Nakiri moja ya upumbavu mkubwa ni Barrack Obama kuwa
kikaragosi kwake na serikali. Mwanzoni kupitia Hilary Clinton walisema wakenya
wasichague watuhumiwa wa ICC yaani Kenyatta na Ruto. Baadaye akaja Barrack Obama akasema atawaunga mkono wakenya
katika chaguo lao. UNAFIKI, na nilishawaambia watu Barrack Obama sio mwafrika
kwa vile tunavyotaka kumtafsiri kama akina Jesse Owen, Jesse Jackson ambao ni
zao la utumwa.
Obama hakuachagua lakini yeye sio zao la utumwa bali mapenzi
tu wa binti na mvulana. hajui madhira ya akina jese jackson. kwa suala la kenya
Raila Odinga nampenda harakati zake lakini bado naguswa na UZEMBE aliofanya na
kudhani atashinda kirahisi. Nimeandika hili, inshallah itachapishwa wiki ijayo
jumanne(TAZAMA). Odinga amejitakia sana, kwa njia zake alizopita tangu 2002,
2007 na 2013 sishangai kushindwa kwake.
Hata wengi walipomshinikiza Jaji Willy mutunga katika kesi
ya Uhuru kenyatta na Ruto kutogombea, jaji mutunga alisema wanaopinga hawana
hoja. Kimsingi Odinga alikuwa na timu dhaifu mno, wala hata
CHADEMA sijui kupeleka nini au nini sijui bado Odinga alikuwa na timu dhaifu
sana kuliko ile ya mwaka 2007 iliyojaa wababe wa siasa na wenye ushawishi. Hivi
nani pale alikuwa na msaada kwa Odinga mwaka huu?
Sioni hata mmoja. Kwahiyo kuwalazimisha wakenya wamchague
Odinga ni ukosefu wa heshima tu. wakenya sio wajinga, na wanaolalamika ni watu
wa Kisumu tu. Ujinga aliofanya Odinga ahata akiongea na mimi nitamwambia
ulifanya makosa haya na haya. kwahiyo CHADEMA kumsaidia Odinga ni kawaida na
tunawaheshimu kwa hilo, lakini uamuzi wa mwisho ulikuwa mikoni mwa wakenya.
Sio Obama ambaye sio raia wa kenya. ....... sio mpiga kura
wa kenya. kama alitaka Odinga ashinde alipaswa kuwa na adabu sasa. Marekani
kutomtaja sio issue kabisa, haitabadilisha kitu, ni ujuha tu. wala Marekani
ikitaja jina la kenyatta haina maana ndio inahalalisha. Marekani sio wakenya.
Hayo mataifa yaliyowapongeza WAKENYA, na WAKENYA wamemchagua
nani? Je, kupingwa matokeo mahakamani kunazuia kupongezwa kwa Uhuru Kenyatta
ambaye ametangazwa na TUME? ....
na kama Raila Odinga akishinda hiyo kesi, kuna sheria
inayozuia kutompongeza Raila Odinga? mimi nadhani USA kutotaja jina la kenyatta
ni woga na udhaifu kiakili, sababu ilibidi hata pongezi wasitoe wasubiri hatima
ya majibu ya mahakama. ... vilevile, mataifa ya magharibi kutotaja jina
kenyatta au kutompongeza bado hakumanishi wao wana uhalali wa kuwamrisha
wakenya wamchague nani. .....kwa upande mwingine kisiasa Odinga amejitakia
ANGUKO.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako