiasi gani. Iwe hivyo tu maana hamna namna na kama hawawezi wawapishe wanaoweza.

Balozi zote ziwe na tovuti zinzofanya kazi ambazo zitatumika kama chombo cha mawasiliano. Kama ni kumiliki tovuti kwa kila ubalozi ni gharama basi pawepo na tovuti moja inayo wakilisha balozi zote.
baruapepe na namba za simu zinazofanya kazi. Biashara ya kuuza Visa sio wakati wake huu.  Msimamo na mtizamo mzuri Rais ameshautoa kazi kwenu mabalozi, hili nalo liwe jukumu zito kwenu mulichukulie kwa uzito uleule wa kazi zingine za intelijensia na siasa. Tuna Vijana waliotayari kuitumikia nchi kwa ustadi sasa kama hawa wazee hawawezi basi tupeleke vijana wetu huko wakapige mzigo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako