NA HONORIUS
MPANGALA
Awali sikulifahamu hilo kwa Nandy lakini katika picha mnato hii nikiri wazi naye ni mmoja wale ambao huweza kuhusika vyema popote kwa mazingira ya mjini au kijijini. Wakati Aslay na timu yake ya kuchukua picha mnato wa wimbo huo ilipofika kijijini hapo wakanusa harufu ya Pilau lililokuwa likiivishwa katika mgahawa mmoja hapo Matimbwa magengeni. Ulikuwa mgahawa Wa mama Regina Shija almaarufu kama mama Boni.
Ni
mwendo wa Kilometa 30 kutoka Mlandizi ili ufike Kijiji cha Matimbwa. Pia ni
kilometa 8 ukitokea Bagamoyo Mjini ili ufike hapo kijijini. Ilinichukua masaa
yasiyo zidi manne kutoka Morogoro hadi nafika kijijini hapo. Yawezekana
ikawa ni jina la kijiji ambacho wengi wao wasiweze kukifahamu kama ilivyo Msata
katika wilaya hiyo ya Bagamoyo. Ni eneo la jimbo la mheshimiwa Shukuru
Kawambwa. Wakazi wake wengi wakiwa Wazaramo,huku Wakwere nao wakiwepo kwa
kiasi.
Nyumba mojawapo iliyoko katika video ambapo Nandy kaonekana kaegemea kwenye ukuta huku akiimba |
Wakati
napanda gari Mlandizi wenyeji wangu Mathayo Venance na Saidi Zimbwe wakanipa
maelezo shukia kituo cha Matimbwa Magengeni. Nilikuwa na shauku ya kuijua
Matimbwa na Bagamoyo kwa kweli na nilifika salama na kufanya kazi yangu vyema. Jambo
kubwa ninalotaka kuwajuza sio mimi nilisafiri vipi kufika huko. Bali nataka
nikupe umaarufu wa Matimbwa ambao hata mtayarishaji wa picha mnato Hans Cana
autambue vyema.
Ni
katika picha mnato ya wimbo wa ‘Subakheri mpenzi’ ulioimbwa na Aslay na Nandy
ulimfanya mtayarishaji Hans Cana awapeleke Kijiji cha Matimbwa na kufanya video
huko. Kama
umjuavyo msanii Aslay huwa mtu wa kupenda picha mnato ambazo hupendwa na watu
wa viwango vyote vya Maisha. Hupenda kufanya video akiwa kijijini na huvaa
uhusika haswa uhalisia Wa mazingira.
Pikipiki iliyotumika katika wimbo wa Subakheri Mpenzi |
Awali sikulifahamu hilo kwa Nandy lakini katika picha mnato hii nikiri wazi naye ni mmoja wale ambao huweza kuhusika vyema popote kwa mazingira ya mjini au kijijini. Wakati Aslay na timu yake ya kuchukua picha mnato wa wimbo huo ilipofika kijijini hapo wakanusa harufu ya Pilau lililokuwa likiivishwa katika mgahawa mmoja hapo Matimbwa magengeni. Ulikuwa mgahawa Wa mama Regina Shija almaarufu kama mama Boni.
Harufu
ya pilau ikamfanya Nandy awe Wa kwanza kusogelea mgahawa huo. Kitu pekee
alichokifanya Nandy ni kuingia hadi jikoni na kumwomba Mama Boni ampatie pilau
lenye samaki na mboga za majani. Hiyo
ikawafanya na wengine kusogea hapo kama Hans Cana na timu nzima kuagiza pilau
hilo. Wakati chakula kikiendelea ndipo Nandy alipokiri kuwa aliisikilizia
harufu ya pilau akiwa mbali na mgahawa huo ikabidi asogee hapo.
Wakiwa
chini ya kiongozi Wa kiongozi Wa kikundi cha ngoma Vanga bwana Kondo Milonge
kila kitu kilienda sawa. Katika
picha mnato ya wimbo huo kuna pikipiki ambayo anaonekana Aslay kaikalia ambayo
ni ya aina yake. Ni pikipiki ambayo iko katika mfumo Wa gari na hiyo yote ni
kazi ya mmiliki ambaye ni Fundi pikipiki kijijini hapo.
Ile
pikipiki ni ufundi wa Fikiri Gombe almaarufu kama Magoso. Nafikiri wengi
mtakuwa mmetambua kwanini Fikiri kapewa jina la Magoso ni kutokana na mchezaji
Wa zamani Wa Simba aliyeitwa jina la Fikiri Magoso. Mwonekano
Wa ile pikipiki ulimfanya Hans Cana ahitaji kuitumia katika kazi yake. Ina
usukani kama Wa gari,Krachi yake inakanyagwa kama ya gari,hata gia pia hutumia
mkono kuingiza na kutoa.
Ni
upande wa mafuta tu ambao uko sehemu yake kama zilivyo pikipiki zingine ila
haufabani kwa mwonekano kwani badala ya kunyonga yeye Magoso alitengeneza mfumo
Wa kukandamiza kwa kiganja chake.Hiyo ndo pikipiki ya Fundi Fikiri Gombe
almaarufu kama Magoso.
Katika
kipande ambacho Nandy kaonekana kasimama akiwa ameegemea ukuta Wa nyumba huku
akiimba,sasa mita chache ndio kuna Nyumba anayoishi huyo Bint Kessy. Aslay
akakaribishwa chakula hapo jamaa 'hakuvunga' akajisogeza na mmoja ya watu
aaliotanguzana naye na wakala chakula katika hali ya kawaida kabisa. Wanaposema
ishi kulingana na mazingira basi huyu kijana naweza kusema ana nyendo kama za
Juma Kassim almaarufu Juma Nature.
Ukitaka
kujua uhusika wa watu katika picha mnato za wenzetu wa mataifa mengine huwa
wanalipwa. Kitendo cha kutoka katika video lazima ulipwe kwa kile
utakachokifanya. Lakini yawezekana hapa kwetu Tanzania hali ikawa tofauti na
inavyofikiriwa.
Katika
picha mnato hiyo wako waliolipwa kutokana na kupangwa mapema uhusika wao.
Lakini wako ambao hawakulipwa na waliridhika kwa mioyo yao vitu vyao au nyumba
zao zitumike na mambo kwenda bila taabu yeyote. Yawezekana
mwonekano wa Aslay na jinsi alivyoifanya picha mnato hii kuwa ya mazingira ya
kijijini ndo ulipelekea hata wanakijiji waone haina haja ya kumtoza chochote.
Walijiuliza kaacha vijiji vingapi hadi aje Matimbwa?
Huu
ndo Utanzania ambao mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwaachia Watanzania.
Kuishi kijamaa kuonana tuko ssawa kama katiba yetu inavyoeleza.
Licha
ya hayo yote kufanyika hapo lakini kumbe baba aliyemzaa msanii Feruoz anaishi
kijijini hapo.Hata msaani maarufu Wa muziki Wa Dance Muumini Mwinjuma anatokea
huko. Nikionyeshwa dad yake Muumini akiyeolewa hapo kijijini pia.Unaambiwa hata
marehemu Banza Stone alikuwa mwenyeji sana Matimbwa.
Hiyo
ndiyo Matimbwa ya Wazaramo ambayo Mtayarishaji Hans Cana aliamua kumpeleka
Aslay na Nandy kwenda kufanyia picha mnato ya wimbo Wa Subalkheri mpenzi.
Waweza
ingia katika mtandao kama YouTube na kujionea maandalizi ya picha mnato hii na
ukajionea Mengi zaidi ya niliyoeleza. Si unajua 'behind the Scene' ndo pahala
ambapo watu huweza jione kila jambo lililojiri katika utayarishaji Wa picha
mnato ya filamu au wimbo.
0753 44 92 54
No comments:
Post a Comment
Maoni yako