Na
Markus Mpangala, Dar es salaam
Angola
imechapwa magoli 2-1 na Cape Verde, taifa ambalo taifa linalokadiriwa kuwa na
idadi ya watu 500,000 tu kulingana na sense zao. Cape Verde imeingia robo fainali
huku kocha wake, Lucio Antunes akiongeza sifa katika kazi yake ya ukocha. Ingawa
nahodha wake Fernando Neves alijifunga bao la kwanza, lakini aliongoza vema
kikosi chao kuishinda Angola kisha kutinga robo fainali. Ni mafanikio makubwa
kwao.
Cape
Verde inashiriki michuano ya mataifa ya afrika yanayoendelea nchini Afrika
Kusini. Kama tujuavyo michuano hii ilitakiwa kufanyika nchini Libya, lakini
kutokana na matatizo ya kisiasa yaliyotokea nchini humo yalisababisha
majadiliano baina ya chama cha soka cha Afrika kusini na kile cha Libya hivyo
kubadilisha michuano.
Kocha wa Cape Verde, Lucio Antunes |
Kimsingi
Afrika Kusini ilitakiwa kuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka 2015, hivyo basi
kwakuwa imekuwa mwenyeji mwaka huu basi michuano ijayo itafanyika nchini Libya. Tukiitazama
Cape Verde inayoshiriki michuano hiyo ikiwa na wachezaji wengi vijana
wameonyesha soka safi ambalo liliwafanya waweze kufuzu kwa michuano hiyo.
Cape
Verde imetinga fainali hizo ikiwa na kumbukumbu ya kuisambaratisha Cameroon kwa
mabao 4-0 wakati wa kuwania kufuzu kwa AFCON. Kwa sasa wengi wanaitazama Cape
Verde kama somo la kuendeleza soka. Idadi
ndogo ya watu, kujiamini, kujua soka, lakini imejikuta ikikosa jambo moja tu
uzoefu wa mashindano ya kimataifa kama AFCON. Pambalo la kwanza la Cape Verde
lilikuwa baina yao na wenyeji Bafana Bafana. Pambano
hilo lilimalizika kwa suluhu ya kutofungana hali ambayo iliibua maswali kwa
wadau wa soka wa kote afrika hususani wenyeji waafrika kusini.
Matokeo
ya pambano hilo ilimlazimu kocha wa Afrika kusini, Gordon Ingesund kufanya
mabadiliko katika kikosi chake. Awali alimweka benchi mshambuliaji hatari
Katlego Mphela na kumwanzisha Majoro hali ambayo iliwakuta wakishindwa
kufurukuta mbele ya ngome ya Cape Verde inayoongozwa na nahodha Neves na T. Varela.
Pambano
la kwanza kwa Cape Verde lilionyesha ushahidi kuwa ilijiandaa kwa AFCON mwaka
huu na ilipania kufanya vema. mpaka sasa Cape Verde wamejikusanyia pointi
mbili, wakiwa nyuma kwa pointi mbili kutoka kwa vinara Afrika kusini. Cape
Verde ilitoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Morocco, hivyo kushika nafasi ya pili.
Huku Morocco ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi mbili na bao moja baada
ya kutoka suluhu na Angola.
Aidha,
pambano la pili Afrika Kusini iliichapa Angola kwa mabao 2-0, huku mshambuliaji
Siyabongwa Sangweni wa Afrika Kusini akiibuka shujaa kutokana na mchezo mzuri
uliomfanya apachike bao la kwanza. Afrika
kusini iliingia pambano la pili ikimwanizhs beki wake hodari Tsepo Masilela
ambaye alikosekana kwenye pambano la kwanza. Hali hii ilimsaidia sana nahodha
wao Khumalo kucheza kwa kujiamini na kuongoza jahazi la nchi hiyo kwa ufanisi.
Lakini
kwa Cape Verde ni wazi imeingia kwenye michuano hii ikielewa kuwa ni sehemu ya
kujifunza licha ya kushindana kwa dhati. Washambuliaji wake Platini, Ryan
Mendes wamekuwa kivutio kwa mashabiki wa soka wanaoifuatilia timu hiyo. Ryan
Mendes akicheza kama shambuliaji wa pili katika mfumo 4-3-3, ameng’ara sana
kutokanana kujaliwa kipaji kikubwa cha soka. Platini licha ya kuwa mshambuliaji
mwenye kipaji anakabiliwa na ukosefu wa stamina ambayo ingelimwezesha kufanya
maajabu mbele ya lango la adui.
Kwa
upande wa kushoto beki Nivaldo anaonekana kucheza kwa utulivu lakini anaoksa
kasi ya mchezo. Yeye ni beki aina ya Timothee Atouba, wanaocheza soka la
taratibu sio kasi kasi kama Essou Ekotto. Lakini
moja ya mabeki wanavutia kuwatazama jinsi wanavyoshughulikia washambuliaji ni
nahodha wa Cape Verde, Neves na
Gege ambaye ni beki wa kulia wa timu hiyo.
wachezaji wa Cape Verde wakishangilia |
Wanacheza
soka la nguvu na vipaji. Wanajua namna ya kukabiliana na washambuliaji hatari
kama Belhanda wa Morocco, mawinga hatari kama Siphiwe Tshabalala wa Afrika kusini. Kila
unapoitazama Cape Verde ikitandaza soka, utaona kwua inao vijana wanaojiamini
sana, na wanajua kucheza soka. Mpangalio wao wa mashambulizi mara nyingi
hutegemea kasi ya Ryan Mendes, ambaye amekuwa mchezaji kivutio zaidi na mwenye
kilifahamu lango la adui kwa ufasaha.
Pia
Cape Vaerde inayo bahati moja kubwa, viungo Soares na Mendes wake wanajua
kupiga mashuti makali wakiwa na lengo la kujaribu kufunga. Mashuti
hayo yanaweza kulenga goli (on target) au kutoka nje ya goli(off target) lakini
jambo la msingi wanajaribu kutuonyesha kile walichonacho katika soka. Kwenye
safu ya ushambuliaji Platini na Tavares wamekuwa tishio kwa kiwango cha
kuridhisha, lakini wanaosa uzeofu tu.
Tavares
anatumika kama mshambuliaji wa kupambana na mabeki, huku Platini akiwa
mshambuliaji wa pili maalumu wa kupachika mabao. Ni sababu hii inaonekana timu
pinzani zinamfanya rafu mbaya sana Platini kuliko mchezaji mwingine yeyote wa
Cape Verde. Kila
dakika wanayocheza dimbani wanavutia, wanaburudisha na kujenga taswira mpya ya
soka baada ya vigogo kama Cameroon na Senegal kukosekana kwenye michuano hii.
Kwa watanzania wanaikumbuka Cape Verde iliyotuchapa mabao 2-1 wakati Taifa
Stars ilipokuwa ikinolewa na Marcio Maximo.
Ni
wazi wakati ule Cape Verde nayo ilikuwa kwenye kipindi cha mpito cha
kujitengenezea njia ya mafanikio kisoka. Hatimaye mwaka huu wanashiriki AFCON,
na wametuonyesha kuwa vipaji, kujiamini na kupangilia mambo ni msingi mkubwa wa
mafanikio. Jambo
lililo wazi na kufurahisha ni kwamba mfumo wa Cape Verde wa 4-3-3 uko wazi sana
na unaonekana kwa uwazi ambao timu pinzani zinaweza kuichapa mabao mengi.
Lakini Cape Verde wana nidhamu sana katika mchezo. Wanajua
soka, wanajiamini lakini safu ya ulinzi inahitaji uzoefu zaidi. Platini
anahitaji stamina, Mendes atakuwa bonge la kiungo siku za mbele. Tujifunze, na
ku-graduate.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako