November 10, 2017

ZAWADI YA VITABU

Zawadi ya vitabu niliyopewa na Molio Baldwin. Asante sana rafiki
Mimi na Molio Baldwin ni marafiki Facebook. Tumetimiza miaka mitano ya urafiki wetu kwa kufanya kitu tofauti. Sote ni wapenzi wa kusoma vitabu. Badala ya maneno ya pongezi tuliamua kununuliana vitabu vitano kadiri ya umri wa urafiki wetu. Leo nimepokea zawadi yangu ya vitabu (pichani). 



Namshukuru sahibu yangu huyu kwa ubunifu na uungwana. Nina bahati kufahamiana naye. Daima nitaenzi urafiki huu kwa msemo wa bondia Deotany Wilder,"A King don't chase the peasant. A King takes kings." Aghalabu unatakiwa kupata marafiki bora na vitu maridadi.
Kwako msomaji wangu hapa, mimi nakusihi, madhali muda unakuwapo, ni vema ukajipatia maarifa kupitia vitabuni.

#KitabuNiSilaha.
#AsanteMolio.
©Markus Mpangala, Sinza Kijiweni, Dar es salaam
Novemba 9/2017
                                            MOLIO BALDWIN 
Molio Baldwin

Zawadi ya vitabu niliyompatia Molio Baldwin.
So facebook wakatukumbusha kuwa sisi tu marafiki kwa miaka mitano....nikawaza zawadi yani out of blue..nikajua sisi wote tunapenda vitabu basi tukakubaliana tununuliane vitabu idadi ya urafiki tuliodumu....sikuwahi kumuona popote huyu kaka zaid ya.kumsoma hapa kwa ukurasa tu, and so today kanipa zawadi zangu za urafiki wetu namm nikampa na yeye, Mungu ni mwema na hutukutanisha na watu wenye faida sana na mafunzo maishani be it good or bad. Asante sana kaka Markus Mpangala hivi vitabu vitaongeza ufahamu zaidi na zaidi na umebarikiwa zaidi na zaidi pale ulipotoa. 
Barikiwa sana.
Wako msoma vitabu mwenzio na miaka ya urafiki iendelee kuja na mazawadi kemkem.
Asante.
#PeopleIvalue
©Molio Baldwin, Dar es salaam
Novemba 9/2017.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako