Mfalme Ramon Berenguer wa IV wa Barcelona alimuoa Malkia
Petronilla kutoka ufalme wa Aragon. Ndoa hiyo ilichochea muungano kati ya
ufalme wa Aragon na Catalonia(Barcelona).
Mwaka 1469 ulishuhudia ndoa nyingine ya kifalme. Ilikuwa
ndoa kati ya Mfalme Ferdinand wa II (Antequera) wa ufalme wa Aragon na Malkia
Isabella wa I wa Castila (Madrid). Ndoa hiyo ilichochea muungano Castila na
Aragon.
Baada ya ndoa hiyo ndipo nguvu ya mamlaka na siasa ilihama
kutoka Aragon kwenda Castila (ambako iko serikali kuu kwa sasa yaani jijini
Madrid). Kuanzia hapo serikali kuu ilitoka Madrid, na Catalonia kuwa na
serikali ya jimbo.
Tayari tumeona ufalme wa Aragon umeungana na Catalonia (Barcelona),
kisha Castila (Madrid) ikaungana na Aragon. Maana yake falme zote nne ziliunda
nchi moja. Hispania. Baadaye ikaongezeka Sevilla, Granada na kadhalika.
Hakika lilikuwa la taifa. Lakini sasa WANATAKA KUACHANA.
Malkia Isabella wa I |
No comments:
Post a Comment
Maoni yako