September 22, 2017

MV. NJOMBE YATIA NANGA MBAMBA BAY LEO

NA VITUS MATEMBO, MBAMBA BAY

MELI mpya ya mizigo iitwayo Mv. Njombe imetia nanga kwa mara ya kwanza katika bandari ya Mbamba Bay tangu kukamilika kwa ujenzi wake uliofanyika katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela mkaoni Mbeya. Meli hiyo itafanya safari zake katika Ziwa Nyasa. 

Meli hiyo ni moja kati ya ahadi za serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa na rais mstaafu Jakaya Kikwete. Taarifa zinasema meli hiyo itafanya safari zake katika ziwa hilo ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo mbalimbali ya wafanyabiashara ambao walikuwa wakipata shida ya usafiri wa mizigo.
Aidha, imeelezwa kuwa kuanzia wiki ijayo meli nyingine mpya ya abiria iitwayo Mv Ruvuma nayo itaanza safari zake katika ziwa Nyasa. 



JE WAJUA?



Kulala kwa muda mrefu kunasababisha  upweke. Utafiti unaonyesha kuwa watu wapweke wanatumia muda mwingi wakiwa kitandani licha ya kujua hatari zinazotokana hali hiyo. Upweke husababisha kudhani kitandani ni sehemu muhimu zaidi hata kama wakiwa hawana uchovu.

KITONGOJI FEKI CHAGUNDULIKA NDANI YA HIFADHI NYASA

NA ALBANO MIDELO, NYASA

NYUMBA 25 zilizokuwa na kaya 65 ambazo zilijengwa katika hifadhi ya msitu milima ya Ruhekei katika Halmashauri ya Nyasa mkoani Ruvuma zimebolewa na kuondolewa ndani ya hifadhi hiyo.

Afisa Maliasili na Utalii wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bugingo Bugingo amesema zoezi la kubomoa nyumba hizo katika hifadhi hiyo limedumu kwa miaka mitatu na kwamba zoezi limefanyika kwa amani na utulivu kwa njia ya kidiplomasia hadi wananchi hao walipoamua wenyewe kubomoa nyumba zao na kuondoka hifadhini mwezi Agosti 2017.

BASI LA KISUMAPAI LAPATA AJALI NANGOMBO





Basi la kampuni ya Kisumapai lenye namba za usajili T 606 CTY   linalofanya safari zake  kutoka Songea kwenda Mbamba Bay, Liuli hadi Mango wilayani Nyasa limepata ajali mapema leo katika kijiji cha Nangombo wakati likitokea Songea kuelekea Mbamba Bay.
Taarifa inasema kuwa abiria wanne wamefariki dunia kutokana na ajali hiyo, huku wengine wakiwa wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Mbamba Bay.

September 21, 2017

MAELEZO YA NDUGU KABWE Z. RUYAGWA ZITTO (MB), MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE

Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati, 

Mnano tarehe 13 Septemba, 2017 nilipata wito wa kufika mbele ya Kamati yako kutoa ushahidi wa masuala mbalimbali. Nilipata wito husika saa nane na dakika 40 mchana, nikitakiwa kufika mbele ya kamati yako, hapa Dodoma saa saba mchana siku hiyo hiyo. 

Nililetewa wito huo na RCO Mkoa wa Kigoma nikiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kigoma Ujiji. Sikuweza kufika, isingewezekana katika mazingira hayo niwe na uwezo wa kusafiri kutoka Kogoma na kufika mbele ya kamati yako hapa Dodoma. Kwanza muda ulishapita, lakini hata taratibu za kiusafiri pamoja na umbali kati ya Kigoma na Dodoma hazikuwezesha Jambo hilo.
 
Siku iliyofuata nilipata ajali, ambapo nyumba yangu iliwaka moto wakati nikiwa njiani kwenda Nairobi kumuona mbunge mwenzetu mgonjwa, ndugu Tundu Lissu. Jana tarehe Septemba 20, 2017 nikiwa natokea Kigoma ili kuja kwenye Kamati nilikamatwa na Polisi ili kufikishwa mbele ya Kamati yako.
Leo nimefika mbele yenu na nitajibu wito wenu kama ifuatavyo:

UJENZI WA UKUTA MKOANI MANYARA

PICHANI:  Meja Jenerali Michael Isamuyo atua Mererani, Mkoani Manyara kukagua maeneo ambayo ukuta utajengwa kwa ajili ya ulinzi wa madini.


Wananchi wakiangalia Helikopta ya JWTZ iliyomleta meja jenerali Michael Isamuhyo kusimamia ujenzi ukuta wa eneo la vitalu A hadi D katika machimbo ya Tanzanite ,Mirerani.

PICHA KWA HISANI YA; Innocent Vitalis Inno

SIDHANI KAMA UTU UMEZINGATIWA HAPA.



NA DK. RICHARD MBUNDA

MOJA ya misingi mikuu ya tanu na ccm ni kujali utu wa binadamu. Kamati ya Haki, na Maadili ya Bunge imeshindwa kumhoji Mh. Saed Kubenea baada ya kujiridhisha kwamba hali yake ya afya sio nzuri. Mh kubenea amepelekwa Hospital ya bunge baada ya kamati kuona afya yake sio nzuri.

Kamati hiyo imesema Kubenea ataitwa tena kuhojiwa baada ya kujiridhisha kuwa afya yake imeimarika. Ikumbukwe jana jeshi la polisi lilimtia nguvuni Mh. Kubenea akiwa hospital ya Aghakhan ambako alikuwa anapatiwa matibabu.

TUNAJENGA NCHI YA AINA GANI?

KWANINI MAJAJI WANAVAA MAWIGI?



Kwa wenye taaluma mjadala huu unafaa. Kuna mengine pia yamesema, mfano majina ya Victoria Falls, Ziwa Victoria na kadhalika. Makala hayo yalichapwa kwenye gazeti la THE CITIZEN toleo la Jumatano, Septemba 20, 2017. 

Swali linabaki kwanini Majaji huvaa mawigi hadi sasa wakati ni ishara ya ukoloni? Kwa mujibu wa gazeti hilo Wigi moja hugharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 6,500.