November 22, 2017

MAONI YA MHARIRI: ‘Nani atalinda samaki wa Ziwa Nyasa?


Naanza katika maliasili zetu. Sisi kama Tanzania tuna maliasili nyingi sana na watu wengi hawajui kabisa hilo na pia tuna wataalamu wangeweza kuwafumbua watu macho. Tukianza kwa kusafirisha nje ya nchi, Samaki hai wa maji baridi yaani Tanzania ndio ina samaki wa bei kubwa kuliko wote duniani. 
Samaki wa mapambo wanapatikana zaidi Ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika. Samaki mmoja anafika dola 19 na kuendelea. Ukifua katika mtandao huu hapa uone www. liveaquaria.Com.or Google African cichlids. Hao ni Samaki tu, na kumbuka hawa samaki tunasafirisha baada ya miaka kidogo watazalisha hawata nunua tena kwetu Ziwa Nyasa hivyo bei nayo itashuka sana.


Hilo limefanyika hata kwenye wadudu tulisafirisha moja kwa moja na sasa wameshuka bei. Samaki wa mapambo unaowaona mitaani hapo Bongo wanao toka Malaysia na kwingineko wote wamehasiwa huwezi kuwazalisha akifa ununue mwingine.

Wenzetu wanajua kudhibiti soko hapo ndio suala la wataalamu wetu linapoingia kati. Wadudu wa Tanzania walikuwa wakiuzwa bei sana katika soko la nje mdudu mmoja alikuwa ni dolla hadi 400, mdudu 1 sasa ni dola 20. Yote hayo unaweza kuyapata kwenye mtandao Goliathus orientalis.

Utaona wataalamu wetu au serikali imeshindwa kudhibiti na kutoa fursa kwa wananchi kujua ni kitu gani kinaweza kuingiza pato la kigeni. Mwisho kabisa kuna wadudu wanatoka Dodoma wanapatikana wakati wa ukame serikali kwa kutokujua haijabaini fura hiyo.

Badalka ya kuitumia kama fursa ya pesa, yenyewe imepiga marufuku kuwasafirisha tena hao ni wale waliokufa wala sio wazima, bei hizo ni wadudu wakavu tu. Tutunze mazingira na mazingira yatutunze sisi. Kuwe na ushirikiano kati ya watu na wataalamu wanao jua haya mambo. Nawajua watu wengi sana walioipatia serikali pesa za kigeni kwa kupitia biashara halali kabisa lakini serikali kwa kutokujua mambo wanakuja na matamko ambayo yana wafanya wakose mapato.
Taumke!

Markus Mpangala
Novemba 22/2017.
Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

Maoni yako