MIAKA
mingi enzi za babu zetu kulikuwa na ngoma maarufu iliyoitwa GEUZA. Hakukuwa na
Ligambusa kama ilivyo sasa walisafiri kutoka Lundu kwenda Mbaha au Hinga
kucheza Geuza usiku nyakati za Mbalamwezi na wakarudi nyumbani.
Kwa
upande wa Ngoma ya Mganda, Maboma yaliyoka hadi sasa ni Mawili na yenye
upinzani wa Kama vilabu vya soka. LICHUMA LINDU na LIHEGHELYA KONI majina hayo
ni kama yanajibizana .Ni ngumu kuona mshiriki wa boma moja kwenda boma lingine
nyakati za mazoezi utafukuzwa na kuonekana kama umeenda kuiba stepu(mtindo Wa
uchezaji).
Kihoda
ndo kimetia fola nyakati za nyuma Lundu ilikuwa na maboma mawili tu yaani Maji
na Uamuzi. Lakini kutokana na ongezeko la watu kikafanya kuonekana wanawake
wako wengi na wote wanataka kuonyesha uwezo wao wa kusakata ngoma.
Ndipo
maboma mengine yakazaliwa. Boma Maji limafanikiwa kuzaa boma linaloitwa Upendo
ambao wao wanchezea pale nyumbani kwa Mzee Matamelu. Huku wenyewe Maji wakiwa
pale nyumbani kwa Mzee Nduru Cosmas au kwa Lipambeka (maeneo ya Kunkwachu).
Pia
kuna boma ambalo limezaliwa kwa kuwamega wachezaji toka Maji na Uamuzi ambalo
linaitwa Kisiwani ambalo wanachezea kwa Mzee Lendela. Lilianzishwa mwakajana na
wakaita kihoda. Linajumuisha watu wote Wa mlimanani na kitongoji cha maliwa..
Boma
uamuzi amemzaa boma Amani lililopo Kitongoji cha Likwambe na wengine walipunda
boma la kisiwani. Hivyo maboma ya kihoda yapo 5 hadi sasa.
Ligambusa
na kindeku zinakuwa bado ngoma za kwenye sherehe kama ilivyokawaida yake. Ila
wameongeza matumizi ya ligambusa hadi katika mkesha Wa mwaka mpya lazima
lipigwe ili watu waburudike.
©HONORIUS
MPANGALA
No comments:
Post a Comment
Maoni yako