NA SAMWEL CHITANYA.
Ilkuwa
ni Furaha kubwa sana kuwaona vijana wa Serengeti Boys wakiwa wanashindana na
timu kama Mali,Niger, Congo na timu nyinginezo zilizoshiriki mashinano Yale. Ingawa
hatukufanya vema sana lakini angalau nasi tulionekana kama tunaweza. Nani
alikuwa hafurahii kumuona Ramadhan Kabwili akiwa langoni na wenzie kama akina Ally
Nganzi, Nasho Naftari, Nickson kibabage, Abdi Suleiman, Said musa, Yohana
Nkomola kwa kuwataja wachache.
MWAKA
2017 utabaki kuwa mwaka unaokumbukwa na Watanzania wapenda soka. Mwaka huo ni
mwaka ambao timu yetu ya vijana Serengeti Boys ilishiriki kwa Mara ya kwanza
mashindano ya vijana kwa Afrika tangu Tanzania iwepo. Ushiriki huo ulikuja
baada ya miaka 37 tangu Tanzania iliposhiriki kwa Mara ya kwanza fainali za
kombe la Mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON mnamo mwaka 1980.
Kikosi cha Serengeti Boys |
Hakika
ilikuwa ni furaha na Faraja kubwa kwa soka la Tanzania. Tukiacha ujanja ujanja
na kuamua kusimia soka kwa uhakika tunaweza fika tunakohitaji.
Mwaka
2019 Tanzania itakuwa mwenyeji Wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana
walio na umri chini ya miaka 17. Tuliomba kuwa wenyeji Wa michuano hiyo maika
miwili iliyopita. Ni jambo la kujivunia kuona mashindano makubwa ya vijana kama
hayo yakifanyika katika ardhi yetu. Hii inaweza kuwa njia ya kuelekea kuomba
kuandaa mashindano ya wakubwa maarufu kama AFCON.
Bila
shaka tunaweza kuandaa AFCON miaka kadhaa ijayo maana kama tunashindwa
kushiriki fainali hizo kwa njia ya kawaida, kundaa ndio njia pekee itakayo
tuwezesha kushiriki mashindano hayo.
Tunaenda
kuwa wenyeji Wa michuano ya vijana hapo mwakani lakina bado Nina hofu na
ushiriki wetu katika michuano hiyo. Hofu yangu haiko katika viwanja vitakavyo
tumika la hasha!! Kama viwanja tunavyo, tuna uwanja wa taifa, uwanja Wa Uhuru,
uwanja Wa Gombani kule Pemba, uwanja Wa Amani unguja, Uwanja Wa Azam complex na
Uwanja Wa Kaitaba pia. Hofu yangu iko katika ushiriki wetu uwanjani maana pale
ndio sehemu pekee inayoonesha namna gani tumejiandaa.
Soka
ni mchezo unaochezwa hadharani na kila Mwenye uwezo Wa kuona anaona. Soka siyo
bao au karaka usema utajificha mahali Fulani ucheze hapana. Hadi wakati huu
sijasikia chochote kuhusu mashindano hayo nikiwa na maana ya maandalizi yetu
kama wenyeji, kuanzia kwa Shirikisho la soka FFF, Serikali na wadau Wa soka kwa
ujumla wake. Wote wako kimya.
Sijasikia
timu yetu ikicheza mechi za majaribio kujiandaa na mashindano hayo, au bado
mapema??. Soka linahitaji maandalizi ya muda mrefu kama tunahitaji kushindana
katika michuano hiyo basi tulikuwa hatuna budi kuanza maandalizi mapema Mara tu
baada ya kupewa taarifa rasmi kama tumekubaliwa kuwa wenyeji wa michuano hiyo.
Inawezekana
Mimi ndio Niko nyuma pengine timu imekwisha andaliwa na iko kwenye mazoezi ya
kujianda kwa michuano hiyo hapo mwakani sijui. Kama tunania ya kushiriki hakuna shida
tunaweza endelea na taratibu Nyingine. Maana kushiriki na kushindana ni mambo
mawili tofauti. Lakini tukumbuke hakuna njia ya mkato kwenye kandanda,
usipojiandaa vema utaumbuka tu.
Tunatakiwa
kujiandaa kushindana na siyo kushiriki, vinginevyo tunatolewa mapema na
kuwaacha wageni wakichuana kwenye ardhi yetu jambo ambalo ni aibu kubwa, kwa
muandaaji Wa mshindano kundolewa mapema. Rai yangu kwa Serikali na shirikisho
la soka TFF tutumie muda huu uliobaki kuindaa timu yetu.
Tusitegemee
muujiza kama tutakuwa na maandalizi ya zima moto. Soka linahitaji maandalizi ya
muda mrefu siyo kama muziki usema utaandika mashairi Leo, kesho
ukarekodi,keshokutwa wimbo utoke na watu waanze kuuimba la hasha!!!
Soka
haliko hivyo. Uchaguzi ulishamalizika, sasa ni wakati kusimamia soka letu ili kusogea mbele. Mheshimiwa Rais wa TFF kama kuna jambo ambalo
litakufanya usisahaulike miongoni mwa Watanzania wapenda kandanda basi ni
Ushiriki mzuri Wa timu yetu ya Serengeti boys katika michuano ya Afrika hapo
mwakani.
Uongozi
Wa Leodgar Tenga unakumbukwa na wapenda soka wote hapa nchini pamoja na
kuifanya TFF kuwa taasisi inayoaminika na kujenga misingi bora ya utawala kuna
jambo la ziada linalofanya uongozi ule uendelee kukumbukwa nalo ni ushiriki Wa
timu yetu ya taifa katika michuano ya CHAN iliyofanyika mwa Mara ya kwanza
mwaka 2009 pale Ivory cost.
Uongozi
Wa Tenga ulifanikisha hilo kwa kushirikiana na Serikali na wadau Wa soka na
kuifanya Tanzania kuwa nchi iliyokuwa inaogopeka kwenye kandanda Afrika
mashariki na kati yote na hata Afrika kwa ujumla.
Hata
mtangulizi wako bwana Jamal Malinzi pamoja na mapungufu yalijojitokeza kwenye
uingozi wake, alijitahidi kuiweka Tanzania kwenye ramani ya soka kwa
kufanikisha kuifikisha Serengeti boys kwenye fainali za mataifa ya Afrika kwa
vijana wenye Wa umri chini ya miaka 17 naye anaheshima zake. Kipindi cha
uongozi wake ndipo tulifanikiwa kupata uwenyeji Wa michuano hii hapo mwakani
anastahili pongezi.
Rais
Wa TFF na kamati yako ya utendaji huu ni wakati wenu kuipaisha Tanzania kwenye
kandanda kupitia michuano hii itakayo fanyika mwakani ambayo sisi ni wenyeji.
Ushiriki
mzuri wa Serengeti boys unaweza kuwa ni kampeni tosha katika uchaguzi ujao Wa
TFF. Tujiandae kushindana na ikiwezekana kulibakisha kombe nyumbani kwa Mara ya
kwanza tangu kuumbwa kwa dunia. Itawezeka endapo tu tutakuwa na maandalizi
mazuri na kuwepo kwa ushirikiano baina ya TFF, Serikali na wadau Wa soka kwa
ujumla.
Watanzania
wanapenda sana kandanda, pamoja ma madhaifu yote yanayojitokeza kwenye
uendeshaji Wa mpira wetu lakini bado hawachoki kwenda viwanjani kuzitazama timu
zao. Nawakumbusha TFF, Serikali na wadau Wa soka wote kuwa mwakani Tanzania
itakuwa mwenyeji Wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 17. Tuna miezi 12 tu ya kujiandaa. Wahenga walisema"
Kiuangukacho majivuni hakiishi kupulizwa.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako