NA MWANDISHI WETU
WIZARA zimeongezeka kutoka 19 hadi 21, Mawaziri kutoka 19 hadi 21, Manaibu Waziri kutoka 16 hadi 21. Wataapishwa ni Jumatatu tarehe 9/10/2017 asubuhi kwenye saa tatu au saa tatu na nusu.
Rais Magufuli: Pia tumeongeza Mawaziri 2 na Manaibu Waziri 5
Rais Magufuli: Waziri wa Mazingira amebaki kuwa January Makamba, Naibu atakuwa Mh. Kangi Lugola.
Rais Magufuli: Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi tumeigawa na kuwa Wizara 2 za Wizara ya Kilimo na
Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Selemani Jaffo amepandishwa na kuwa Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, kabla alikuwa Naibu kwenye Wizara hiyo. Mbunge George Mkuchika ameteuliwa kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora.
Rais Magufuli: Mbunge Luhaga Mpina ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Abdallah Ulega ameteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo. Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kuwa chini ya Waiziri Dr Philip Mpango na Naibu Waziri Dr Ashatu Kijaji
Wizara ya Kilimo Waziri ni Charles John Tzeba, na Naibu Waziri ni Marry Mwanjelwa. Wizara ya Habari utamaduni wasanii na Michezo, Waziri ni Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri ni Juliana Shonza
Wizara ya Madini, Waziri ni Angela Kairuki na Naibu Waziri Harun S Nyongo. Wizara ya Nishati, Waziri atakuwa Medadi Kalemani, Naibu Waziri atakuwa Subira Hamisi.
Katibu wa bunge atakuwa Steven Kagaigai na Dkt. Thomas Kashilila atapangiwa kazi nyingine.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako