Na Markus Mpangala
Mwaka 1986 Diego Maradona alifunga bao la mkono, lakini
mwamuzi hakuona akakubali kuwa ni bao halali. Waingereza
walilalamikia hilo, lakini mwamuzi alishapitisha uamuzi wake ni bao halali.
Tangu hapo Maradona amekuwa akisema bao lake hilo ni la ‘mkono wa
mungu’. Mwaka 1966, kiungo wa England, Geoff Hurst apiga shuti kali
likagonga mtambaa panya na kugonga chini kisha kurudi uwanjani.
Diego Maradona |
Lakini wakati mwamuzi wa mchezo hajaamuru chochote wachezaji
wa England wakaungana na kiungo huyo kushangilia na mwamuzi
akakubali ni bao halali. Lakini mpira ule ulipogonga mtambaa panya kisha kugonga
chini wala haukugusa mstari. Geoff Hurst akaingia kwenye rekodi ya
dunia kwa
kufunga mabao matatu katika mechi ya fainali. Rekodi hiyo imefikiwa na kinda wa Brazil, Oscar Dos Santos
ambaye alifunga mabao matatu wakati wa mechi ya fainali ya kombe la
dunia kwa vijana chini ya miaka 20 dhidi ya Ureno.
Lakini miaka 44 baadaye yaani mwaka 2010 katika michuano ya
kombe la dunia nchini Afrika Kusini, ni England iliyonyimwa bao.
Frank Lampard alifumua shuti kali likagonga mtambaa panya
kisha litua ndani ya lango huku kwa kasi ya ajabu golikipa wa Ujerumani,
Manuel Neuer alidaka kiustadi mkubwa.
Mbwana Samatta, akikabiliana na beki wa Zamaleki ya Misri |
Mwamuzi wa pambano hilo alikataa kuwapa bao England.
Waingereza walichachamaa baada ya michuano hiyo huku wakikumbuka kipigo
cha mabao 4-1 walichopata kutoka kwa Ujerumani.
Waingereza wakasahau kuwa wao walitwaa kombe la dunia
kupitia bao lenye utata, kwani walifanikiwa kuifunga Ujerumani ya akina
Franz Backenbauer na
Gerd Muller. Lakini ilipotokea kwao kunyimwa bao wakapayuka dunia nzima.
Na sasa majadiliano ya kutumia Teknolojia ya goli yakachukua mkondo
wake.Teknolojia hiyo maarufu kwa jina ka Jicho la Kipanga (Hawk
Eye) ilipenyezwa katika korido la FIFA ili ipate uungwaji mkono.
Nadhani teknolojia hiyo ilipaswa pia kutumika kutambua mpira
wa kichwa uliopigwa na mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, John Bocco
dhidi ya Burundi kwenye michuano ya CECAFA inayoendelea nchini
Uganda. Tukiacha hilo, ni wazi sasa teknolojia ya goli (Hawk Eye)
itakuwa njia mbadala huku tukikumbuka shirikisho la soka la Ulaya
linatumia waamuzi watano katika pambano moja.
Waamuzi wawili wanakaa nyuma ya goli, yaani mmoja mmoja kila
upande. Hivyo ukiongeza na mwamuzi wa akiba wanakuwa watano. Naam, Jicho la Kipanga(Hawk Eye) imeshakubalika na
kuthibitishwa na FIFA. Kwahiyo, FIFA imesaini Mkataba Matumizi ya Teknolojia ya kutambua goli (Hawk Eye). Teknolojia hiyo itafanyiwa majaribio nchini Japan, ambapo
baadaye itajaribiwa kwenye michuano ya klabu bingwa dunia
itakayofanyika nchini humo.
Dhumuni la teknolojia hii ni kutoa msaada kwa waamuzi ili
kuamua kama Mpira umevuka mstari wa Goli na hivyo kuwa Goli halali. FIFA imepiga hatua mbele baada ya kusaini Mikataba na
Kampuni mbili za Waundaji wa Mitambo itakayotumika ya kutambua goli. Mitambo
hiyo inajulikana kwa jina la GLT (Goal Line Technology).
Kampuni za zilizoshinda tenda hiyo ni Hawk-Eye Innovations
na Fraunhofer ISS (GoalRef), ambapo mitambo yake itatumika
kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani huko Japan
kuanzia Desemba 6 hadi 16 mwaka jana.
Franz Beckenbauer |
Katika hali hiyo wengi wanaweza kusema ni suala zuri kwa
maendeleo ya mpira wa miguu. Lakini vilevile tunapaswa kuwaangalia
waamuzi na mamlaka yao katika mechi na soka kwa ujumla. Kwa hali halisi kwanza teknolojia hiyo itaondoa kabisa
malalamiko ya mabao ambayo yanakataliwa na waamuzi. Lakini vilevile
itasaidia waamuzi kuwa na nafasi bora kuondoa malalamiko yoyote ambayo yatachangiwa na uamuzi wao.
Tekonoliia hiyo inatumika pia katika mchezo wa Tennis ambapo
humsaidia mwamuzi kuangalia mpira kama umegusa mstari au umeangukia
nje ya mstari au ndani ya uwanja. Teknolojia hiyo inasaidia sana waamuzi wa Tennis kuamua
pointi halali kwenye kutafuta Seti. Tumeona hayo kwenye michuano mingi
kama US Open, Wimbledon, Ausralia Open, Beijing Open, Olimpiki, na
michuano kemkem
inayosimamiwa na shirikisho la Tennis. Hata hivyo kwa suala hili bado naona tunawahitaji sana
waamuzi ambao wanaweza kutuletea matokeo mazuri dimbani. Licha ya kuletewa teknolojia hii bado tunahitaji kuwaamini
waamuzi ingawaje kuna nyakati wanakera. Pia teknoloajia hii inaamua
magoli tu, lakini haitoi nafasi kwa rafu mbaya au mchezo mbaya wa
mchezaji fulani ambao mwamuzi anashindwa kuona.
Mathalani Mwinyi Kazimoto, David Beckham, Dickson Daudi, na
wengineo wamekuwa waathirika wa ukosefu wa teknolojia ambayo ingeweza
kusaidia namna bora ya kubaini uchezaji mbaya kwa baadhi ya
wachezaji.
Madhara ya teknolojia hii ni kuongezeka kwa malalamiko
mengine ya uamuzi wa waamuzi. Hali ambayo itawapotezea uwezo wao wawapo
dimbani. Ni hatua nzuri kwa Hawk Eye lakini ni wakati mzuri pia
kuchambua makosa mengine dimbani yanayostahili kutegemea kamera ili
kuepusha madhara kwa wachezaji.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako