Na KIZITO MPANGALA
Kila mmoja anatamani kuendeleza
siri kubwa ya taarifa zake katika simu yake au tarakilishi (kompyuta) yake ili
zisijulikane na wengine. Ulizni wa taarifa hizo husaidiwa na nywila (password).
Nywila (password) inaweza kuwa ya haerufu tupu, namba tupu au mchanganyiko wa
herufi pamoja na namba na baadhi ya alama za uandishi kama vile mkwaju (/) na
kadhalika. Nywila ina umuhimu mkubwa katika ulimwengu huu wa Sayansi na
Teknolojia ingawa ilianza kutumika zamani ila siyo kwa kiwango kikubwa kama
ilivyo sasa.
Kabla ya kuboreshwa kwa
teknolojia ya mawasiliano, zamani password ilijulikana kama “passphrases.”
Kwa hiyo nywila ni ufunguo unaolinda lango la kuingilia katika kuzijua taarifa
zako ili zisivamiwe na wengine (hackers). Hii ni kwa ajili ya usalama wa
mawasiliano yako. Kila mmoja duniani ambaye anatumia tovuti au kurasa
mbalimbali hukutana na kipengele cha kuingiza password ili apate
anachokihitaji. Malengo ya nywila (password) ni:
1. Kukupa
ruhusa ya kuingia kwenye akaunti husika unayaotembelea,iwe ya kwako au ya mtu
mwingine au kikundi au kampuni.
2. Kuipa
ruhusa barua pepe ifunguke ili kuona taarifa zilizomo. Baruapepe inaweza kuwa
ya kwako au ya mtu mwingine kadiri ya maelewano kati yenu.
3. Kulinda
vifaa vya kielektroniki ili visitumiwe na wengine ikiwa mmiliki hapendi
vitumiwe na wengine. Vifaa hivyo ni kama vile simu, tarakilishi (kompyuta),
tarakilishi mpakato (laptop), ubamba (tablets) na kadhalika.
4. Kupata
mtandao (network) ikiwa itahitajika kutumia password.
5. Kulinda
tovuti ili isiingiliwe na wengine (hackers)
6. Ulinzi
wa data binafsi, za kikundi au za kampuni fulani.
Tarakilishi (kompyuta)
nyingi zinaonyesha alama ya nyota (*) au nukta (.) unapoandika password
yako, lakini hasara mojawapo ya kuonyesha alama hizo ni kwamba huoni herufi za
nywila yako na hivyo hata ukikosea huwezi kung’amua mapema, hivyo utakuwa
unarudia mara kadhaa kutokana na kukosea. Hii hupelekea wengi kuunda password
dhaifu ili waikumbuke haraka na kwa urahisi. Katika hilo, kwa mfano mtu mwenye nywila
(password) kama hii,PKDSC56523/TDSCX&&$$2lvEhpi$KnVn901C4Y23zsVZK1/UILbTkKIU6hA6V/
opXZ3yQUEhVxQS6/KjaO2bH7VZOOr/DTGko9LjqWOi7CrU:Ggy0:15569:0:99999:7wakati fulani
atashawishika kuibadili na kuunda nyingine ambayo ni dhaifu na inaweza kuotewa
na wadukuzi (hackers) kwa sababu anapoiandika inaonyesha alama ya nyota au
nukta tu. Kompyuta nyingi zimeundwa kwa mfumo ambao:
1. Hauruhusu
kuonyesha nywila (password) kwenye kioo bapa (screen) lakini unapoandika
password yako yenyewe inang’amua na kama umekosea inakutaarifu. Zinaruhusu
alama ya nyota (*) au ya nukta (.) tu.
2. Unaruhusu
password yenye urefu maalumu. Yaani unapounda password unaambiwa iwe na herufi
ngapi. Nyingi huruhusu mwisho herufi 8 au mchanganyiko wa herufi na alama,
jumla ziwe 8.
3. Unaruhusu
uunde password yenye mchanganyiko wa herufi kubwa na ndogo.
Vilevile kuna sera ya nywila
ambayo ina lengo la kuhakikisha kwamba password zenye nguvu, yaani zile ambazo
siyo dhaifu, zinatumika ipasavyo bila kuingiliwa au kuvamiwa na wadukuzi
(hackers). Sera hii mara nyingi hutumika katika taasisi au kampunu mbalimbalio
ambazo kwao mtandao ni wa lazima katika utendaji wa shughuli zao za kila siku
kulingana na maudhui ya kampuni au taasisi husika. Lengo kuu ni kuilinda
tarakilishi (kompyuta) na taarifa zao zoet zilizomo. Hivyo, uhitaji wa nywila
una uangalizi mkubwa kuliko kawaida iliyozoeleka na wengi kama vile nywila za
kuingilia facebook au instagram na mitandao mingine ya kijamii.
Sera bora ya nywila ni ili
inayompa nafasi mtumiaji kuunda password bora ambayo haitakuwa rahisi
kukaririwa na mtu mwingine na pia haitakiwi mfumo wa kompyuta umlazimishe
mtumiaji atumie nywila ya kuundiwa kutoka kwenye mfumo kwa sababu itakuwa
rahisi kudukuliwa. Kutengeneza nywila imara kulingana na sera ya password ni
kazi inayohitaji umakini kwa kuwa mara nyingi makosa mdogo madogo yanajitokeza
na husababishwa na binadamu mwenyewe.
Baadhi ya wataalamu wa usalama
wa kimitandao hupendekeza kuwa kuundwe nywila nyingi na zihifadhiwe kwenye
kompyuta au simu ili mtumiaji akihitaji nywila achague kutoka katika orodha
hiyo. Hii kwa nadharia ni wazo zuri sana, lakini kwa vitendo (practical) siyo
pendekezo rafiki kwa watumiaji wa password kwa sababu kuna uwezekano wa
password moja kutumiwa na watu zaidi ya mmoja na pia zipo nywila tata (complex
password) ambazo zitahitaji muongozo kutoka kwa kiongozi wa mfumo (system
administrator). Kuchagua password nzuri kunahitaji umakini na kuelimishwa.
Pendekezo hili huchangia wtu engi kusahau nywila zao wanapoingia katika akaunti
zao na vilevile hata wenye nywila rahisi (simple password) wanwa uwezekano wa
kusahau kama hawatazitumia mara kwa mara. Inashauriwa pia kubadili nywila
(password) yako pengine kila baada ya miezi sita au mitatu ili kumzubaisha
mdukuzi na kwa usalama wa taarifa zako.
Sera ya nywila (password)
inaweza kutofautiana kati ya kampuni moja na nyingine lakini iliyo ya jumla na
ambayo ni bora ni ile inayompa ruhusa mtumiaji kuunda nywila imara kulingana na
mahitaji ya kampuni au taasisi husika kama nilivyosema hapo awali. Nywila hiyo
inatakiwa kuwa na lengo, mlengwa (mtumiaji) na pia sera itoe ruhusa kwa
mtumiaji kuunda nywila nyingine ikiwa ile ya awali imesahauliwa au imepotea, na
pia kuhakikisha kwamba nywila (password0 haipewi muda wa mwisho wa kutumika.
Muda wa mwisho wa kutumika kwa nywila ni pale mtumiaji anapoamua kuibadilisha
na kuunda nyingine.
Kufanikisha katika matumizi ya
nywila (password), sera zake ziwe na programu maalimu kwa ajili ya kuwaelimisha
watumiaji au wale ambao bado hawana nywila. Kuchagua nywila na kuwaelimisha
wale wanaopata changamoto mbalimbali za nywila (password) zao na wale
walioshindwa kufuata sera za nywila, yaani wale wenye nywila dhaifu. Vilevile
kuwapa motisha wenye nywila imara na kupunguza uwezekano wa kubadilishwa kwa
nywila ni sera ambazo ni muhimu katika teknolojia kwa sasa. Pia, kuwachochea
watumiaji wabadili nywila zao mara kwa mara kunaweza kusababisha changamoto ya
kuunda nywila mpya ambazo ni dhaifu, ingawa vitendo vya kubadili nywila
(password) havikwepeki.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako