MIAKA mitano iliyopita nilipata
kuandika kuwa, ‘utamaduni wa wananchi kupigwa risasi, kushambuliwa kwa riasi za
moto, kushuhudia wapendwa wao wakifariki dunia mbele ya macho yao, kuna matokeo
hasi yenye athari kubwa nchi yetu.
Nilisema wananchi wanazoeshwa
kupigwa risasi za moto. Wanazoeshwa kuuana. Watatamani kuuana. Watatamani
kujiua. Wanazoeshwa kuchukia kwa vitendo vinavyoumiza mioyo yao.
Mwishowe nilisema kuwa wananchi
hawa wanapotenda jinai wakitumia mapanga, marungu au visu, jawabu ni kwamba
wanatumia vitu hivyo kwasababu ‘hawana bastola wala bunduki’.
Nilisema hali hii inachochea
ghadhabu inayoota mizizi na kuumba tabia za chini kwa chini kiasi kwamba
madhara yake hayawezi kuonekana haraka, lakini yatakuwa makubwa sana.
Nimepokea taarifa za kufariki
dunia mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji
katika shahada ya
Manunuzi na Ugavi, Aqulina Akwiline (AKWILINA),
mwenyeji wa wilaya ya Rombo, Kilimanjaro. Binti huyo anatajwa kuwa alikuwa
anatumia usafiri wa daladala za kutoka Makumbusho kwenda Mabibo. Tumeambiwa risasi zilipigwa hewani. Kwahiyo mkoa wa Dar es salaam
una barabara za hewani zinazotumiwa na Daladala?
SWALI; Hivi kama risasi
zilipigwa hewani ina maana daladala hiyo ilitumia ‘Flyover’ ipi kutoka Gerezani
(Kariakoo) kwenda Makumbusho via Mabibo? Aibu ilioje!
Pumzika kwa amani mrembo
Akwilina.
--MARKUS MPANGALA©Andunje wa
Fikra
No comments:
Post a Comment
Maoni yako