November 22, 2017

WEMA SEPETU NA KISA CHA J.LO

NA MARKUS MPANGALA
NIMEPATA tabu kuandika makala haya tangu kumalizika mahojiano ya mwigizaji wa filamu na mshindi wa taji la Miss Tanzania, Wema Isack Sepetu aliyofanyiwa wiki iliyopita (Mei 24/2016) na kampuni yetu ya New Habari (2006) Ltd inayochapisha magazeti ya Rai, Mtanzania, Dimba, Bingwa na The African.
Mwandishi wa makala haya akiwa na mwanamitindo Wema Sepetu.
Tabu hii niliyopata ni kutokana na kuujua ukweli wa pili kuhusu maisha ya mlimbwende huyo. Ni mhariri wa Michezo wa gazeti dada na hili la Mtanzania, Mwani Nyangassa ndiye hasa aliyefanikiwa kumbana vilivyo Wema Sepetu na kujikuta akifunguka zaidi kuhusu maisha yake na mambo mengine yanayomzunguka kama msanii wa filamu, mjasiriamali na mwanasiasa na kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM). 

Mambo yaliyonishtua ni uamuzi wa Wema kueleza kiundani kabisa nini kinachoyasibu maisha yake kwa ujumla kwenye filamu na maisha binafsi. Makala haya naelezea mambo ya kujifunza kwa Wema Sepetu pamoja na kisa cha Jennifer Lopez. 


KUPOTEZA IMANI
Katika maisha tunaishi na watu wenye tabia tofauti. Tunaishi na watu wakorofi, wenye husda, wenye wivu, chuki na hasira na wengine wenye upendo na amani daima. 

Lakini kama unakosa watu wa kuweza kushirikisha mawazo yako au kushauriana nao mara nyingi unakutana na matatizo ya kukosa uamuzi. Mbaya zaidi ni pale unapojikuta unashindwa kusema jambo la moyoni kwakuwa dunia imekutenda kisha huna imani na mtu yeyote kuwmeelza tatizo lako.
Eneo hili Wema anakiri wazi wazi kuwa alipata wakati mgumu juu ya mtu wa kumwamini kumweleza mambo yake.

“Nilijikuta najiuliza sana, nani nitamwamini nimwambie mambo yangu. Ilifikia hatua sikuona wa kumwamini na hata nikajiona sina maamuzi sahihi. Kichwani sikujua nitaamua nini, kwakuwa sikuwa kwenye hali nzuri kiakili na kifikra,’ Tunachojifunza ni kuchagua marafiki waminifu pia, wazazi ndiyo watu waaminifu wa kwanza. 

 MADHARA YA UTOAJI MIMBA
Hapa ninapenda kukumbuka simulizi za kitabu cha ‘Ndoa ya Hawayani” kilichoandikwa na gwiji Beka Mfaume, ambaye pamoja na mambo mengine anasimulia matatizo makubwa ya utoaji mimba miongoni mwa wanawake. Anawataja wanaume kuwa chanzo ya yote hayo. Anawataja wanawake kuwa kufanya makosa kukubali kutolewa mimba. Si hilo, ninakumbuka msichana mmoja alifariki dunia baada ya kutolewa mimba vibaya katika kitongoji kimoja jijini Dar es salaam. 
 
Mwezi uliopita msichana mwingine alifariki baada ya kutoa mimba. Lakini tatizo hili likoje kwa Wema Sepetu? Kwanza tunatakiwa kutambua yeye ni binadamu ambaye ana hisia za uchungu, kupenda, masikitiko na kadhalika. Ndiyo maana alipokiri kutoa mimba sikushangaa. 

Ni habari ya pili kutoka maisha ya mrembo huyo ambaye baadhi ya mashabiki wanamwita ‘Drama Queen’.  “Nimehangaika sana, nimesafisha kizazi ili kuweka mambo sawa nipate mimba. Natamani mtoto na sijakata tamaa. Hata kwa kupandikiza nipo tayari kupata mtoto, nilinde heshima yangu kama mwanamke mwenye heshima kwa jamii,” alisema Wema.
Wema Sepetu akiwa na wahariri wa gazeti la michEzo la kila wiki la DIMBA
Wema anakiri kwa kusema, “Nilipokuwa na uhusiano na Steven Kanumba nilikuwa naishi na wazazi, niliwazia sana kama wakijua nina mimba wangejisikiaje? Na pia sikuwa tayari kwa kipindi hicho na utoto ulichangia nikatoa,”

Leo hii dada yetu na mrembo Wema analilia mtoto, na wapo akina dada wengi wanatoa mimba huko mitaani. Anzia mkoa wa Mara hadi Arusha, kisha nenda Mwanza hadi Dodoma na jiji la Dar es salaa. Funga safari hadi Mbeya kisha ingia kwetu Ruvuma na baadaye nenda Mtwara.

Tatizo la utoaji mimba ni kubwa mno na limesababisha madhara iwe kifo au kuharibu kizazi. Vyanzo vya yote hyao ni sisi wanadamu, na ambayo wengine hushauriwa na madakatri kulinda afya zao. Wema ni somo tosha kwa wale wanaobeba ujauzito kw abahati mbaya au makusudi lakini wanalazimika kutoa.

KISA CHA J.LO
Jennifer Lopez ni mwanamke ambaye alichukuliwa kama vile hajatulia. Uswahili kwetu tungesema ni ‘malaya’. Mwenendo wake katika mapenzi ulikuwa balaa. Alianzisha uhusiana na kuacha. Alifunga ndoa na kuachana. Kifupi kisa chake kinaonekana kama mwanamke asiyetulia na mwenye taswira mbaya kwa jamii. Alionekana mwanamke ‘mwingi wa habari’ labda tungesema ‘mpenda wanaume’. Swali moja tunaweza kujiuliza, je tatizo lilikuwa kwa Jennifer tu au ni yeye au wanaume walikuwa wanamzingua? Ni hilo pia kwa Wema tatizo ni yeye au wanaume wanamtumia kimpenzi?

Kisa cha Jennifer Lopez kinaanza kwa mumewe wa kwanza Ojani Noa. Ni ndoa yake ya kwanza, lakini ikavunjika na wakashinda mahakani kutatua mgogoro wao. Akafuata nguli Sean Combs mmiliki wa lebo ya mavazi ya  Sean John na muziki ya Bad Boys. Nguli huyo kimuziki aliitwa Puff Daddy au  kama aitwavyo sasa P.Diddy. 

Uhusiano wa kimapenzi wa Diddy na Jennifer ulivutia watu wengi ingawa walijua P.Diddy ni mwanamuziki wa Hip Hop kwamba ni mgumu, sasa inakuwaje mtu mgumu anaingia penzini na mrembo laini kama Jennifer?
Zilikuwa simulizi tamu kama za Juma Nature na Sinta. Jennifer alitunga wimbo wa “I am Real” aliomshirikisha Ja Rule ikiwa ni sehemu ya masimulizi ya mahusiano ya kimapenzi aliyopitia kwa nguli huyo. 

Nakumbuka naye P.Diddy ahakubaki nyuma enzi zile, akatunga wimbo wa ‘I Need A Girl” aliomshirikisha Usher Raymond na bishoo Loon. Huyu Loon alikuwa kichwa kikali cha Lebo ya Bad Boys ambayo ni ya kitambo katika muziki na ilianzishwa na Diddy mwenyewe akiwa na washkaji zake. 

Kwenye vesi ya mwisho kabisa Diddy ana-rap kama ifuatavyo;
“I had a girl that would've died for me
Didnt 'preciate her so I made her cry for me
Every night she had tears in her eyes for me,
“First we were friends the become lovers

Tafsiri isiyo rasmi ni hivi;
Nilipata mwanamke aliyekuwa tayari kwa lolote,
‘Hata kufa kwa ajili yangu,
“Sikumheshimu, nilimfanya anililie
“Daima usiku alimwaga machozi kwajili yangu,
“Kwanza tulikuwa marafiki,
Baadaye tukawa wapenzi,

P.Diddy alikuwa akimlilia wazi wazi Jennifer Lopez, ingawa hawakuweza kurudiana tena kama wapenzi waliotarajia kufunga ndoa.  Cris Judd, alikuwa mcheza dansi wake ambaye alianza naye uhusiano baada ya kuachana na Diddy. Hawakudumu. Wakaachana kama ilivyokuwa kwa Wema Sepetu, hadumu kwenye mahusiano. 

Ben Affleck mwigizaji mashuhuri wa Hollywood. Filamu yake The Town ninaipenda zaidi kuliko zingine. Wengi wanaifahamu filamu hii. Affleck alianza uhusiano na Jennifer. Hawakudumu, wakaachana. Marc Antony Mwanamuziki, prodyuza na mwigizaji mkongwe. Alitumbukia kwenye mapenzi na Jennifer Lopez. Wakafanikiwa kuzaa watoto wawili mapacha Maximilian David na Emme Maribel. Hadi hapa utaona jinsi Jennifer alivyozunguka kimapenzi hadi kuapata watoto. Ni kama kisa kinachomfuata Wema Sepetu.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako