...TULIPOFIKA hapa tukiwa
tunatafakari sehemu ya kupita Mdogo wetu Thobias (mwenye tisheti nyekundu) akaniambia
brother nimekumbuka movie moja inaitwa The Hard Way Is The Only Way. Akanielezea
kidogo maana jamaa anapenda movie sana.
Moja ya msitu ulioko eneo la jiwe maarufu Tingitingi.
Karibu na ukuta wa mawe wa wampoto.Hapa ilikuwa tunasikiliza sauti za kanga
pori tu na kuona kenge na mijusi wa rangi rangi.
Nchi hii ina historia toka maeneo ambayo unakutana na
wasimulizi waliohifadhi kumbukumbu za miaka mingi. Wasimulizi hawa hawajawahi
hata kukutana na mtaalamu yeyote wa masuala ya wahifadhi kumbukumbu katika Taasisi
yoyote kama ilivyo wale wanahistoria au watu wa Maliasili. Shughuli za binadamu
zinazofanyika maeneo haya zitasababisha wanyama kama ngedere kutoweka.
Ukitaka kujua habari za “Dragon” aliyeko maeneo ya Jiwe la Stima
au Tingitingi ni miongoni mwa historia iliyopo hadi sasa. Mabaki na mapango
yaliyotumiwa na mababu kujisitiri wakati vita.
Picha ya chini nikiwa na Kizito, Thobias katika Forodha ya
Lundu hapa Nyasa.
Honorius Mpangala
Desemba 28/2017
Lundu, Nyasa
No comments:
Post a Comment
Maoni yako