February 01, 2018

WANYASA NISIKILIZENI KWA MAKINI.

NA HONORIUS MPANGALA
Kwanza mtoto wenu nimefika salama kutoka safari yangu ya Dodoma. Nishafika kwa Mbaraka Mwishee salama. Leo naomba nishiriki nanyi haya yawezekana yalikuwa yananisumbua kila siku halafu nilawa naogopa kuwaambia wenzangu ukweli. Lakini kuna mtu anaitwa James Chiggs ni kama amenifanya nami niondoe ile hofu ya kufikiriwa tofauti. Kama naweza kutukanwa na mashabiki Wa Simba na Yanga kutokana na Kalamu yangu kwanini niogope kwa nyie ndugu zangu.

Miaka ya Nyuma aliwahi kutokea mmoja Wa viongozi Wa kisiasa kwa ngazi ya uwaziri aliitwa ALFRED TANDAU nafikiri mnamfahamu nyie Wanyasa na hata Watanzania kwa ujumla kwani alikuwa Waziri Wa mawasiliano.
Hadi naondoka Duniani hakuna unachoweza kusema hii ni alama ya Tandau aliyoifanya Nyasa. 
Miaka ikaenda tukapata mwakikishi Wa wananchi kupitia jimbo la Mbinga Magharibi Mh. Tadei Luoga kila mmoja anakumbukumbu za huyu mtu sitaki kusema kwasababu sio vyema kuwazungumzia watu ambao mwenyezi mungu aliwachukua kwa ubaya walioufanya. Hata Jambazi kwao wanafanya matanga.

Kuna kosa kubwa ambalo limekuwa la muda mrefu kutokana na yale yaliyotokea kwa mababu zetu. Imani potofu ilikimbiza watu yawezekana hata malalamiko yanayotokea sasa ni mshahara Wa mbegu chafu iliyosababishwa na mababu waliokuwa magwiji na wakawafanya vijana Wa zamani wakakimbia kwetu kwasababu za kujisalimisha. 

Leo hii mandeleo ya Nyasa tunapoyahitaji kwa jicho la kuyapigania lakini tunapaswa kufahamu wako ambao mioyo yao ilishakufa kutokana na mambo waliyofanyiwa na mababu miaka hiyo. Hivyo uwepo wao katika kitengo fukani bado kunawapa shaka ya kuwa wenye kuhitaji harakati za kweli juu ya maendeleo ya Kwetu.Siwezi kuwalaumu sana kwa waliokutana na changamoto ya namna hiyo.


Lakini pia baada ya Luoga alifuata Kepten Komba. Sitaki kumzungumzia kwa ubaya wake wala uzuri wake kwasababu ameshatangulia mbele ya haki.
Maendeleo ya mahali huletwa na watu na sio ngedere au Mbuzi. Hakuna kitu kinakikera kama hizi harakati ambazo wanazifanya wanyasa walioko mjini kwa kuonekana wanajua mambo kwa kutolea mifano mbalimbali lakini hawajawahi kufika eneo husika ambalo wao hujisemea ndo kwao.

Utasikia kikao cha wanyasa waishio Dar es salaam kitafanyika Lamada. Kudadadeki mnashindwa kwenda Nyasa mnajifanya mnakusanyikia mjini. Kama unaona Nyasa sio kitu kwako kwanini uusemee moyo kwa kutaka kuonekana machoni pa watu ni miongoni mwa wapigania maendeleo ya Nyasa halafu una miaka 10 mjini hata Nyasa huijui. Halafu mnasema oneni wezetu wachaga sijui wanafanya moja mbili tatu. Mi najiuliza uliwahi kwenda Nyasa ukasikia wanachokisema usiishie kupiga simu.

Wilaya ya Nyasa kama inavyotambulika ina tarafa tatu. Yaani Mpepo Ruhekei na Ruhuhu. Hakuna tafara imekosa watu Wa kuisemea kama ya Ruhuhu. Hakuna uwiano wa miradi kati ya tarafa hiyo na hizo zingine. Wakati barabara ya Kitai hadi Lituhi iko chini ya Tanroad lakini hakuna anayekumbuka hata kuuliza labda kwa wahusika hivi na kule vipi. 

Yawezekana Mimi niko karibu sana watu wa tarafa ya Ruhekei kutokana na kupata kwangu elimu ya Sekondari Liuli na pia Mamangu Binti Machusa kwao Ng'ombo hivyo Ruhekei kwa wajomba na Ruhuhu kwa Baba. Huwa naumia rohoni ninapoona harakati za kuifanya Nyasa ifanane na Msoga au Chato inafanywa na Wanyasa Wa Ruhekei pekee najiuliza hivi wale Wa Ruhuhu ni kweli wamesusa kwao. 

Hakika kama kutelekezwa basi rumetelekezwa kwelikweli. Maana kila niki fikiria adha tuipatayo kwa upande Wa Mawasiliano na uchukuzi najiuliza hivi kama serikaki inasema inapeleka maendeleo kwa wananchi ,hivi hao wananchi ni Wa maeneo gani?.

Wakati komredi Komba alipokuwa madarakani aliboost kidogo watu Wa kata ya Lituhi wakapata Unafuu Wa mawasiliano ya simu. Ilijengwa minara kama mitatu haraka. 

Miaka ya karibuni nimeshangaa kampuni ya Tigo kwenda kujenga minara mitatu katika eneo ambalo liko ndani ya km 10 wakati kijiografia ya Nyasa hata minara miwili ingefaa na kuongeza km zingine 10 na kupata km 20 zenye minara mitatu kutokana na jiografia ya Nyasa kuwa ya milima hivyo kusingekuwa na shida yoyote katika nguvu za mvutano kutoka mnara moja hadi mwingine. 

Mwaka wa tatu mnara wa Halotel uliojengwa mlima "Lilengalenga" kijiji cha Lundu haufunguliwi na kuwasaidia wakazi wa maeneo ya jirani kuwasiliana. Sasa walijenga wa nini si wangeacha tu.. Kila siku sarakasi ambazo hazina majibu stahiki kwa wahusika. 

Hakuna watu wana shida ya mawasiliano kama kata ya Mbaha, Ngumbo na Liwundi. Sio kama tumeridhika ila iko siku mkija na shangingi zenu mtapigwa mawe sana kwasababu ya utapeli ambao wanasiasa mnaufanya. Na haya maeneo yana madiwani walewale ambao sifa yao Kuu ni KKK. Sasa unafikiri watamwanbia nini mkurugenzi.

Mwaka juzi niliwahi kusema mimi sifurahii mbunge wa jumbo letu kuwa waziri na hata kesho ukiniuliza kwanini nitakupa sababu ninazo amini. Wengi mlimpa sana pongezi Stella Manyanya lakini hamkujua kazi kubwa anayotakiwa kuifanya ni ipi.

Ndo maana hadi leo bi mkubwa tangu achaguliwe hajawahi pita vijiji vyote na kuongea na wanachi wake. Matokeo yake mnatimuliwa vumbi tu huku ndugu zangu wakipunga mikono. Hapo ujue anaenda kwenye Tamasha la Utalii.
Naunga juhudi za utalii kwa Nyasa lakini kuna mahali ubongo wa wengi akiwemo Manyanya ume- stack kama kompyuta. Utawezaje kutangaza vivutio vya utalii wakati huko unakokutangaza hakuna barabara ya uhakika ili watalii wakafika na kuongeza pato kwa kuwekeza?

Barabara mbovu sasa huyo mtalii atakujaje. Atatumia usafiri gani ili afike. Kucheza ngoma na kula nyama sio mwisho Wa kuutangaza utalii tunaoutaka lazima tuumie na kuumia kwenyewe ni kuhakikisha miundombinu iko Sawa.
Wakati watanzania wakiwashangaa wasukuna wa Bariadi kwa kumchagua Chenge itabidi muwaulize ni kipi anachowafanyia wale hadi waendelee kumuweka madarakani.

Achana na harakati za kuikomboa Nyasa ila kiukweli mko wengi mlioko mjini na mmesusa kwenda kusaidia hata kwa mawazo juu ya nini kifanyike kwa wanyasa wenzenu.

Kwa macho yangu nimeshuhudia watu wanafikia alikoolewa Dada yao na kwao hakuna mji kwasababu tangu wazazi wafariki basi watu wamekacha hata kwenda kwao. 

Sasa ukienda ndo unafikia kwa shemeji yako. Wako wanaofikiri ni ujanja kupotela kwa watu na kukaa miaka mingi mikoa ya watu bila kwenda Nyumbani.

Nilisafiri na Mzee mmoja ambaye aliniambia aliondoka Mbinga akiwa na miaka 30 na kakaa Tanga miaka 30. Tukiwa kwenye gari sikutaka kumvumilia nikamwambia huo sio ujanja Mzee ni ushamba kwasababu unajionyesha wewe ni mtumwa wa fikra. Huwezi jisifia kwa waelewa kuwa sijaenda nyumbani miaka 30. 

Sasa wako waliokuwa kama huyu Mzee na wanajitambulisha ni Wanyasa na hujifanya wanatoa maelezo mengi kuhusu Nyasa ya zama zao. Kutokana na kawaida yetu ya kuwaona walioko mjini ni miungu watu ndo maana wanyasa wakichinjiwa Mnyama tu tayari wanakuona kama mfalme wao. 

Elimu ya kujitambua ndugu zako huwezi itolea kwa mikusanyiko ya Lamada au msimbazi bali nenda kwa wanyasa kulekule kaongee nao..

Binafsi nimepanga kama mbungu atanipa uhai kuanza na darasa la kujitambua kwa wanyasa pamona na elimu ya uraia kwa kata ya Mbaha. Ndani yake nitakuwa na elimu ya kufuata fursa kwa kujiinua wenyewe katika familia zao.
Yawezekana hakuna niliyewahi kumwambia lakini najua nafasi ya kuongea na Ndugu zangu Wa Mbaha nitapa haya mambo yakuuza utu kwa vimboma vya nyama vinatuonyeaha jinsi gani hatuna elimu ya utambuzi katika masuala ya msingi kwenye maendeleo.

Mungu endelea kunipa uhai ili yale ninsyoyafikiria kwa jamii yangu yaweze kutimia. Nimechoshwa na wanasiasa kwabkiasi kikubwa sana kwasababu wanawadanganya sana bibi zangu babu zangu kaka zangu na wengine.
Kama kuna mtu nitakuwa nimemkwaza we umia tuu kwasababu sina mpango Wa kumwomba mtu msamaha kwa haya.

Acheni ulimbukeni hizo kanda zilizoendelea hazikufikia hivyo bila watu kupeleka maendeleo kwao. Halafu ubataka Nyasa ifanane na uchagani wakati we kwenu huendi unasema kuna wachawi huu ni ushamba. Tunaoenda hawatuoni?

Keneth Kondowe Lihambanda's sauti unayopaza sasa inafaida kesho. Chiggs endelea hivyo hivyo yawezekana ndoto ya kuwa Robin Hood ikatimia kwako.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako