Na Kizito Mpangala
Alizaliwa tarehe 10 Novemba
mwaka 1919 nchini Urusi. Alikuwa ni mtoto wa wazazi Timofey Aleksandrovich
Kalashinkov (baba) na Aleksandra Frolovna Kalashinkova (mama) akiwa ni mtoto wa
17 kati ya watoto 19 katika familia waliozaliwa katika familia hiyo ya wakulima.
Baba yake aliweza kusoma na kuandika lakini mama yake katika maisha yake yote
hakuweza kusoma wala kuandika. Jenerali Mikhail Kalashinkov alikuwa ni mhandisi
wa jeshi la Urusi hasa katika masuala ya silaha ambapo aliiboresha bunduki aina
ya AK-47 na kuwa AKM, AK-74, PK Machine Gun, na LMG (Light Machine Gun).
Alinusurika kifo baada ya kugua
mara kwa mara alipokuwa mdogo. Alivutiwa na aina mbalimbali za mashine lakini
pia alikuwa mtaalamu wa kuandika mashairi akiwa na tumaini la kuwa mshairi
mahiri katika fasihi ya Urusi. Aliendelea na morali hiyo na kuweza kuandika
vitabu sita na kuendelea kuandika
mashairi muda wote wa maisha yake.
Alipokuwa akiishi na wazazi
wake katika kijiji cha Kurya nchini Urusi alijishughulisha na uwindaji pamoja
na kilimo, hiyvo alikuwa akiitumia mara kwa mara bunduki ya baba yake katika
shughuli hiyo ya uwindaji ili kupata kitoweo. Hakupata elimu katika chuo
chochote lakini alijifunza umakenika. Shughuli ya kuwinda aliendelea nayo mpaka
alipotimiza miaka 90 mwaka 2009.
Alichukuliwa na jeshi na
kufundishwa shughuli za umakanika baadae akawa askari kamili huku akiendelea na
uundaji wa silaha ndogo ndogo. Mwaka 1941 aliumizwa vibaya katika moja ya
pambano aliloshiriki hivyo akalazimika kulazwa katika hospitalai ya jeshi la
Urusi tangu mwezi Oktoba 1941 hadi mwezi April 1942, ni zaidi ya miezi minne.
Alipokuwa wodini askari wenzake
walikuwa wakija kumjulia hali na katika mazunguzmo aliwasikia baadhi wakilaumu
silaha duni za jeshi lao. Yeye hakutia kauli yoyote katika jambo hilo katika
mazungumzo yale lakini alilitunza kichwani lalamiko lao na baada ya kupata
ahueni akaanza kazi ya kubuni bunduki mpya ambayo itataondoa kero ya askari
wenzake waliokuwa wakilalamika, ndipo alipoanza na Ak-47.
Bunduki aina ya AK - 47 |
Mwaka 1947 aliunda silaha
ambayo mwanzo aliipa jina la MIKHTIM ambalo lilitokana na herufi tatu za mwanzo
za jina lake na herufi mbili za mwazno za jina la baba yake yaani MIKHail
TIMofeyevich, lakini baadae ikapewa jina rasmi ambalo ni AUTOMAT KALASHNIKOVA MODEL
1947 hapo ndipo ikafupishwa na kuitwa AK – 47 na ikaanza kutumika huko Urusi
lakini baadae ziliundwa nyingi na kuuzwa nchi zingine.
Mwaka 1949 aliunda bunduki
nyingine ambayo ilipewa jina la ufupisho AKM (AßTOMaT KaлáШHиKOßa MoдepHизиpoßaHHbIŇ). Baada ya
kuafanikisha utengenezaji wa AKM aliweka wazo jipya la kutengeneza bunduki
nyingine ambayo ni ya gaharama ya chini. Alifanikisha zoezi hilo na kuipa jina
la RPK likiwa ni kifupi cha maneno “Russian
PyЧHOŇ пyлeMeT KaπáШHиKOßa” ambayo kwa sasa ni jina
maarufu ni LMG yaani Light Machine Gun.
Aliunda silaha nyingine nyingi kwa manufaa ya jeshi la nchi yake ingawa baada
ya kuwaongezea utaalamu wenzake, waliunda silaha nyingi zaidi na kuziuza kwa
mataifa mengine.
Sifa kuu anuai kwa silaha zote
alizounda ni urahisi wa jinsi ya kuunda, na ubora wake wa kufanya kazi katika
hali yoyote ya pamabano, iwe kiangazi, mazika, kipupwe na kadhalika, zinafanya
kazi kwa uhakika.
Kalashikov mwenyewe alisema
kwamba juhudi zote hizo ni kwa manufaa ya nchi yake katika suala la ulinzi na
usalam lakini siyo kwaajili ya kufanya biashara ya silaha kama ilivyokuwa
imezoeleka miaka kadhaa baada ya kuwazoesha utaalamu askari wenzake ambapo
walitengeneza silaha nyingi zaidi na kuziuza kwa matifa mengine. Hii ni
kutokana na utaalamu wake ma uzoezfu wake.
Alimiliki asilimia 30 ya
kampuni aliyoianzisha huko Ujerumani ambayo aliiacha chini ya usimamizi wa
mjukuu wake bwana Igor Kalashinkov. Kampuni hiyo ina lebo ya neno VODKA, ambayo
hujishughulisha na utengenezaji wa pombe aina ya Vodka, visu vyenye lebo ya
Vodka, na miamvuli yenye lebo hiyo pia. Pombe ya Vodka unaypiona sasa ndiyo inatoka
kwenye kampuni yake.
Luteni Jenerali Mikhail Kalashinkov enzi za uhai wake |
Rais wa Urusi Mh. Vladmir Putin akiwa na maafisa wa jeshi walipokuwa wakizindua toleo jipya la AK - 47. |
Bunduki aina ya AK – 47 imekuwa
katika matumizi rasmi katika zaidi ya mataifa 55 duniani kama sehemu ya michoro
ya bendera zao kama vile Msumbiji, Zimbabwe, pia na baadhi ya vikundi kama vile
kikundi cha wanamgambo cha Hezbollah. Katika
maisha yake yote ametunukiwa nishani mbalimbali ambazo kwa ujumla zote ni 53. Alikuwa
mwanajeshi wa kutumainiwa nchini Urusi katika masuala ya utengenezaji wa
silaha. Hii ni kutokana na morali yake alipoona kuwa askari watatu au wane wanatumia
silaha moja kwa kupokezana.
Baadhi ya matamko yake katika maisha yake ya kijeshi ambapo
aliamini kuwa Mungu ndiye msimamizi wa kipawa chake cha ufundi, aliwahi kesema
“Walaumuni Wanazi wa Adolf Hitler kwa kuwa
wamenichochea niunde silaha nyingi zaidi. Mimi nilitaka kutengena mashine za
kilimo lakini Wanazi wamenigeuzia kibao”
“Nilipokuwa mdogo nilisoma mahali
pameandikwa kuwa Mungu anasema chochote ambacho lina utata achana nacho ila
kilichorahisi kwako basi kiendee, basi mimi kicho rahisi ni ufundi wa silaha
ili kulinda nchi ya mababu zangu”
“Nina furaha sana kwa ugunduzi na ubunifu
wangu katika silaha kwa lengo la kuilinda Urusi, lakini ninasikitika sana kwa
kuwa zinatumika kigaidi. Nilipenda kuunda mashine za kilimo ziwasaidie wakulima”
“nilitengeneza silaha kwaajili ya ulinzi wa
nchi yangu, kwa hiyo, siyo kosa langu jinsi inavyotumika mahali ambapo
hapastahili. Wanasiasa ndio walaumiwe kwa hili”
Kalashinkov
alimwandikia barua padre wa kanisa alilokuwa akisali. Barua hiyo aliiandika
miezi sita kabla ya kifo chake mwaka Disemaba, 2013. Barua hiyo iliruhusiwa
kuchapishwa magazetini, na aya mohawapo aliandika hivi
“Ninaumwa maumivu ya kiroho. Ninapaswa kuwajibishwa
kutokana na uvumbuzi wangu wa silaha kwa kuwa vifo ni vingi mno
vinavyosababishwa na silaha zangu ingawa sikuwa na matarajio hayo”
Alisifiwa
sana kwa uzalendo wake katika taifa lake la Urusi mapaka kifo kilipomkuta mnamo
mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 94.
© KizitoMpangala
0692
555 874
No comments:
Post a Comment
Maoni yako