Na KIZITO MPANGALA
Abdu-Rahman Ibrahim bin Sori
alizaliwa mwaka 1762 katika mji wa Timbo kitongoji cha Futa Djallon (sasa ni
nchi ya Guinea) huko Afrika Magharibi katika jamii ya kabila la Fulani. Baba yake
alikuwa mfalame wa mji wa Timbo (Guinea) na hivyo Abdul-Rahman alikuwa ni
mwanamfalme (Prince)
Katika makuzi yake alipelekwa
mjini Timbuktu kujifunza masuala yanayohusu dini ya Kiislamu. Akiwa mjini
Timbuktu, Adul-Rahman alijifunza lugha nne za makabila ya Afrika Magharibi
pamoja na lugha ya Kiarabu na aliporudi mjini timbo alijiunga na jeshi la baba
yake ambaye alikuwa kiongozi wa kitongoji cha Futa Jallon mjini Timbo (sasa ni
Guinea).
Abdul-Rahman alipofikisha miaka
26 alifanywa kuwa kiongozi wa jeshi hilo liliokuwa na askari 2000. Kazi yake
kuu katika jeshi hilo ilikuwa kuhakikisha ulinzi wa pwani yote ya Timbo
(Guinea) umeimarika na kuliweka jeshi lake tayari kwa kupambana na adui yeyote
ambaye angeivamia pwani hiyo.
Kutokana na uwezo wake wa
kijeshi, Abdul-Rahman aliwindwa sana na wazungu wa Uingereza ambapo mwaka 1788
wazungu hao walifanikiwa kumteka na kusafiri naye hadi katika mji wa
Mississippi nchini Marekani kisha aliuzwa na kuwa mtumwa. Akiwa mjini Mississippi
laitumikishwa kufanya kazi katika mashamba ya pamba ya tajiri Thomas Foster kwa
zaidi ya miaka 38 kabla ya kuachiwa huru.
Kutokana na uwezo wake katika
kilimo cha pamba alichokuwa akifanya huko Mississippi, Abdulrahman alikuwa
akijishughulisha pia na kilimo cha bustani ya mboga za majani, bustani hiyo
ilikuwa ni ya kwake mwenyewe. Na mwaka 1894 alimuoa binti Isabella mtumwa
mwenzake katika mashamba ya pambo walimokuwa wakifanya kazi.
Abdul-Rahman alibahatika
kupatana vizuri na dakitari wa merikebu ya Waingereza, John Cox ambaye
alimkaribisha nyumbani kwake mara kwa mara kwa kuwa kwa mara ya kwanza
walionana katika pwani ya mji wa Timbo (Guinea) wakati alipotekwa na Waingereza
hao. Dokta John Cox alimuomba tajiri wa mashamba ya pamba, Thomas Foster
kumuachia huru Abdul-Rahman Ibrahim bin Sori ili arudishwe kwao Timbo (Guinea)
lakini tajiri huyo alikataa kufanya hivyo kwa kuwa Abdulrahman alikuwa
mchapakazi hodari katika mashamba hayo. Dokta John Cox aliendelea kubembeleza
kwamba Abdul-Rahman aachiliwe huru mpaka alipofariki bila mafanikio ya ombi
lake. Baada ya dokta John Cox kufariki, kijana wake wa kiume alikendeleza
kubembeleza kwamba Abdurahman aachiliwe huru.
Mwaka 1826 Abdu-Rahman Ibrahim
bin Sori aliandika barua kwa ndugu zake huko Timbo (Guinea). Baada ya kuiandika
barua hiyo, ilichukuliwa na Andrea Marschalk ambaye alikuwa Mdachi na kazi yake
ilikuwa ni katibu muhtasi. Barua hiyo ilipelekwa kwa Seneta wa jimbo la
Mississippi, Thomas Reed ambaye alikuwa katika matembezi yake wakati huo
kuelekea mjini Washington, hivyo aliibeba barua hiyo na kuipeleka kwa Balozi wa
Marekani nchini Morocco na kisha kupelekwa mjini Timbo (Guinea). Ilipelekwa nchini
Morocco kwa sababu Abdul-Rahman aliiandikwa kwa lugha ya kiarabu, hivyo
alidhaniwa kuwa ni mwenyeji wa Morocco.
Barua ilipokelewa na kupelekwa
kwa Sultan wa Morocco. Baada ya Sultan kuisoma barua hiyo, alituma ombi la
kuachuliwa huru Abdul-Rahman Ibrahim bin Sori. Ombi hilo lilitumwa kwa Rais wa
Marekani wakati huo, John Quincy Adams.
Mwaka 1829 tajiri wa mashamba ya
pamba, Thomas Foster alikubali kumuachiliwa huru Abdul-Rahman Ibrahim bin Sori
bila kumpa ujira kwa kazi aliyoifanya mashambani humo, kwa makubaliano kwamba
arudi Afrika na siyo kubaki Marekani akiwa huru.
Abdul-Rahman na mkewe kabla
hawajaondoka Marekani, walizunguka katika miji mingi ukiwemo Washington D.C
ambapo alionana ana kwa ana na Rais John Quincy Adams. Abdul-Rahman aliomba kubaki
kwa muda mjini Mississippi ili ajiandae na familia yake kurudi Afrika. Taarifa hii
ilimfikia tajiri Thomas Foster ambaye alichukulia taarifa hii kuwa Abdu-Rahman
amekiuka mkataba aliokubaliana naye.
Miezi kumi baadae, Abdul-Rahman
na mkewe Isabella walikuwa wamepata nusu ya fedha kwa ajili ya kulipia uhuru wa
watoto wao ili wasiwe watumwa Mississipi nchini Marekani wakati wao wakirudi
Afrika. Baada ya kufanya hivyo, Abdul-Rahman na mkewe Isabella walirudi Afrika
na kufikia mjini Monrovia, Liberia bila watoto wao. Abdul-Rahman Ibrahim
aliishi kwa muda wa miezi miine tu nchini Liberia na kufariki kutokana na
kuugua kwa muda mrefu. Hakuiona tena Timbo, Futa Djallon wala watoto wake tena.
Fedha ambazo walizipata
walipokuwa Mississippi walilipia uhuru wa watoto wao wawili tu ambao baadaye
waliwasili mjini Monrovia, Liberia na kuishi na mama yao, Isabella. Naye tajiri
wa mashamba ya pamba mjini Mississippi, Thomas Foster alifariki mwaka huo huo
ambao alifariki Abdul-Rahman Ibrahin bin Sori na ukwasi wake uligawanywa kwa
mtoto wake na watoto na wajukuu wa Abdul-Rahman ambao alibaki katika kasri ya
tajiri huyo kama watumw. Baada ya kugawana, walisambaa maeneo mbalimbali kusini
mwa Mississippi.
Mwaka 1977, Profesa wa
Historia, Terry Alford aliandika kitabu kilichokuwa na simulizi ya maisha ya Abdul-Rahman
tangu alipokuwa Afrika hadi alipotekwa na kurudi tena Afrika. Kitabu hicho
kinaitwa PRINCE AMONG SLAVES.
Mwaka 2006, kizazi cha
Abul-Rahman na kizazi cha Thomas Foster viliungana kama wanafamilia katika
kasri ya Thomas Foster na kuishi pamaoja katika kasri hiyo na kushika maeneo
yote ya mashamba ya pamba.
Mwaka 2007, mwongozaji wa
filamu nchini Marekani, Andrea Kalin alitengeneza filamu iliyokuwa ikisimulia
maisha ya Abdul-Rahman Ibrahim bin Sori na kutolewa rasmi mwaka 2008. Filamu hiyo
imebeba jina la kitabu kilichoandikwa na Profesa Terry Alford, PRINCE AMONG SLAVES.
0692 555 874
No comments:
Post a Comment
Maoni yako